Tuesday, April 27, 2010
Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010. Mshindi kupata kitita cha Dola 5,000/=
Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010.
Mshindi kupata kitita cha Dola 5,000/=
Shirika la GTZ likishirikiana na Tamasha la nchi za Jahazi (ZIFF) kwa mara ya tatu tena mwaka huu 2010 watatoa tuzo ya Filamu ya Ousmane Sembene, tuzo hii italenga hasa katika filamu fupi ambazo hazijazidi dakika 20 na ambazo zitakua zimezungumzia au kugusia masuala yanayoikabili jamii ya kitanzania hasa katika mambo ya Ukimwi, Jinsia, Elimu na umasikini.
Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 taslimu papo hapo kwaajili ya kumsaidia katika kutengeneza filamu nyingine ama kuboresha kazi zake.
Wale wote watakaotaka kushiriki katika tuzo hii wawasilishe filamu zao kabla ya tarehe 30/04/2010 kwa kujaza fomu za kawaida zinazopatikana katika tovuti yetu www.ziff.or.tz
Daniel Nyalusi
Events and Film Program Coordinator
Zanzibar International Film Festival
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment