Friday, March 19, 2010

BIKIDUDE ANAFUNIKA MBAYAAA



Bibi mwenye sauti ya ajabu na mvuto Bikidude ndani ya miezi hii mitatu ameonekana akitikisha vizuri katika anga za mziki wa kizazi kipyaa. Katika hali isioaminika Bikidude ameshirikishwa na kundi la offside trick katika ngoma yao mmpya inayotamba kwa sasa iitwayo Ahmada. Ambayo ipo katika style ya mduara . Bikidude anasikika akighanii katika style za kiaarabu katika ngoma hiyo . Katika hali nyengine ambayo huwezi kuamini mkali wa Hip Hop Bongo Fareed Kubanda aka Fid Q amemshirikisha Bikidude Katika Ngoma inayokwenda kwa jina la Juhudi kwa wasiojiweza ambapo kwa maneno yake mwenyewe Fid Q ngoma hiyo imefanyika katika studio za Jupiter Record ilioko hapa Zanzibar.

“Niliona nimweke Bi Kidude ili kunogesha ladha katika ngoma yangu,kwani sauti yake ni adimu na kila mtu anajuwa kazi yake Bi Mkubwa” alisema Fid Q
Album ya ya Fid inaitwa Propaganda tayari ipo madukani ambapo kuna ngoma 12 zimesimama humo kama Hey Lord (Mzungu Kichaa), Temanoleji, Wananiita King (Nylon wa Manzese Crew), Mama (Bizman), Ripoti za Mtaa (Zahir Zorro), Kila Siku (Q-Jay), Shimo limetema (Ncha Kali na AY),

No comments: