Wednesday, March 17, 2010

MATONYA " WANANISINGIZIA NAUZA UNGA"



Baada ya taarifa kuzagaa mitaani hasa kwa wapenzi wa muziki wa bongo fleva kuwa msanii Seif Shaaban a.k.a Matonya amenyongwa baada ya kukamatwa na unga huku wangine wakidai jamaa amekamatwa huko China anasubiri hukumu ya kunyongwa.
Leo Matonya amekata mzizi wa fitna kupitia mawimbi ya 96.8 Zenj fm ndani ya "the crush"
Wakati akifanyiwa mahojiano na mtu mzima Dj Side pamoja na Rama B Matonya amedai huo ni uzushi ambao anazushiwa na watu wasiomtakia mema katika game ya muziki wa kizazi kipya.

Kifupi jamaa alikwenda Brazil kwa mambo yake ya mziki na wakati anarudi alipitia China ambako alinunua vifaa vya muziki kwa ajili ya Bendi yake mpya itakayo itwa Matonya Bendi.
Hata hivyo amesikitika sana na kudai yote hayo yanakuja kutokana na maendeleo yake huku akidai enemies wengi walomzunguka ndio wanamfanyia hao na hii ikiwa ni mara ya tatu kumzushia mambo kama hayo.

Mwisho Tonya amedai kwa hasira anaachia mizigo miwili kwa mpigo abiria chunga mzigo wako akimshrikisha Mr Blue na haki sawa akimshirikisha Mrisho Mpoto. Kaeni mkao wa kula wapenzi wa Matonya. Ili kusikiliza mahojiano hayo bonyeza hapa (MATONYA LIVE ZENJI FM)

No comments: