Tuesday, December 22, 2009

TATIZO LA UMEME ZNZ KIZAAA ZAAA WAZIRI ASEMA SI CHINI YA MWEZI MOJA NDIO UPO UWEZEKANO WA KURUDI


Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja itaendelea kukosekana kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kuripuka kwa kifaa kingine cha kugawia umeme katika kituo cha Fumba.
Akizungumza na wandishi wa habari waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema hitilafu hiyo imetokea wakati mafundi walipokuwa wakijaribu kurejesha huduma hiyo iliyokosekana kwa kipindi cha wiki mbili.
Amesema kifaa kilichoharibika cha Spliter hakiko madukani na kinahitaji kutengenezwa, lakini kutokana na wakati huu wa kusherehekea siku kuu ya Krismas na mwaka mpya utengenezaji wa kifaa hicho utachelewa.
Hivyo amesema uwezekano wa kurudi tena huduma ya umeme kwa kipindi cha mwezi mmoja ni mdogo sana Aidha waziri Mansour amewataka wananchi kuendelea kuwa na moyo wa subira huku serikali ikiendelea na juhudi za kurejesha huduma hiyo muhimu
Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja ilikatika Desemba 10 mwaka huu baada ya kuripuka njia ya kupitishia umeme katika kituo cha kupokelea umeme kutoka Tanzania bara cha Fumba
Bonyeza hapa kumsikiaa Waziri akieleza tatizo la umeme (Waziri)

No comments: