Monday, August 23, 2010

BALOZI WA WAREKANI TZ NDANI YA MJENGO WA ZENJIFM LEO


Balozi wa marekani Alfonso E. Lenherdt’s leo alipata nafasi ya kufika ndani ya mjengo wa Zenjifm na kufanya kipindi maalum . Lengo hasa la kuja Zenjifm ni Kufuatia kauli ya Rais Obama ya Kuipongeza Tanzania , Nae balozi wa marekani Bwana Alfonso ameamua kusisitiza kile alichosema Rais Obama na alipata nafasi ya kufanya mahojiano maalum na Zenj fm Radio ambapo kwanza amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa ujasiri wao wa kupiga kura ya ndio na kusema kuwa siasa za uhasama na chuki zimkufa na kwa sasa wananchi wanachotakiwa kufanya ni kushikamana katika kujenga Zanzibar mpya yenye matumaini kwa vizazi vijavyo.
Katika mazungumzo yake Balozi Alfonso amesema kuwa kura ya maoni itarsaidia sana kudumuisha uhusiano wa muda mrefu uliopo baina ya Marekani na Zanzibar

No comments: