Wednesday, August 11, 2010
BIKIDUDE AFUNIKA MBAYA KWENYE VUNJAJUNGU PARTY NA FLAVA DJS
Hapa Bi Kidude anashuka ndani ya gari kutoka Town akiwa na wadau wa Zenj fm Radio na Fleva Djs,kutoka kushoto kwa Bikidude ni mtu mzima Dj Side, kulia ni mwanadada Emy c na nyuma kabisa ni Dj Sam
Pozi la nguvu la Bi kIdude akionesha kuwa na yeye wamo katika mambo ya pozi za picha aliyemuegemea ni Emy C na nyuma hapo ni Aziza Wazir aka Azwii
Nani anasema Bikidude hana nguvu? hapo alikuwa akishuka ngazi kuelekea katika ufukwe wa Kendwa Rocks Hotel ambapo alifanya makamuzi ya ukweli.Pichani hapo kama unavyoona Dj Side alikuwa akiburuzwa
Wameshamaliza ngazi hapo, Bikidude hapo ni mwendo wa kijeshi hataki mchezo katika kazi
Mwendo mdundo kudadadeki
Hawa ni wachina ambao walimpokea vizuri Bi Kidude na kwa mujibu wa maelezo ya Bi Kidude alisema kuwa hao ni wazee wake, sijui alikuwa akimaanisha nini maana hapo kwa mtazamo tuu anaonekana yeye ana umri mkubwa zaidi ya hao aliodai ni wazee wake!!!
Kundi zima la Unyango Band likisubiri kufanya makamuzi katika msosi kabla ya kufanya mambo ya ukweli ukweli katika stage.
Bi Kidude akiwa na wamiliki wa Hoteli ya Kendwa Rocks Mama Nuhu na Omar Kilupi
Jamani Emy c nae wamo katika mambo ya kubugi msondoo?? hapo akiwa na Bi Kidude wakioneshana kazi.
Wamiliki wa Kendwa Rocks na Kundi zima la Unyago Band wakibadilishana mawazo hapo kama unavyoona.
Nani kasema Bi Kidude hana nguvu? huwezi amini huyu Bibi ana nguvu sana kiasi ambacho wengi tulishangaa sana, ona jinsi alivyojifunga ngoma yake hiyo na huku anaitwanga kisawa sawa? kwa kweli huyu ni LEGENDARY OF MUSIC IN ZANZIBAR.
Vijana wa Unyago Band wakionesha vitu vyao hadharani.Mambo yalikuwa kiunyago unyago tuu yaani ni full kufundwa zaidi!!
Hatimaye Bi Kidude alijipatia Handsome wake na kuanza kumfunda kiunyago zaidi.
Non stop music jamani Bi Kidude akiwa kazini hataki masihara kabisa ona jinsi alivyo seriuos na kazi yake amejifunga msondo wake akiendelea na makamuzii!!
Jamani shughuli ni kuchakarika eeehh?? Unyago Band wakichakarika katika kutoa ile kitu roho inapenda kwa mashabiki waliohudhuria katika show hiyo!!Haya na radhi ama kwa hakika zilimwagwa si unaona jamaniii???!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kaka hii kali na miss sana vituko na wana vituko vya bikidude. kwakweli unapoweka vitu kama hivyo na sisi tunaonekana up to date. Tuwasiliana ila nimechukua pic hizi kuweka kwa blog yangu kama kuna ubaya na omba msamaha. Wenu Kaka blaza tzswahilivillage.blogspot.com
Post a Comment