Sunday, December 27, 2009

NANI ATASHINDA MILLION MBILI TASILIM ?


Mshindi wa mpambano wa kumtafuta mfalme wa jukwaa katika tamasha lililopewa jina la ˜Hip Hop Battle King of Stage anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh milioni mbili.

Mchujo wa kuwapata washindi ambao watashindana mwezi machi katika fainali utafanyika siku ya sikukuu ya mwaka mpya Januari mosi kwenye ufukwe wa Coco beach, ambapo kiingilio kitakuwa ni sh 5000.

Akichonga na The Crush kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga Masoud Kallapina amabye ndiye anayeratibu shindano hilo alisema mshindi wa pili atapata fursa ya kurekodi albamu nzima katika studio ya 41 record na watatu atarekodi albamu nzima kwenye studio ya Kikosi record na mshindi wanne na watano watarekodi nyimbo moja moja kila mmoja Kikosi record.

Alisema pia kutakuwa na shindano la Freestyle ambapo watakaoshiriki katika shindano hilo ni Dogo sajo, Niki mbishi, Godzillah, Lufunyo na Rage.

Huu mpambano wa kumaliza ubishi wa nani mkali wa Hip Hop Tanzania

No comments: