Monday, April 12, 2010
J NATURE AUNDA KIKOSI KIPYA
Kundi la TMK HALISI limesaini mkataba na kampuni inayoitwa DLC ambayo inafanya biashara zake China na Tanzania, kampuni hii ambayo yenyewe ndiyo itasimamia kila kitu ikiwemo mambo ya promosheni kutafuta maonyesho ya nje na ndani ya nchi pia kusimamia mauzo ya kila kitu.
Juma alipata wakati mgumu wa kuchuja na kuchagua vichwa vinne atakavyo fanya navyo kazi ya kuunda TMK Halisi mpya na yeye awe watano,Badala ya ile ya awali iliyokuwa na watu 12. Walio chaguliwa kusaini mkataba huo ni DOLO, BABA LEVO,JB WA MABAGA FRESH,KG SON pamoja na Juma Nature mwenyewe.
kwa sasa kundi hilo linalodhamiria kuja upya katika anga ya muziki wa kizazi kipya,limeshafanya kazi inayoitwa MNATAKAJE? ambayo imeanza kusambazwa redioni tangu mwishoni mwa wiki. Kumbuka kwamba Hivi karibuni wameanzisha studio maeneo ya home kwa nature aka mbagala, na studio hiyo inaitwa HALISI REC. Sio kwamba ni studio kuuuubwaaaa hapana ni cha kiaina tu na ndio ambayo imedondosha ngoma ya jebi, HATUFANANI, mkono wa producer jazz.na wiki hii watatambulisha ngoma yao mpya dizaini ya kwaito. Pia ngoma mpya ya mabaga fresh inaitwa 770 ambazo zote zimegomgwa kwenye Halisi record
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment