Wednesday, February 3, 2010
JEE? NI KWELI VICHECHE WASIOPENDA MAENDELEO YA HAS J NDIO WALIO MVUNJA MGUU?
Katika kile kinachoonekana kuwa ni bif, mtangazaji wa zamani wa Coconut fm Has J amechonga live na blog ya kijanja ya the crush.
Katika maelezo mchizi ameeleza kuwa siku ya tukio alikuwa akitoka katika ukumbi wa gymkhana akiwa na Berry Black na washakaji wengine.
Katika mazungumzo yake na blog hii ameeleza kuwa wakati akishuka katika usafiri mitaa ya michenzni ambapo hapo ni karibu na kwao kijana mmoja alimtaja kwa jina la Dill alimvamia kwa kumpiga teke la mguu wake wa kulia
Baada ya kitendo hicho Has J anasema kuwa aliamua kumdhibiti yule kijana lakini kutokana na kijana yule kuwa na washakaji zake, alitokea mtu mwengtine ambae alimkaba na wakashirikina kumpiga.
Baada ya Tafrani hizo Has J anasema kuwa alielekea nyumbani kwao kujipumzisha ambapo wakati huo hakuhisi maumivu ya aina yoyote lakini baada ya kulala na kuamka
ndipo alipoanza kuhisi maumivu makali katika goti lake.
Aidha Has J anasema kuwa baada ya kujiona yupo katika hali hiyo ndipo familia yake ilipoamua kumpeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa Matibabu
Mpango mzima wa hii kesi kwa sasa imesharipotiwa katika vyombo vya sheria na uchunguzi zaidi unendelea.
Has J ambae anonekana akiwa na Pio pio mguuni kwake . amesema yote hayo sababu ni beef na choyo kilichowajaaa washkaj zake .. Kwasasa anaendelea vizuri akiwa anapata matibabu.
Has J akiwa na mimi ndani ya studio za Zenjfm wakati anatuhadithia mpango mzima juu ua skedo ambayo imemkuta .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment