Thursday, April 29, 2010

Wednesday, April 28, 2010

FULL MOON PARTY ONCE AGAIN


DJ SIDE ON 1 & 2
We are at Moon this Saturday!!labor day!! Full moon party ever!! . The speakers will be smoking. Starting at 2pm DJ Side from Zenjifm fm will be entertaining you at the decks. Get ready for 10 hours of house, deep house, funky house, breaks, hip-hop, lounge, you name it, we will have all the time in the world to spin it!
Moon is setting us up by the pool next to a specially set cocktail bar. Drink specials will be available so get your swim suit, sun lotino and appetite for beats and meet us at Kendwa Rock Hotel Instist 1/5/2010 . Come & show love with Us!!

FLEVA DJS MORE THAN DJS

FULL MOON PARTY IMEWADAI .NI IJUMA MOSI HII

FLEVA DJS MORE THAN DJS

FLEVA DJS MORE THAN DJS
Full moon party Imewadia tena .. Ni Ijumamosi hiii siku ya wafanyakazi Duniani Spika zitaanza kufuka moshi kianzia 2pm Dj side kutoka zenjifm atawapa burudani mwanzo mwisho.. Kaa tayari kwa burudani ya masaa 10 bila ya kuchoka… Burudani zote house hip hop , dancehall bongo flava bila kusahau reggae ….Mpaka kunakucha … vinyaji vya aina zote vitapatikana cheza mpaka basi burudika mpaka mwisho… Tukutane basi Siku ya Jumamosi ya tarehe 1 /May/2010. ndani ya Kendwa rock hotel ,,,,,,, Karibu uapate Burudani za ukweli Usisahau Flava Djs Ndani ya nyumba. Mimi Dj side nitakuwa kwenye 1 na 2 mwanzo mwisho . Karibuni sana
FLEVA DJS MORE THAN DJS

UZINDUZI WA ALBUM YA OFSIDE TRICK NDANI YA KENDWA ROCK

FLEVA DJS MORE THAN DJS

Muda cris akiitendea haki mic wakati wakikamua wimbo wa bata ndani ya hotel ya Kendwa rock juzi . Show hii iliandaliwa na kikosi cha maangamizi Flava Djs .Katika show hii kulikuwa na wasani kama 9 hivi. alikuwepo Lil Geto. Rico singo, Dorica, Lil zinyo, Bad sky. Jackob B,Tani B na kadamila . Mc wa show hii alikuwa Mb squash.. aka The matrixx . Kwa upande wa 1 na 2 nilikuwa mimi (Dj side)
Show ilikuwa mzuka sana. Kulikuwa na watu kibao.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa wakina dada wakibanjuka baada ya kumaliza show, Unaemuona hapo kulia yako ni mwana dada Dorica akiwa na shoga yake wakiruka kwanja. Hii ilikuwa baada ya kumaliza show ya uzinduzi , Kulikuwa na Disco la nguvu. Si unajua mtu mzima nipo kwenye mashine? Usipime!!!
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mb Bobby!!! Yeye ndie aliekuwa Mc wa shughuli nzima. Alinifurahisha sana kwani jamaa kwenye mic ni noma. Alikuwa anongea lugha 3. Kiswahili, English, na Kitaliano. Jamaa aliimudu hasa Mic. kwani kila aliefika pale kendwa kwenye show alijiskia burudani. Unajua kwa nini? Yap coz Mc wenyewe ni burudani raha raha tu .
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mwana dada Emy C wa Zenjifm hapa akiwa kwenye pozi ya ukweli na star wa miondoko ya Hip hop Rico singo. Hapa ilikuwa baada ya Mtu mzima Rico kumaliza tu kukamua . Kushuka tu chini wakaanza Kukamua Mapicha wow!!! Hapa nimependa style.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mtu Mzima Shot Gun aka metaya aka Dege la jeshi akiwa kwenye Pozi na mwana dada wa Zenjifm Aziza wariz Baada tu ya kumaliza show ya kula bata. Hapa walikuwa wanajipongeza.Hii ni ndani ya Kendwa rock . Kulikuwa na mastar kibao ambao walikuja kuwapa wazzeee wa albaataa
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa ni mastar watupu . Mkali rico singo kushoto . katikati ni Mtangazaji wa Zenjifm Emy C kuliani mwake ni Shot Gun .
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa Emy C akiwapongeza boyz baada ya kushuka kwenye stage .. Jamaa malikamua na Ngoma yao mpyaa ambayo bado haijatoka Inaitwa Nipe CHORUS . Huyu hapa kwenye poz ni Jackob B akiwa na Emy C
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Washakaji wakibanjuka... Albaaata ndio nyimbo iliyowabamba sana siku hiyo. Ama kweliiiii Zanzibar kwa miduara?
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa ni timu nzima ya Jupiter Record. Kulia ni Producer Aron name . akima wa Metaya. katikati ni Aziza wariz na kulia ni Rico singo baada ya kula bata.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa hakija badilika kitu ila hapa katikati ni Emy c . Mtu mzima aron name kulia , metaya, emy c katkati na rico singo . Kiufupi hiii ilikuwa show ya kuenjoy zaid . Baada ya kumaliza wasanii kuparform hapo tena ilikuwa kazi yangu ya kuwarusha. Hapo ni kwanja hadi Kumekucha.
FLEVA DJS MORE THAN DJS
Hii ndio mambo yalivyokuwa ndani ya Hotel ya kendwa rock Juzi Ijuma mosi . kwenye uzinduzi wa Album ya Ofside Trick . Ambapo tulianza Ijumaa ndani ya Kiwengwa Obama Pub. na siku ya pili tukahitimsiha Ndani ya Hotel ya Kendwa rock
Nawashukuru wote waliohudhuria. Pia nawashukuru wote walisababisha kufanikisha show zote mbii. One love
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Tuesday, April 27, 2010

Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010. Mshindi kupata kitita cha Dola 5,000/=

FLEVA DJS MORE THAN DJS

Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010.
Mshindi kupata kitita cha Dola 5,000/=

Shirika la GTZ likishirikiana na Tamasha la nchi za Jahazi (ZIFF) kwa mara ya tatu tena mwaka huu 2010 watatoa tuzo ya Filamu ya Ousmane Sembene, tuzo hii italenga hasa katika filamu fupi ambazo hazijazidi dakika 20 na ambazo zitakua zimezungumzia au kugusia masuala yanayoikabili jamii ya kitanzania hasa katika mambo ya Ukimwi, Jinsia, Elimu na umasikini.

Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 taslimu papo hapo kwaajili ya kumsaidia katika kutengeneza filamu nyingine ama kuboresha kazi zake.

Wale wote watakaotaka kushiriki katika tuzo hii wawasilishe filamu zao kabla ya tarehe 30/04/2010 kwa kujaza fomu za kawaida zinazopatikana katika tovuti yetu www.ziff.or.tz

Daniel Nyalusi
Events and Film Program Coordinator
Zanzibar International Film Festival

UZINDUZI WA ALBUM YA OFSIDE TRICK ZANZIBAR

FLEVA DJS MORE THAN DJS

Muda criss akikamua Ipasavyo ndani ya Pub ya Obama kiwengwa kwenye uzinduzi. show hii Niliandaa mimi. Flava Djs ndani ya nyumba
FLEVA DJS MORE THAN DJS
href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEji9PTvLyzSCX7B50rTe-2RIH-qRD_5qoEvoJ_N6VqxGfmxK9PcQi26kAPfSc_yhonHWNeRfRuO1oQM7_LFJ9I604nnVF0zmOd5TD_3MOq94AiaQWack2ys-kY1Kmarys0c7dxggrhd7LM/s1600/Tani+2.JPG">
TANI BANTANI AKA NDEVU TATU AKIWARUSHA NA DANCE HALL YAKE YA MIKONO HIZO JUU
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mtangazaji wa Zenjifm Grac kiondo au wengi wanamwita Sister Dread hapa akishow love na Rafiki wake mpyaa Bw Silers ambae ni Mannager wa Hotel ya Ocean Paradise .Hii ilikuwa katika uzinduzi wa Album ya Ofside Trick Kiwengwaa
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mwana dada Dorica hapa wakiwa na Muda cris Juu ya Opama Pub wakisubiria muda wa zam yao kufika ili wakamue
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Tani aka Ndevu tatu akiwa na Lil zinyo wakiwa wanasubiria makamuzi kuanza. Show hii imeandaliwa na (Fava Djs) wa Zenjifm. Ilikuwa ni Uzinduzi wa Album ya Ofside Trick Bata . Show hii ilikuwa siku ya Ijumaa juzi siku ya pili mambo yakendelea Tena Nugwi. KENDWA ROCK HOTEL

HUYU NDIE ALIE KUWA AL-BATA TOBATIATA WA SIKU HIYO

FLEVA DJS MORE THAN DJS

FLEVA DJS MORE THAN DJS

FLEVA DJS MORE THAN DJS

FLEVA DJS MORE THAN DJS
Hii ilikuwa siku ya Ijumaa ndani ya ukumbi wa Obama Pub kiwengwa katika uzinduzi wa Album ya Ofside Trick .. Mwana dada huyu alimwaga radhi mpaka bac maana alipanda kwenye stage akiisakata hasaaa ngoma ya bata. Ilibidi ngoma ya bata Niirudie kama mara 4 kila ikiisha watu wanapiga kelele Dj side rudia rudia . Kwenye stage . Mc alikuwa Mb skwash ambae aliwafanya muda cris na Lil Getto uzalendo uwashinde ili bidi tu tufanye hivo. Wana dada walimwaga radhi mpaka bc maana picha nyengine aaa hazifai ..maana imenibidi nisiziweke Blog yangu itakuwa mashakani .
FLEVA DJS MORE THAN DJS

MAMBO YA BATA NDANI YA KIWENGWA

FLEVA DJS MORE THAN DJS

FLEVA DJS MORE THAN DJS
MUDA CRIS NA LIL GETTO WAKIKAMUA IPASAVYO KWENYE STAGE MITAA YA KIWENGWA KWENYE UZINDUZI WA ALBUM YAKO
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Afande Sele’ juzi Aprili 25 alianguka chini na kupoteza fahamu jukwaani wakati akipafomu kwenye tamasha la siku ya Malaria duniani, event ambayo ilifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Habari za kuaminika zinaeleza kuwa Mfalme Sele alikuwa akisumbuliwa na Malaria kali, na alikuwa amelazwa Hospitali, ila kwa kuwa alikuwa ameshalamba ‘mkwanja’ akalazimika kuhudhuria huku akiwa mgonjwa.
Ilikuwa ni kama muvi kali kwani sherehe zilikuwa ni za maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, na Prezidaa alikuwa akiwahimiza Watanzania kujikinga na ugonjwa huo hatari, huku wasanii, akiwemo Afande Sele wakisaidia kuufikisha ujumbe kwa walengwa, kumbe tayari adui malaria alikuwa ndani ya mwili wa Afande. Mkali huyo wa Rhymes ambaye awali alikuwa amelazwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu, alipanda jukwani kwa kujikongoja, na sababu kubwa inaelezwa kuwa tayari alikuwa amevuta mkwanja.

Baada ya kudondoka, Mfalme Sele kwa msaada wa mabaunsa na wasanii wenzake akiwemo Joseph Haule ‘Profesa Jay,’ alikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa kwa mara ya pili na kuendelea kupata tiba ya uhakika ya malaria.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

MKONO MOJA WEKA JUU VIDEO. CHEGE & TEMBA

FLEVA DJS MORE THAN DJS

Friday, April 23, 2010

MPANGO MZIMA WA MSANII (I.T) AU MKALI WA HUZUNI TOKA ZANZIBAR UKO HIVII!

FLEVA DJS MORE THAN DJS
Juzi katika tembea tembea yangu Nilienda Pale Mtoni Marine Hotel kupata mambo mambo flani . Wakati nafika pale nikakutana na Kijana huyu I.T) au mkali wa huzuni . Nilishangaa kumkuta Reception . Nilidhani ameacha mziki , Nilidhani amekuwa hotely , Mziki bac. Kumbe ilikuwa tofauti Katika maonegzi yetu aliniambia hivi

Nimejiandaa vilivyo kaka katika mikakati ya kuachia ngoma yangu mpya
ambayo inaitwa(POKEA) imefanywa na producer mahiri kutoka
zanzibar anayeitwa MACONELLAH. Nimekuwa kimya kwa miezi 6
tangu niachie ngoma ya TAMBUA kwasababu producer wangu mara
nyingi akinitengenezea ngoma mimi huwa anapenda kuitulizia zaidi
kabla ya kutoka kwenda redio.
nyimbo yangu hiyo imeelezea jinsi gani ninavyopata tabu mara baada ya
mpenzi wangu kuondoka katika mazingira ya kutatanisha na sijui wapi
alipo kwenda. na ndio maana nikamtumia salamu zangu apokee.
mara baada ya kupata mateso mengi wakati hayupo kaka.

Najisikia furaha kuwa kama ni msanii katika lebo ya maconellah
pia wapenzi wangu wawe tayari kwa mambo mazuri mengi tu.
badala ya ngoma yangu hiyo ya ( pokea) ambayo itaanza kusikika soon
kutoka sasa. mana kuna mawe mengine ambayo yanakuja nimeshiirikiana na
wasanii tofauti. na pia nnampango wa kufanya ngoma na dorica wiki hii katika
studio hiyohiyo ya maconellah rec. na nyimbo hiyo inaitwa (SAUTI YA MAHABA)
imesimama katika miondoko ya zuku raggah.

never the less my vdo is finished so they are going to see it soon. that all.
Hapa hoteli napiha mzigo just kutafuta ruzuku kaka . si unajua mziki wetu bila ya kazi pembeni mambo hayendi ..

niite the son of maconellah (I.T) mkali wa huzini toka zanzibar.

Jamnai ni hayo tu kutoka kwa jamaa.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

TUWASILAINE


Habari yako mdau wa blog hii.. Natumai Unatembela ili upate unachokitaka . Tuwasiliane bc . Kama ni msanii basi nitumie Picha yako au nyimbo yako Ili Niweke kwenye blog. Na kama una ushauri wowote kuhusu blog hii bc niandikie tu TUWASILIANE Email yangu ni djside_dj@yahoo.com

Thursday, April 22, 2010

ITAKUKUTA NA WEWE


Habari yako ndungu unaetembelea Blog hii. kwa takribani wiki moja hivi tumeshindwa ku upload story au habari . Hii ilikuwa kutokana na mabadiliko ya Technology.. Hii imetukuta sisi Zanzibar . Kwa wale wote waliokuwa wakitumia window xp service pack 2 basi walikuwa hawawezi kusoma email ya yahoo . hotmail wengine hata kufungua face book au ku upload chochote kwenye mtandao. Ndio maana tulikuwa tunasumbuka sana Hadi tumelitaftia ufumbuzi suala hili. Kumbe ni Windo xp service pack 2 imepitwa na wakati na nilazima uwe na Windo xp service pack 3 au Window vister au window 7 .. Endapo na wewe imekutokea basi usishangae just upgrade yr window .

Naamini hii ni kutoka kwa Microsoft wenyewe. So na wewe itakukuta tu.

Kuanzia kesho kama kawaida habari zitakuwa update . Thx
Posted by Zenjifm Radio Zanzibar at 9:33 AM

TATIZO LA INTERNET ZNZ LAZOROTESHA UPATIKANAJI WA HABARI KWENYE BLOG

WADAU WIKI HII ZNZ TUMEKUA NA MATATIZO YA INTERNET

Wednesday, April 14, 2010

DOWNLOAD BERRY BLACK NEW SONG


Direct Link to Downlaod. RADIO PROMO http://usershare.net/w8l7un3ntknf - NJOO - BERRY BALCK FT SHIRKO

DOWNLOAD JUMA 20 NEW SONG


DOWNLOAD JUMA 20 NEW SONG JUNE JULY RADIO PROMO

Direct Link to Downlaod http://usershare.net/5zmsi4yvrq38

SHAA AACHIA PINI MPYAA - SHOGA


Mwana dada machachari katika Gemu Shaa ameachia wimbo wake Mpyaa Unaokwenda kwa jina la SHOGA . Shoga ni goma ya nne ya Shaa kutoka katiba album yake iitwayo ZAMU YANGU. SHOGA ni wimbo ulionadikwa na kutungwa na Shaa mwenyewe .Producer Marco Chali ndia alieisimamia vizuri ngoma hii . Style ya beat ya wimbo huu ni mchanganyiko wa Twist na Kwaito na hiyo ilitokana na Shaa kuwa mpenzi wa style zote mbili na vilevile kutaka kutoka kitofauti. Video ya wimbo huu itakuwa on air ndani ya siku chache zijazo … Bonyeza Hapa ku download Ngoma mpya ya Shaa

Tuesday, April 13, 2010

RAY C MATATANI KWA ATAPELI NORWAY


Mwimbaji wa nyota wa kike nchini, Rehema Chalamila ”Ray C” amejikuta akiingia katika kashfa kubwa ya kutapeli Dola za Kimarekani 4000,- ambazo ni zaidi ya shilingi milioni nne za Kitanzania.

Kwa mujibu wa Mtanzania anayeishi Norway aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Ng´anzo, pesa alizotapeli Ray C zilikuwa ni malipo kwa ajili ya kufanya shoo katika nchi za Uholanzi, Sweden, Norway na Ujerumani.

Hassan ambaye anajishughulisha na kazi za ”upromota” nchini Norway, ameliambia Sani kwamba alimuunganishia Ray C kwa promota wa Kiganda anayefanya kazi zake katika nchi za Skandinavia, Eddy Bukenya.

”Eddy aliniomba nimuunganishie kwa Ray C kwa kuwa alikuwa anafahamu ni mtu wa nyumbani, nilimsifia kwake kuwa ni mtu mzuri ambapo walikubaliana.” alisema Hassan.

Aliongeza kwamba, pamoja na malipo ya Dola 4000,- kwa maonyesho hayo, lakini Ray C aliweka sharti kwamba ni lazima aende na mpenzi wake, Lord Eyes wa kundi la Nako 2 Nako ambapo promota huyo alikubali.

Habari zaidi zimesema kwamba, walimtumia Ray C pamoja na Lord Eyes viza na kuwataka wakachukue katika ubalozi wa Uholanzi mjini Dar es Salaam.

”Tulimpigia simu Ray C kwamba anatakiwa akachukua viza lakini akawa anajichelewesha, tulimsisitiza sana awahi lakini siku zikawa zinakwenda bila kutekeleza na hiyo ikatuonyesha kwamba alipanga kufanya utapeli” Hassan amesema.

Amezidi kuongeza kwamba, baadaye wakafuatilia katika ubalozi wa Uholanzi ambapo uliwajibu kwamba si Ray C wala Lord Eyes aliyekwenda ubalozini hapo, wakajua wameshapigwa ”changa la macho”

Amesema kwamba, katika onyesho ambalo alitakiwa kufanya katika mjini wa Oslo nchini Norway, watu walijitokeza kwa wingi wakitegemea kumuona Ray C lakini wakaambulia patupu.

”Kwa kweli ametuletea matatizo makubwa kwani watu walianza kudai viingilio vyao, hakika ilikuwa vurugu mechi kubwa sana” alisema Ng´anzo na kuongeza kwamba hata katika shoo nyingine ambazo ilibidi azifanye wamepata hasara kubwa.

”Ray C kaniharibia mimi na pia kuwaharibia wasanii wenzake, amewapotezea soko kabisa wasanii wa nyumbani na wanaonekana matapeli.” amesema.

Ng´anzo amesema kwamba hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kusumbua kwani aliwahi kuandaa onyesho ambapo Ray C aliahirisha kwenda mara mbili.

Ray C alipoulizwa kuhusiana na ”utoto wa mjini” alioufanya aliporomosha matusi kwa mwandishi wetu.

”Wewe fala tu, wewe mjinga unaongea ujinga!” alisema mwanadada huyo aliyevaa nguo za aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika Onyesho la ”Malaria No More.”
Habari hii ni kwa mujibu wa Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo http://watanzaniaoslo.blogspot.com/

WITO KWA WASANII WANOATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2011


Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote.

Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 280 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jose Chameleone, Samba Mapangala, Saida Karoli, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate,Banana Zorro & the B Band, Joh Makini, Nako2Nako Soldiers, Nyota Ndogo,Thandiswa, Culture Musical Club na wengineo wengi.

MWISHO wa kupokea maombi
31 July 2010

Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri , malazi,chakula na matumizi madogo madogo.Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri

Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa
Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi kutoka kwako kabla ya MWISHO wa kutuma maombi. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:

* form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
* nakala moja au mbili ya kazi zako (CD au DVD)
* picha moja au mbili( JPG au karatasi)

Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo

Busara Promotions, PO Box 3635, Zanzibar, Tanzania au Email busara@zanlink.com
Tel: +255 24 223 2423 or +255 784 925 499 or +255 773 822 294

(Form inaweza kujazwa kupitia mtandao wa intenate) http://www.busaramusic.org/
au http://www.busaramusic.org/callforartists/2011e.php

Monday, April 12, 2010

HATIMAE NA DULLY NAE AJITOA KWEMYE TUZO


Hatimae nae Dully sykes ametangaza rasmni nae kujitoa katika tuzo za kili. Nimesema na nilishasema sitaki kuwekwa katika kategory yoyote, sioni faida ya tuzo, sijawahi kupata tuzo tangu nianze mziki, single 36 mpaka sasa kama salome hunifahamu hakuna hata moja nimepata tuzo.ni bora nitoe single tu na wala hata album sitaki.amesema dullu.Dully amekuwa msanii wa pili kujitoa baada ya t.i.d kujitoa wiki mbili zilizopita.kwa sasa dully yuko katika mazoezi ya band yake ijayo inayoitwa BROTHERMAN BAND Kwa sasa tayari ameshadondosha ngama yake mpyaa inayokwenda kwa jina la Papa..

J NATURE AUNDA KIKOSI KIPYA


Kundi la TMK HALISI limesaini mkataba na kampuni inayoitwa DLC ambayo inafanya biashara zake China na Tanzania, kampuni hii ambayo yenyewe ndiyo itasimamia kila kitu ikiwemo mambo ya promosheni kutafuta maonyesho ya nje na ndani ya nchi pia kusimamia mauzo ya kila kitu.

Juma alipata wakati mgumu wa kuchuja na kuchagua vichwa vinne atakavyo fanya navyo kazi ya kuunda TMK Halisi mpya na yeye awe watano,Badala ya ile ya awali iliyokuwa na watu 12. Walio chaguliwa kusaini mkataba huo ni DOLO, BABA LEVO,JB WA MABAGA FRESH,KG SON pamoja na Juma Nature mwenyewe.

kwa sasa kundi hilo linalodhamiria kuja upya katika anga ya muziki wa kizazi kipya,limeshafanya kazi inayoitwa MNATAKAJE? ambayo imeanza kusambazwa redioni tangu mwishoni mwa wiki. Kumbuka kwamba Hivi karibuni wameanzisha studio maeneo ya home kwa nature aka mbagala, na studio hiyo inaitwa HALISI REC. Sio kwamba ni studio kuuuubwaaaa hapana ni cha kiaina tu na ndio ambayo imedondosha ngoma ya jebi, HATUFANANI, mkono wa producer jazz.na wiki hii watatambulisha ngoma yao mpya dizaini ya kwaito. Pia ngoma mpya ya mabaga fresh inaitwa 770 ambazo zote zimegomgwa kwenye Halisi record

QUICK RACKA - BULLET VIDEO

Saturday, April 3, 2010

MAMBO Y A EASTER PARTY NA FLAVA DJS


Nachukua nafasi hii kuwashukuru wale wote tulokuwa nao pamoja jana kendwa rock kwenye Easter party... Nawashukuru Ndugu zangu kutoka Dar es salam...Jana tulikuwa nae Sebastian ndege wa Clouds fm Pia nduguza ngu wa Arusha nao pia waliwakilisha . Wageni ndio walikuwa wengi sana . Kutoka Canada Norway. Italy .German , Denmak . Bila kuwasahau ndugu zangu kutoka Indiaa. wahindi walikuwa wengi sana . Unajua Zanzibar kwa sasa kuna Festival ya Agakhan so wahindi walikuwa wengi.
Kiufupi party ilikuwa mzuka sana , Na kila mtu alikua na furaha watu wamee enjoy sana tena sana. Nilihakikisha napiga ngoma all around the world.. kwa rika zote.. I thank all v you for comin!!!
Kwa Upande wa ma Djs nilikuwa mimi j side na Dj Dully.. Bt mimi nilichukuwa mda mwingi sana kuwarusha watu . Pia Alijitokeza Dj wa kike kutoka Norway nae alikuja kukamua nyimbo kama tatu hivi.. I say? Party ilikuwa mzuka

Wadau party nyengine itakuwa tarehe 8 mwezi huu huko huko nungwi.. Sehem zamani palikuwa pakiitwa kwa CHOLO bt sasa panaitwa Golden Fish .. kwa Upande wa Ma Djs Nitakuwepo mimi mwanzo mwisho. (Dj side from Zenjifm) karibuni sana .

SASA NIPO KENDWAA TAYARI NISHAFUNGA MZIKI PARTY INATAKA KUAANZA

WADAU VIPI? PARTY NDO LEO.. MIDA HIZI MIMI NDO NIMEMALIZA KESET SOUND SASA NAPUMUUA . MIDA MIDA NIPOROMOSHE MAWE.... YAANI MPKA KUNAKUCHA . INAONEKANA LEO KUTAPENDEZA SANA COZ WAGENI NI WENGI SANA. HOTEL ZOTE ZIPO FULL .. KARIBUNI SANA WADAU...

Thursday, April 1, 2010



EASTER PARTY EVER!! THE SPEAKER WIL BE SMOKING. STARTING AT 2pm...DJ SIDE FROM ZENJIFM WIL BE ENTERTAINING U AT THE DECK. LADYS AND GENT'S ARE U READY FOR ACROBAT SHOW AND FIRE EATER? SPACIAL BUFFE BEACH EDGE.. DRINKS AND ICE CREAM WIL BE AVAILABLE. GET READY FOR EASTER PARTY EVER!! MEET US AT KENDWA ROCK THIS S ATURDAY FLAVA DJS INA HOUSE!!