Wednesday, March 31, 2010

T i D AJITOA KWENYE KILI AWARDS

SIWEZI KUSHIRIKI


Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:
1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwene same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!
3.Kwa sababu hizi ambazo mimi naona kwangu hazinijengi sioni sababu ya kuwepo kwenye TUNZO hizi tena kwani sidhani kama ni wakati wa kuwaangusha mashabiki wangu ambao natumia muda mwingi na effort binafsi bila ya mdhamini kuwaunganisha na muziki wangu basi nisameheni kama nimewakosea lakini hainisaidii chochote endeleeni na hao mnaowapa kila category i will never stop making good music for my country surely i wont,i was born to do THIS,.. THANKS.

Comment

Anonymous Anonymous said...

HUNAGA MAGAGA TID..JELA IMEKUWEHUSHA
HALAFU UNA LAKO NA HIZI TUZO
HUNA SHUKURANI..ULILALAMIKA ZINAOTA KUTU, MARA ZINAVUNJIKA, MARA ZINAMEGEKA
ONA SASA UNATAKA ZOTE UPEWE WEWE

Anonymous said...

tid nawe huwachi?
huo ustaa haujakutosha bado
mbona hata wasanii wakubwa wakubwa wa kimarekani huwa wanakosa tuzo kubwa kubwa na hawalalamiki?

sio kila siku jumaapili bwana..
wewe chukulia kama kitu cha kuenjoy usiku mmoja tu tu.
au unataka kupata msosi wako kwa kitu kama tuzo?
huumwi wewe?

BY MSEMA UKWELI..

Anonymous said...

tumzo ni hiari ya mtoaji kukupa au kutokupa acha mashauzi tid
kwani lazma kila mwaka upewe tuzo zote

Anonymous Anonymous said...

acha mashauzi tid...tunzo ni hiari ya mtu kukupa au kutokupa...
huna haja ya kulalamika
kama unafanya vizuri kweli mashabiki wenyewe watakutetea kupitia mitandao na vyombo vya habari
kwani unataka zote upewe wewe
au kila siku upewe wewe?

April 7, 2010 12:25 PM

Tuesday, March 30, 2010

RICKY MARTIN AKIRI YEYE NI CHOKO


Baada ya utata wa muda mrefu . Rick amekiri yeye ni choko .. Ameandika hivi kwenye blog ya kwake mwenyewee ---------

A few months ago I decided to write my memoirs, a project I knew was going to bring me closer to an amazing turning point in my life. From the moment I wrote the first phrase I was sure the book was the tool that was going to help me free myself from things I was carrying within me for a long time. Things that were too heavy for me to keep inside. Writing this account of my life, I got very close to my truth. And this is something worth celebrating.

Many people told me: “Ricky it’s not important”, “it’s not worth it”, “all the years you’ve worked and everything you’ve built will collapse”, “many people in the world are not ready to accept your truth, your reality, your nature”. Because all this advice came from people who I love dearly, I decided to move on with my life not sharing with the world my entire truth. Allowing myself to be seduced by fear and insecurity became a self-fulfilling prophecy of sabotage. Today I take full responsibility for my decisions and my actions.

If someone asked me today, “Ricky, what are you afraid of?” I would answer “the blood that runs through the streets of countries at war…child slavery, terrorism…the cynicism of some people in positions of power, the misinterpretation of faith.” But fear of my truth? Not at all! On the contrary, It fills me with strength and courage. This is just what I need especially now that I am the father of two beautiful boys that are so full of light and who with their outlook teach me new things every day. To keep living as I did up until today would be to indirectly diminish the glow that my kids where born with. Enough is enough. This has to change. This was not supposed to happen 5 or 10 years ago, it is supposed to happen now. Today is my day, this is my time, and this is my moment.

These years in silence and reflection made me stronger and reminded me that acceptance has to come from within and that this kind of truth gives me the power to conquer emotions I didn’t even know existed.

What will happen from now on? It doesn’t matter. I can only focus on what’s happening to me in this moment. The word “happiness” takes on a new meaning for me as of today. It has been a very intense process. Every word that I write in this letter is born out of love, acceptance, detachment and real contentment. Writing this is a solid step towards my inner peace and vital part of my evolution.

I am proud to say that I am a fortunate homosexual man. I am very blessed to be who I am.

Duu? Huwezi amini jamaa ana watoto mapachaa. wawili aliowapata mwaka 2008
Kumbe duuu? anakula pipi ya kijiti kama Paris Helton.

Anonymous said...

SIO YEYE TU LISTI HII HAPA:

NE-YO

ENRIQUE EGLESSIAS

JUSTIN TIBERLAKE (Alipokua nsync)

LILL FIZZ

By msema kweli

Tuesday, March 23, 2010

ZANZIBAR MUSIC AWARDS 21/5/2010


Baada ya kimya cha muda mrefu hatimae manager wa zenji entetainment ndg Seif Mohammed Seif Khatib jana amekata ukimya baada ya kutangaza rasmi tarehe ya tunzo za mwanamuziki bora wa Zanzibar "Zanzibar Music Awards" kwa mwaka huu 2010. Ndg Seif aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na Dj Side ndani ya Zenjfm kwenye kipindi cha bongo brain majira ya usiku wa jana.Ameitangaza tarehe rasmi ya tunzo hizo ni 21/05/2010 katika ukumbi wa hoteli ya bwawani.Akiongeza ndg Seif alisema mwaka huu music award imejizatiti kwa kufanya mambo makubwa na mabadiliko kadhaa ambayo yanaweza yakapunguza lawama kwa washiriki,pia alieleza kuwa mwaka huu tunzo hizo zitasindikizwa na wasanii kutoka nje ya Tanzania hata hivyo hakuwa tayari kuwataja ni wasanii gani .Zanzibar Music Award ilikuwa ifanyike mwezi wa tatu lakini tatizo la umeme lililoikumba manispaa ya Unguja kwa miezi mitatu limepelekea kusogezwa mbele,tamasha hili ni pekee linalowatunuku wasanii mahiri wa kizanzibar kila mwaka.Tunzo za mwaka huu zitakuwa ni tunzo za tano tokea lilipoanzisha na kampuni ya Zanzibar Media Corporation .

Post a Comment On: The crush
Anonymous said...

nawatakia kila la kheri wanamuziki na wasanii wote ambao watakua nominated katika tunzo za mwaka huu.
bila kusahau mashabiki watoe support kubwa katika kufanikisha tukio hili tukufu
JUMA20 (FORMER bEST ARTIST OF 2009 WINNER)

Post a Comment On: The crush
Anonymous said...


Hongera kwa waandaji wa tunzo hizi kwa kufikisha miaka mitano.
mungu azibariki na muzidi kuwatoa wenetu wa kizanzibari

MAYASSA SAID. BELGIUM

Post a Comment On: The crush

Anonymous said...

nimepata fununu kwamba baadhi ya wasanii ambao kimsingi hawana confidance wamejitoa katika ushiriki wa tunzio hizi kwa sababu zisizo nam msingi jee kuna kitu gani kinaendelea hapa

SULTAN MOHAMED. Bububu

Post a Comment On: The crush

Anonymous said...

HONGERA KWA MTAA WA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR KWA KUONGOZA KWA KUTOA WANAMUZIKI BORA. KIMSINGI TUNZO NYINGI ZILIELEKEA MITAA HIYO KUPITIA BABY J NA JUMA20...
HONGERA MITAA YA MAGOMENI KWA KUONGOZA KUCHUKUA TUNZO ZA TAARAB

MASOUD MASOUD. Kigamboni Zanzibar.

TAMASHA LA NCHI ZA MAJAHAZI ZIFF KIFANYIKA JULY 10


Mpango mzima wa tamasha la 13 la nchi za majahazi tayari umeshatangazwa rasmin . Shuhuli nzima itakuwa tarehe 10 hadi 18 mwezi wa 7 mwaka huu 2010.. Kaeni tayari na kujiandaa kushiriki kwenye tamasha hili. Mwaka huu takriban filam nyingi sana zinatarajiwa kuonyeshwa . ambazo zimeshinda tuzo mbali mbali katika nchi tofauti. Litakuwa ni Tamasha la aina yake.

The annual Zanzibar International Film Festival is the biggest cultural event on the island and takes place in various historical locations in Stone Town on the island of Zanzibar. During the nine-day festival, visitors can expect a warm introduction to the island's unique cultural heritage through not only film but art, crafts, literature, film, dance, performing arts and music. Events also take place on the nearby islands of Unguja and Pemba. Its on 10 til 18 July 2010 .. You are most welcome

Friday, March 19, 2010

OFSIDE TRICK WAENDELEA KULA BATA


Off side warejea kutoka ughaibuni na kwa sasa wapo mkoani Tanga wakipiga show mbili moja Tanga town na ya pili wanapiga Korogwe.
Kiufupi jamaa walikwenda Dubai ambapo walifanikiwa kufanya show mbili ambazo zilikamata watu ile mbaya na baadae walikwenda Oman ila hawakufanikiwa kufanya show sababu ikiwa ni kwisha kwa visa zao ndipo waliporejea nyumbani ila machizi wamedai watakwenda tena Ughaibuni siku zijazo kwani bado watu wana hamu nao.
Wamesema hayo kupitia mawimbi ya 96.8 pale walipofanya interview na mtu mzima Rama B katika kipindi cha Friday zenj night siku ya ijumaa 19.3.2010 majira ya saa 2:30 usiku.
Mwisho kabisa wanajiandaa kufanya uzinduzi wao hapa Zanzibar katika ukumbi wa Ghmkhana 17.3.2010.
Jamaa wanakula mashavu ya kutosha kwa sasa.
Big up ila Msijisahau.

BIKIDUDE ANAFUNIKA MBAYAAA



Bibi mwenye sauti ya ajabu na mvuto Bikidude ndani ya miezi hii mitatu ameonekana akitikisha vizuri katika anga za mziki wa kizazi kipyaa. Katika hali isioaminika Bikidude ameshirikishwa na kundi la offside trick katika ngoma yao mmpya inayotamba kwa sasa iitwayo Ahmada. Ambayo ipo katika style ya mduara . Bikidude anasikika akighanii katika style za kiaarabu katika ngoma hiyo . Katika hali nyengine ambayo huwezi kuamini mkali wa Hip Hop Bongo Fareed Kubanda aka Fid Q amemshirikisha Bikidude Katika Ngoma inayokwenda kwa jina la Juhudi kwa wasiojiweza ambapo kwa maneno yake mwenyewe Fid Q ngoma hiyo imefanyika katika studio za Jupiter Record ilioko hapa Zanzibar.

“Niliona nimweke Bi Kidude ili kunogesha ladha katika ngoma yangu,kwani sauti yake ni adimu na kila mtu anajuwa kazi yake Bi Mkubwa” alisema Fid Q
Album ya ya Fid inaitwa Propaganda tayari ipo madukani ambapo kuna ngoma 12 zimesimama humo kama Hey Lord (Mzungu Kichaa), Temanoleji, Wananiita King (Nylon wa Manzese Crew), Mama (Bizman), Ripoti za Mtaa (Zahir Zorro), Kila Siku (Q-Jay), Shimo limetema (Ncha Kali na AY),

DOWNLOAD FREE MP3 MUSIC



Enjoy all kind of music just click http://www.magicmuz.com/

If u like my post . just say hi !!! djside_dj@yahoo.com

If U hav any .. u wanna talk with me send me email djside_dj@yahoo.com

NICE WALLPAPER FOR YOUR LAPTOP



Hey!! Let me share this with u. A nice web for nice wallpapers . Just click hire http://www.hdwallz.co.cc/

Thursday, March 18, 2010

INCRESE UR INTERNET SPEED (very simple way)



Follow the step:-

Go to desktop->
My computer-(right click on)->properties->
then go HARDWARE tab->
Device manager->
Now u see a window of Device manager then
go to Ports->
Communication Port(double click on it and Open).
After open u can see a Communication Port properties.
Go the Port Setting:----and now increase ur "Bits per second" to 128000 and "Flow control" change to Hardware.
Apply and see the result..... ...... ....... ENJOY

Don't Forget to Say Thank's if u like my post djside_dj@yahoo.com

Wednesday, March 17, 2010

MATONYA " WANANISINGIZIA NAUZA UNGA"



Baada ya taarifa kuzagaa mitaani hasa kwa wapenzi wa muziki wa bongo fleva kuwa msanii Seif Shaaban a.k.a Matonya amenyongwa baada ya kukamatwa na unga huku wangine wakidai jamaa amekamatwa huko China anasubiri hukumu ya kunyongwa.
Leo Matonya amekata mzizi wa fitna kupitia mawimbi ya 96.8 Zenj fm ndani ya "the crush"
Wakati akifanyiwa mahojiano na mtu mzima Dj Side pamoja na Rama B Matonya amedai huo ni uzushi ambao anazushiwa na watu wasiomtakia mema katika game ya muziki wa kizazi kipya.

Kifupi jamaa alikwenda Brazil kwa mambo yake ya mziki na wakati anarudi alipitia China ambako alinunua vifaa vya muziki kwa ajili ya Bendi yake mpya itakayo itwa Matonya Bendi.
Hata hivyo amesikitika sana na kudai yote hayo yanakuja kutokana na maendeleo yake huku akidai enemies wengi walomzunguka ndio wanamfanyia hao na hii ikiwa ni mara ya tatu kumzushia mambo kama hayo.

Mwisho Tonya amedai kwa hasira anaachia mizigo miwili kwa mpigo abiria chunga mzigo wako akimshrikisha Mr Blue na haki sawa akimshirikisha Mrisho Mpoto. Kaeni mkao wa kula wapenzi wa Matonya. Ili kusikiliza mahojiano hayo bonyeza hapa (MATONYA LIVE ZENJI FM)

NGOMA MPYA YA CHID BENZI

Thursday, March 11, 2010

DOWNLOAD YOUTUBE VIDEOS BY SIMPLY USING T HE "OK" WORD



Hi all....

Download videos from youtube by typing "OK"

yeah,it's not a joke...

type "OK" between WWW. and youtube...

Note::
adding OK will be downloaded in flv format

adding 3.OK will download in 3gp format

adding 4.OK will download in mp4 format

Eg
Dis video link http://www.youtube.com/watch?v=2axRGjAW6bo

so hre we go

http://www.OKyoutube.com/watch?v=2axRGjAW6bo

Done!!

If U like it say Thx to me!!! djside_dj@yahoo.com

Wednesday, March 10, 2010

MJ RECORD KUJIBU SHUTUMA ZA STIGGO


MASTER J AKIWA NA MAKOCHALI NDANI Y A MJ RECORD

Kufuatia tetesi zilizo zagaa Juu ya Instrumental ya ngoma ya Bullet alioimba Quick racka ambayo inadaiwa kwamba Original version yake imetengenezwa na Producer Stigo aliyeko Marekani

Kipindi cha The Crush cha Zenj fm Radio kinachenda hewani kila siku ya juma tatu hadi Ijumaa Saa 8 za mchana hadi 10 leo kilifanya juhudi za kutaka kujua undani wa taarifa hizo kwa upande wa Mj Records studio ambayo ndiyo iliyotengeneza wimbo wa Bullet ulioimbwa na Quick Racka

Mkurugenzi wa Mj Records Master J amesema kuwa kwa sasa hawawezi kuzungumza lolote kuhuisiana na kadhia hiyo kutoka na ushauri wa wakili wao aliyewataka kukaa kimya kwa sasa.

Aidha katika Interview na Dj side kwenye The Crush Master J amesema kuwa kwa sasa wanasubiri kuona hatua zitazochukuliwa na kampuni ya Koch Records ambayo kwa mujibu wa Stiggo ilisema kuwa itawashtaki Mj Records……. Kwa mujibu wa stigoo Koch record ndio studio aliewakabidh beat hiyo. Kwa maana hiyo Stigoo amepeleka malalamiko kuishutumu Koch kwa kuruhusu matumzi ya beat hiyo pasi ya yeye kujua .. Suala la kujiuliza Jeee? Mj wamenunua au vipi? Ndio hivo Mkurugenzi wa Mj Record Master J amesema hawezi kuzungumzia chochote kwa saa mpaka watakapoona Koch record imechukua hatua …. Huu si wakati wa mabishano… Mipasho tuwaachie watu wa taarabu alisikika akisema Master J …

Hata hivyo mkurungenzi huyo amesema kwa sasa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika mziki wa Tanzania. Amesema kwa sasa Tayari washakamilisha Ngoma kama kumi ambazo zote ni za wasanii wenye lebo pale Mj record . Amejigamba kwa kusema watanzania kaaeni mkao wa kula kwani ntaachia ngoma 4 kwa wasanii wenye lebo Mj . na ngoma zote ni moto wa kuotea mbali .

Haya mashabiki mambo ndio hayoo ..

Sunday, March 7, 2010

MAKOCHALI KAIBA BEAT YA BULLET?


Kuna utata mkubwa umejaa kuhusiana na beat aliyotembea nayo Quik Racka Bullet kua beat hiyo imeibiwa Kwa mujibu wa Producer wa S&S record alieko marekan mkali STIGO...amabe Ndie alietengeneza ngoma hiyo... . Haya tuliyajua baada ya kupata email kutok kwa Stigo ambayo ilikuwa ikisema hivi-----
Nilidhani maproducer wa Tanzania wameendelea sana lakini nahisi it was wrong.miaka miwili iliyopita nilitengeneza beat nikaiita Block Running, nikaiuza kwenye lebo moja inaitwa Koch Entertainment iliyoko New York kwa makubaliano ya kuwa lazima kuwa, mtu yeyote atakaeichukua lazima kuwe na jina langu kama mtengenezaji wa beat hiyo.lakkini siku mbili zilizopita nilishtuka sana baada ya rafiki yangu kutoka tanzania kunitumia nyimbo ikiwa na beat ile ile niliyoitengeneza miaka miwili iliyopita!!!! na siku sikia jina langu katika ngoma hiyo nilichiskia ni marcochali tu, nikawapigia Koch Entertainment kuwauliza nini kinaendelea? nao walishangaa kusikia habari hiyo, wakaniambia niwatumie nyimbo hiyo na nimewatumia.wakaniuliza kama nilishawahi kuituma beat Mj records ya Dar-es-salaam? nikasema mi sijawahi!!!

Lakini niliiweka beat kwenye itunes ili watu wainunue na kuitumia kwa ajili ya promotion tu na si kwa biashara, lakini MJ wametumia bila ruhusa kutoka Koch Entertainment na hawakufata makubaliano kwamba atakaetumia lazima kuwe na jina langu kama mtengenaji wa beat hiyo.sina haki yoyote ya kulalamika kwa MJ ila nitakacho fanya nikuwapeleka KOCH mahakamani na wao ndio watadili na Mj records.Ila nitadili na mj kama waliinunua kupitia itunes na kama ndio hivyo kwanini wameitumia ki biashara.

Haya wadau nadhna mnaham kubwa ya kutaka kujua ukweli upo wapi.. Ntajitahid kumtafuta makochali atwambie ilikuwaje?

STANBOI --- UTANIPATA KWENYE WEB KWA SASA!


STANBOI WAKWANZA KWENYE PICHA AKIWA NA J-CO LAURECE NA WILLIUM

Mwana muziki Mtanzanian Anaeishi marekani Anaejulikana kwa jina la Stanboi "The African Child" Ametangaza rasmin kwamba kwa sasa tayari ameshazindua tovuti ya kwake inayoitwa www.stanboi.com. Ambapo katika tovuti hii utapata kujua habari zake na mwenendo mzima wa shughuli zake za kimuziki Kwa sasa mchizi yupo state akisongesha kwenye game Mchizi kwa sasa anamahusioano mazuri sana na wasanii wakubwa kama Omario ,J co na wengineo wengi Kama unakumbuka Stanboi alifanya vizuri sana katika wimbo alishirikishwa na AY uitwao madem wataftaji .. Kwa habari zaid tembelea tovuti yake

Thursday, March 4, 2010

TUMA SMS BURE POPOTE UTAKAPO



Tumia hii link http://for-ever.us/ kwa kutuma sms bure popote duniani. kwa Tanzania mpaka sasa zantel ndio inakubali. kama umependa post yangu sema chochote nitumie email djside_dj@yahoo.com

SEND FREE SMS WORLDWIDE



Hey... Use this link http://for-ever.us/ to Send Free SMS Worldwide Just say thanks if u like my post. send me email djside_dj@yahoo.com