Monday, August 23, 2010
BALOZI WA WAREKANI TZ NDANI YA MJENGO WA ZENJIFM LEO
Balozi wa marekani Alfonso E. Lenherdt’s leo alipata nafasi ya kufika ndani ya mjengo wa Zenjifm na kufanya kipindi maalum . Lengo hasa la kuja Zenjifm ni Kufuatia kauli ya Rais Obama ya Kuipongeza Tanzania , Nae balozi wa marekani Bwana Alfonso ameamua kusisitiza kile alichosema Rais Obama na alipata nafasi ya kufanya mahojiano maalum na Zenj fm Radio ambapo kwanza amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa ujasiri wao wa kupiga kura ya ndio na kusema kuwa siasa za uhasama na chuki zimkufa na kwa sasa wananchi wanachotakiwa kufanya ni kushikamana katika kujenga Zanzibar mpya yenye matumaini kwa vizazi vijavyo.
Katika mazungumzo yake Balozi Alfonso amesema kuwa kura ya maoni itarsaidia sana kudumuisha uhusiano wa muda mrefu uliopo baina ya Marekani na Zanzibar
Sunday, August 22, 2010
LEO KWENYE FACEBOOK YA BENJAMINI WA MAMBO JAMBOS
DORIKA ASEMA ( LEO NAACHIA NGOMA YANGU MPYAA )
DORIKA
Wapenzi wangu leo naachia ngoma yangu mpya.. Ngoma hii nimefanya na kaka moja ambae ni producer wa studio flan.. Unataka kumjua ni nani? unataka kujua mara hii nimetoka vipi? Unataka kujua inaitwaje? usikose kusikiliza Bongo brain leo Juma tatu usiku na Dj side ndani ya Zenjifm Usiku kuanzia saa 3 hadi 5. Naomba maoni yenu mtakapo isikia hiyo ngoma . nimeachia hii kwa ajili ya skukuu ambayo bado siku kadhaa tu. so kaeni mkao wa kula na kitu kipyaa. ni hayo tu !!
LIOYD BANKS AIPA SHAVU TANZANIA
Katika hili pini jipya la mchizi "Any Girl", Lloyd Banks wa G-Unit ameipa shavu nchi yetu Tanzania baada ya kuitaja katika lyrics za ngoma hii , Mchizi anasema "I don’t mind a petty stare, I don’t need a favor, Baby I’m a millionaire, Got a show hoppin outta’ the leer in Tanzania". .. Angalia video chini hapo ujionee..
AVATAR EXCLUSIVE -BEHIND THE SCENES
Aaa jamni hapa tena basi ...the whole thing they used into making this film is amazing, and it shows so much more opportunities in the industry, I mean a whole movie can be done by stunts alone and actors won't have to have their good looks, while we will still be getting an extraordinary end-product. The reality and liveliness of the moves combined with the greatness of the CGI opens up a whole new dimension to the sci-fi/fantasy gender especially, but not only, already looking forwards for Avatar2
Check out Avatar Exclusive -Behind The Scenes
Friday, August 20, 2010
FAN KISS HUU NDO MUDA WAKE WA KULA BATA
Mchizi hii ndo ngoma yake ya kwanza ngoma imetengenezawa pale Jupiter record na Aron name. Katika ngoma hii mchizi amefanya na Baby J ambae ameitendea haki ngoma hii. Juzi nilikuwa studio Jupiter nilikuwa nasikiliza ngoma mpyaa . Pia nilipata kusikiliza ngoma mpya ya Rico singo akiwa na Ay hii ngoma ntaizungumza j4 bt kubwa ni juu ya huyu kijana Fan kiss . I say? amefanya bonge moja la ngoma kuliko hii .Ngoma bado haijapewa jina amefanya na Producer aron. I say ngoma kali sana. Itabamba tuu kuliko hii. Stay tune ntaweka sample hapa uisikie soon tu
FAN KISS KWENY VIDEO TAKE YOU DOWN FT BABY J
Wednesday, August 18, 2010
BERRY BLACK AACHIA VIDEO MPYAA NA MWANA DADA DORICA
Katika hali isio ya kueleweka hatimae berry ameachia video mpyaa inayokwenda kwa jina la Nazila ngoma ambayo amefanya na A T msanii ambae ilikuwa ikisemekana eti wana bifuu ya mdaa mrefu pia akiwa na mwana dada dorica . kama unavyoona hapo juu berry akiwa na A T.... kama unakumbuka kulikuwa na bifu kubwa sana wakati A T alipotimuliwa kutoka kwenye lebo ya Teddy Record . na ikasemekana kuwa wawili hawa ilikuwa haziwivi chungu kimoja. kiasi ikafika hadi kuimbana. Leo tunaona wapo kwenye ngoma moja
Berry akiwa na A T kwenye video yake mpyaa ya Nazira
Mwana dada Dorica akiwa kwenye poz ya camera kwenye video ya Nazira.
Berry akiwa na ma stars kutoka znz kwenye video yake pyaa
Video hii ya Berry imefanywa na Adam juma wa Visual Lab -- Na ngoma hii imefanya na Aron name kutoka pale jupiter record
Sunday, August 15, 2010
RAMBO AJA NA MOVIE MPAYAA THE EXPENDEBALE
Daaa? Jamani Rambo kakusuduia nini hasaa kwenye Hii movie yake mpyaa? Yaani katafuta mastaa watupu .Mtu kama Chwarzenegger? Jet li? Steve Austin? Mickey Rourke na Jason Statham. Yaani ni balaaa. Hapa kasoro Van dame tu amabe pia alipigis sim awemo kwenye hii movie bt mchizi akatole njee. Hii movie Itauza mbayaaaa. Inaitwa The Expendeble. Wiki ndio Imetoka . Yaani ni noma Angalia Trailer yake hapo
Wednesday, August 11, 2010
BIKIDUDE AFUNIKA MBAYA KWENYE VUNJAJUNGU PARTY NA FLAVA DJS
Hapa Bi Kidude anashuka ndani ya gari kutoka Town akiwa na wadau wa Zenj fm Radio na Fleva Djs,kutoka kushoto kwa Bikidude ni mtu mzima Dj Side, kulia ni mwanadada Emy c na nyuma kabisa ni Dj Sam
Pozi la nguvu la Bi kIdude akionesha kuwa na yeye wamo katika mambo ya pozi za picha aliyemuegemea ni Emy C na nyuma hapo ni Aziza Wazir aka Azwii
Nani anasema Bikidude hana nguvu? hapo alikuwa akishuka ngazi kuelekea katika ufukwe wa Kendwa Rocks Hotel ambapo alifanya makamuzi ya ukweli.Pichani hapo kama unavyoona Dj Side alikuwa akiburuzwa
Wameshamaliza ngazi hapo, Bikidude hapo ni mwendo wa kijeshi hataki mchezo katika kazi
Mwendo mdundo kudadadeki
Hawa ni wachina ambao walimpokea vizuri Bi Kidude na kwa mujibu wa maelezo ya Bi Kidude alisema kuwa hao ni wazee wake, sijui alikuwa akimaanisha nini maana hapo kwa mtazamo tuu anaonekana yeye ana umri mkubwa zaidi ya hao aliodai ni wazee wake!!!
Kundi zima la Unyango Band likisubiri kufanya makamuzi katika msosi kabla ya kufanya mambo ya ukweli ukweli katika stage.
Bi Kidude akiwa na wamiliki wa Hoteli ya Kendwa Rocks Mama Nuhu na Omar Kilupi
Jamani Emy c nae wamo katika mambo ya kubugi msondoo?? hapo akiwa na Bi Kidude wakioneshana kazi.
Wamiliki wa Kendwa Rocks na Kundi zima la Unyago Band wakibadilishana mawazo hapo kama unavyoona.
Nani kasema Bi Kidude hana nguvu? huwezi amini huyu Bibi ana nguvu sana kiasi ambacho wengi tulishangaa sana, ona jinsi alivyojifunga ngoma yake hiyo na huku anaitwanga kisawa sawa? kwa kweli huyu ni LEGENDARY OF MUSIC IN ZANZIBAR.
Vijana wa Unyago Band wakionesha vitu vyao hadharani.Mambo yalikuwa kiunyago unyago tuu yaani ni full kufundwa zaidi!!
Hatimaye Bi Kidude alijipatia Handsome wake na kuanza kumfunda kiunyago zaidi.
Non stop music jamani Bi Kidude akiwa kazini hataki masihara kabisa ona jinsi alivyo seriuos na kazi yake amejifunga msondo wake akiendelea na makamuzii!!
Jamani shughuli ni kuchakarika eeehh?? Unyago Band wakichakarika katika kutoa ile kitu roho inapenda kwa mashabiki waliohudhuria katika show hiyo!!Haya na radhi ama kwa hakika zilimwagwa si unaona jamaniii???!!
NIITE 4 SHOW NIZO 4 SHOW BC TENA .
Juzi nilikuwa naongea na nizo 4 show unajua amesemaje kuhusu jina la nizo 4 show? ameniambia kwa sasa anataka watu wa mwite 4 show . Na amenipatia ngoma yake mpya ambayo imetengenezwa na Alan mapigo aka Vampare. pamoja na Producer wake Labi One. au lazizo. Ngoma hiyo inakwenda kwa jina la ngoma ni Cross Boder. Ngoma amefanya na Junior . Nizo ameniambia
lengo lakubadilisha style ya muziki wangu ni kujitofautisha zaidi na ma mc wengine pia kuupeleka music wangu level za kimataifa zaid.nashukuru mwenyezi mungu dalili nzuri zimeanza kuonekana,najivunia kufanya kazi na wanamuziki toka nje ya tanzania.nimeshafanya kazi na JOE KYZE toka congo,amenishirikisha kwenye ngoma yake,nifanya kazi na TIZO mtanzaniaanaefanya muziki southafrica pamoja na wakali toka hapahapa bongo.hiyo kwangu niatua kubwa so naomba shabiki wangu wasaport kwa hiki nachokifanya kwani nina vingi vizuri naitaji kuwapa . Sikiliza The crush siku ya Juma tano Utaisikia pini hii mpyaa ya 4show
Sunday, August 1, 2010
WADAU POLENI SANA KWA KUWA KIMYA KWA MDA MREFU
Kwakweli maisha haya we acha tu. Maana ndani ya huu mwezi ulioisha kwangu ilikuwa balaa. nalala siku chache na kesha mda mwingi . Nilikuwa bize kupita maelezo party nazo zilikuwa nyingi. Nilikuwa na majukumu mengi sana kias nikawa hadi nashindwa ku update blogs zangu. . Lakini sasa nimejipanga na natumai wadau mtafurahi . Ntajitahid niweke vitu vipya na newz kama kawa.
I la usisahau tarehe 7 ni vunja jungu party ndani ya kendwa rock . Dj nitakuwa mimi {Dj side} mwanzo mwisho. Pia kutakuwa na ngoma za kiasili. BIKIDUDE NA UNYAGO BAND watafanya mambo kuanzia saa moja hadi 6. na baada ya hapo ni kujirusha tuu mpaka bac. karibuni sana
Subscribe to:
Posts (Atom)