Tuesday, March 23, 2010
ZANZIBAR MUSIC AWARDS 21/5/2010
Baada ya kimya cha muda mrefu hatimae manager wa zenji entetainment ndg Seif Mohammed Seif Khatib jana amekata ukimya baada ya kutangaza rasmi tarehe ya tunzo za mwanamuziki bora wa Zanzibar "Zanzibar Music Awards" kwa mwaka huu 2010. Ndg Seif aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na Dj Side ndani ya Zenjfm kwenye kipindi cha bongo brain majira ya usiku wa jana.Ameitangaza tarehe rasmi ya tunzo hizo ni 21/05/2010 katika ukumbi wa hoteli ya bwawani.Akiongeza ndg Seif alisema mwaka huu music award imejizatiti kwa kufanya mambo makubwa na mabadiliko kadhaa ambayo yanaweza yakapunguza lawama kwa washiriki,pia alieleza kuwa mwaka huu tunzo hizo zitasindikizwa na wasanii kutoka nje ya Tanzania hata hivyo hakuwa tayari kuwataja ni wasanii gani .Zanzibar Music Award ilikuwa ifanyike mwezi wa tatu lakini tatizo la umeme lililoikumba manispaa ya Unguja kwa miezi mitatu limepelekea kusogezwa mbele,tamasha hili ni pekee linalowatunuku wasanii mahiri wa kizanzibar kila mwaka.Tunzo za mwaka huu zitakuwa ni tunzo za tano tokea lilipoanzisha na kampuni ya Zanzibar Media Corporation .
Post a Comment On: The crush
Anonymous said...
nawatakia kila la kheri wanamuziki na wasanii wote ambao watakua nominated katika tunzo za mwaka huu.
bila kusahau mashabiki watoe support kubwa katika kufanikisha tukio hili tukufu
JUMA20 (FORMER bEST ARTIST OF 2009 WINNER)
Post a Comment On: The crush
Anonymous said...
Hongera kwa waandaji wa tunzo hizi kwa kufikisha miaka mitano.
mungu azibariki na muzidi kuwatoa wenetu wa kizanzibari
MAYASSA SAID. BELGIUM
Post a Comment On: The crush
Anonymous said...
nimepata fununu kwamba baadhi ya wasanii ambao kimsingi hawana confidance wamejitoa katika ushiriki wa tunzio hizi kwa sababu zisizo nam msingi jee kuna kitu gani kinaendelea hapa
SULTAN MOHAMED. Bububu
Post a Comment On: The crush
Anonymous said...
HONGERA KWA MTAA WA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR KWA KUONGOZA KWA KUTOA WANAMUZIKI BORA. KIMSINGI TUNZO NYINGI ZILIELEKEA MITAA HIYO KUPITIA BABY J NA JUMA20...
HONGERA MITAA YA MAGOMENI KWA KUONGOZA KUCHUKUA TUNZO ZA TAARAB
MASOUD MASOUD. Kigamboni Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:

Post a Comment