Wednesday, December 16, 2009

AY ANAKUJA KUFUNIKA NA PINI LAKE JIPYAA ( KINGS AND QUEEN)



Mambo vipi?
Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa katika video yangu mpya inayoitwa KINGS AND QUEENS niliyomshirikisha JOKATE & AMANI kutoka KENYA.Wimbo umetayarishwa na na Super Producer HERMY B ndani ya Studio ya B.Hitz Music Group na kufanyiwa video na OGOPA DEE JAYS toka Kenya.Video ilifanyika Jijini Nairobi na itaanza kuruka wiki ijayo MTV BASE na vituo vingine ndani ya Afrika Mashariki.
Wimbo huu nimejaribu kufikisha fikra zangu kuwa MWANAMKE WA KIAFRIKA NDIE BORA KABISA NA NAJISIKIA FAHARI SANA KUZALIWA NAO NDANI YA BARA MOJA.
Kama nilivyosema TUNAUFUNGA MWAKA NA KUUFUNGUA NA MZEE WA COMMERCIAL basi subirini mambo makubwa toka kwa MZEE WA COMMERCIAL AMBWENE YESSAYAH MWENYE KIU YA KUWAKILISHA TANZANIA NA AFRIKA YA MASHARIKI KWA UJUMLA KATIKA ANGA ZA MBALI.
Pamoja sana

No comments: