Monday, December 14, 2009
Lile bifu la wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohammed ‘TID’ na mwenzake Shabani Katwila ‘Q-Chiller’ lililoripotiwa hivi karibuni, limechukua sura mpya baada ya soo lao kutinga polisi.
Taarifa zilizotufikia zimedai kuwa, bifu la wawili hao limefika polisi baada ya juzi kati Q-Chiller kuanza kumsaka mwenzake huku akiwa na silaha.
Akilonga na DHW, Meneja wa TID Khamisi Dakota alisema kuwa, Desemba 8 mwaka huu, akiwa maeneo ya Magomeni, Q- Chief alimvamia akiwa na wenzake wanne na kuanza ‘kumjazia inzi’ huku akimuuliza aliko TID.
Hata hivyo, kutokana na mazingira ya kutokuelewana kati ya wawili hao, inadaiwa Q-Chiller alianza kumsemea mbovu Dakota na mwishowe kuchomoa kisu na kutaka kumchoma.
Kufuatia hali hiyo, Dakota alikwenda moja kwa moja kuonana na TID ambapo walishauriana kulifikisha suala hilo polisi ambapo walikwenda kituo cha Magomeni na kufungua jalada la kesi lenye namba Mag/RB/22117/09 kutishia kuua kwa kisu.
Kumbuka kuwa tayari Q chila alishatangaza wazi kwenye kituo kimoja cha Tv hapa nyumbani eti Tid amemrogaa. Amemfanyia mambo ya kiuswahili … lakini chanzo cha haya yote ni mkwanjaaaa.. Q chila alikuwa akishutumu juu ya malipo aliokuwa akipata wakati walipokuwa ndani ya Bend yao Top Band kabla ya kujitoaaa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment