Tuesday, April 27, 2010
Afande Sele’ juzi Aprili 25 alianguka chini na kupoteza fahamu jukwaani wakati akipafomu kwenye tamasha la siku ya Malaria duniani, event ambayo ilifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Habari za kuaminika zinaeleza kuwa Mfalme Sele alikuwa akisumbuliwa na Malaria kali, na alikuwa amelazwa Hospitali, ila kwa kuwa alikuwa ameshalamba ‘mkwanja’ akalazimika kuhudhuria huku akiwa mgonjwa.
Ilikuwa ni kama muvi kali kwani sherehe zilikuwa ni za maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, na Prezidaa alikuwa akiwahimiza Watanzania kujikinga na ugonjwa huo hatari, huku wasanii, akiwemo Afande Sele wakisaidia kuufikisha ujumbe kwa walengwa, kumbe tayari adui malaria alikuwa ndani ya mwili wa Afande. Mkali huyo wa Rhymes ambaye awali alikuwa amelazwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu, alipanda jukwani kwa kujikongoja, na sababu kubwa inaelezwa kuwa tayari alikuwa amevuta mkwanja.
Baada ya kudondoka, Mfalme Sele kwa msaada wa mabaunsa na wasanii wenzake akiwemo Joseph Haule ‘Profesa Jay,’ alikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa kwa mara ya pili na kuendelea kupata tiba ya uhakika ya malaria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment