Sunday, December 20, 2009
MZEE ZAHIR ALY ZORO AKAMUA NA VIJANA BONGO FLAVA
Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Zahir Ally Zorro, katika kuonyesha ukomavu ameingia studio na nyota wa bongo fleva nikimaanisha Mr. Blue & Baby Boy na kutengeneza kibao kikali kitakachokuwa kwenye miondoko ya Hip Hop.
Mzee Zorro amefurahi sana kufanya kazi na vijana wake lakini amefurahishwa zaidi na aina ya muziki anaokwenda kucheza. Anapenda hip hop na anaamini ataweka ladha ya aina yake katika nyimbo hiyo alisema.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mkongwe huyo kushirikiana na vijana wa bongo fleva, kwani aliwahi kufanya kazi pamoja na nyota mwingine wa Hip hop Farid Kubanda katika kibao kilichoitwa Ripoti za Mtaani.
Zahir hivi sasa anatamba na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Barua pepe wakati Mr. Blue na Baby Boy nao wanafanya vizuri na nyimbo zao walizotoa hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment