Friday, March 19, 2010
OFSIDE TRICK WAENDELEA KULA BATA
Off side warejea kutoka ughaibuni na kwa sasa wapo mkoani Tanga wakipiga show mbili moja Tanga town na ya pili wanapiga Korogwe.
Kiufupi jamaa walikwenda Dubai ambapo walifanikiwa kufanya show mbili ambazo zilikamata watu ile mbaya na baadae walikwenda Oman ila hawakufanikiwa kufanya show sababu ikiwa ni kwisha kwa visa zao ndipo waliporejea nyumbani ila machizi wamedai watakwenda tena Ughaibuni siku zijazo kwani bado watu wana hamu nao.
Wamesema hayo kupitia mawimbi ya 96.8 pale walipofanya interview na mtu mzima Rama B katika kipindi cha Friday zenj night siku ya ijumaa 19.3.2010 majira ya saa 2:30 usiku.
Mwisho kabisa wanajiandaa kufanya uzinduzi wao hapa Zanzibar katika ukumbi wa Ghmkhana 17.3.2010.
Jamaa wanakula mashavu ya kutosha kwa sasa.
Big up ila Msijisahau.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment