Wednesday, December 22, 2010
ZIFF KUSABABISHA ZNZ MKESHA WA MWAKA MPYA
Ndugu zetu wadau wa kiwanda cha filamu Tanzania, Zanzibar International Film Festival (ZIFF) inapenda kuwataarifu kuwepo kwa ZIFF Min-Festival itakayofanyika Ngome Kongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 31/12/2010 hadi 2/01/2011, itakua ni Tamasha dogo la siku 3 katika kutoa muamko kwa Tamasha kubwa la ZIFF lijalo (2-10 Julai, 2011).
Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake ili kuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili litaonesha filamu 6 za Kitanzania na filamu 2 bora kati ya hizo zitaenda kuoneshwa katika Tamasha kubwa la filamu Afrika - FESPACO huko Burkina Faso.
Kama ilivyo ada ya Tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi, tutakua pia na makundi ya muziki na wakati huu kundi zima la THT litafanya maonesho kwa siku zote tatu, watakao kuwepo ni Mwasiti, Marlaw, Mataluma, Amin, Barnaba, Pipi, THT Dancers na wengineo. Kwa habari zaidi tembelea www.ziff.or.tz
Tunapenda kuwakaribisha wadau wote na waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi wa habari utakaofanyika katika ukumbi wa Habari - Maelezo, Dar es Salaam, kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi kesho Jumatano, tarehe 22/12/2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment