Sunday, August 23, 2009

JUMA 20 NA NDOTO ZA HOLLYWOOD


Inawezekana ikawa ni ndoto kwa baadhi ya vichwa vya watu ambao watasikia hii.
lakini mkali wa ngoma ya "June july" Juma Malhalass Mohamed (JUMA20 )kutoka visiwani hapa amesema kua,
moja kati ya vitu anayoviwaza sasa katika maisha yake ni kua katika Jiji la wasanii,waigizaji,waongozaji na mastaa
wa kimarekani la HOLLYWOOD huko Carlifornia!
akichonga na ZC Mkali huyo amesema kua kinachomsukuma kuamini kua ipo siku atakanyaga ardhi za huko ni
kutokana na kipaji chake cha kuigiza sauti (Vocal mimic) ambacho kimeanza kumzolea umaarufu Visiwani hapa na Tanzania kwa ujumla!

Juma20 ambae pia ni Mshindi wa tunzo kubwa kabisa ya mwanamuziki Bora wa mwaka muziki wa kizazi kipya visiwani Zanzibar
amesema kua sambamba na hilo la kua na kipaji, pia ana nia ya kua mzanzibar wa mwanzo kuweza kuishi katika jiji hilo la maraha duniani

"Sijajua ni lini na vipi ndoto zangu zinaweza kutimia, lakini naamini ipo siku nitakua ndani ya Hollywood,Nataka kua muongozaji wa filamu na
mtaalamu wa sauti" alisema mwanamuziki huyo ambae ni mbunifu wa matangazo wa kulipwa na kampuni ya Zanzibar Media Corporation
Iwapo kweli ndoto za Juma20 zitatimia,huenda akawa Mtanzania wa Tatu kupenya ndani ya jiji hilo la ma camera kila chochoro akitanguliwa na mwanadada T.K aliyekua mtangazaji wa kituo cha luninga maarufu cha Channel 5 (kwa sasa E.A tv) na mwanadada Mange Kimambi ambae ni mwanamitindo Mtanzania mzaliwa wa Dubai..

No comments: