Tuesday, April 13, 2010

RAY C MATATANI KWA ATAPELI NORWAY


Mwimbaji wa nyota wa kike nchini, Rehema Chalamila ”Ray C” amejikuta akiingia katika kashfa kubwa ya kutapeli Dola za Kimarekani 4000,- ambazo ni zaidi ya shilingi milioni nne za Kitanzania.

Kwa mujibu wa Mtanzania anayeishi Norway aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Ng´anzo, pesa alizotapeli Ray C zilikuwa ni malipo kwa ajili ya kufanya shoo katika nchi za Uholanzi, Sweden, Norway na Ujerumani.

Hassan ambaye anajishughulisha na kazi za ”upromota” nchini Norway, ameliambia Sani kwamba alimuunganishia Ray C kwa promota wa Kiganda anayefanya kazi zake katika nchi za Skandinavia, Eddy Bukenya.

”Eddy aliniomba nimuunganishie kwa Ray C kwa kuwa alikuwa anafahamu ni mtu wa nyumbani, nilimsifia kwake kuwa ni mtu mzuri ambapo walikubaliana.” alisema Hassan.

Aliongeza kwamba, pamoja na malipo ya Dola 4000,- kwa maonyesho hayo, lakini Ray C aliweka sharti kwamba ni lazima aende na mpenzi wake, Lord Eyes wa kundi la Nako 2 Nako ambapo promota huyo alikubali.

Habari zaidi zimesema kwamba, walimtumia Ray C pamoja na Lord Eyes viza na kuwataka wakachukue katika ubalozi wa Uholanzi mjini Dar es Salaam.

”Tulimpigia simu Ray C kwamba anatakiwa akachukua viza lakini akawa anajichelewesha, tulimsisitiza sana awahi lakini siku zikawa zinakwenda bila kutekeleza na hiyo ikatuonyesha kwamba alipanga kufanya utapeli” Hassan amesema.

Amezidi kuongeza kwamba, baadaye wakafuatilia katika ubalozi wa Uholanzi ambapo uliwajibu kwamba si Ray C wala Lord Eyes aliyekwenda ubalozini hapo, wakajua wameshapigwa ”changa la macho”

Amesema kwamba, katika onyesho ambalo alitakiwa kufanya katika mjini wa Oslo nchini Norway, watu walijitokeza kwa wingi wakitegemea kumuona Ray C lakini wakaambulia patupu.

”Kwa kweli ametuletea matatizo makubwa kwani watu walianza kudai viingilio vyao, hakika ilikuwa vurugu mechi kubwa sana” alisema Ng´anzo na kuongeza kwamba hata katika shoo nyingine ambazo ilibidi azifanye wamepata hasara kubwa.

”Ray C kaniharibia mimi na pia kuwaharibia wasanii wenzake, amewapotezea soko kabisa wasanii wa nyumbani na wanaonekana matapeli.” amesema.

Ng´anzo amesema kwamba hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kusumbua kwani aliwahi kuandaa onyesho ambapo Ray C aliahirisha kwenda mara mbili.

Ray C alipoulizwa kuhusiana na ”utoto wa mjini” alioufanya aliporomosha matusi kwa mwandishi wetu.

”Wewe fala tu, wewe mjinga unaongea ujinga!” alisema mwanadada huyo aliyevaa nguo za aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika Onyesho la ”Malaria No More.”
Habari hii ni kwa mujibu wa Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo http://watanzaniaoslo.blogspot.com/

No comments: