Wednesday, March 10, 2010
MJ RECORD KUJIBU SHUTUMA ZA STIGGO
MASTER J AKIWA NA MAKOCHALI NDANI Y A MJ RECORD
Kufuatia tetesi zilizo zagaa Juu ya Instrumental ya ngoma ya Bullet alioimba Quick racka ambayo inadaiwa kwamba Original version yake imetengenezwa na Producer Stigo aliyeko Marekani
Kipindi cha The Crush cha Zenj fm Radio kinachenda hewani kila siku ya juma tatu hadi Ijumaa Saa 8 za mchana hadi 10 leo kilifanya juhudi za kutaka kujua undani wa taarifa hizo kwa upande wa Mj Records studio ambayo ndiyo iliyotengeneza wimbo wa Bullet ulioimbwa na Quick Racka
Mkurugenzi wa Mj Records Master J amesema kuwa kwa sasa hawawezi kuzungumza lolote kuhuisiana na kadhia hiyo kutoka na ushauri wa wakili wao aliyewataka kukaa kimya kwa sasa.
Aidha katika Interview na Dj side kwenye The Crush Master J amesema kuwa kwa sasa wanasubiri kuona hatua zitazochukuliwa na kampuni ya Koch Records ambayo kwa mujibu wa Stiggo ilisema kuwa itawashtaki Mj Records……. Kwa mujibu wa stigoo Koch record ndio studio aliewakabidh beat hiyo. Kwa maana hiyo Stigoo amepeleka malalamiko kuishutumu Koch kwa kuruhusu matumzi ya beat hiyo pasi ya yeye kujua .. Suala la kujiuliza Jeee? Mj wamenunua au vipi? Ndio hivo Mkurugenzi wa Mj Record Master J amesema hawezi kuzungumzia chochote kwa saa mpaka watakapoona Koch record imechukua hatua …. Huu si wakati wa mabishano… Mipasho tuwaachie watu wa taarabu alisikika akisema Master J …
Hata hivyo mkurungenzi huyo amesema kwa sasa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika mziki wa Tanzania. Amesema kwa sasa Tayari washakamilisha Ngoma kama kumi ambazo zote ni za wasanii wenye lebo pale Mj record . Amejigamba kwa kusema watanzania kaaeni mkao wa kula kwani ntaachia ngoma 4 kwa wasanii wenye lebo Mj . na ngoma zote ni moto wa kuotea mbali .
Haya mashabiki mambo ndio hayoo ..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment