Wednesday, April 28, 2010

UZINDUZI WA ALBUM YA OFSIDE TRICK NDANI YA KENDWA ROCK

FLEVA DJS MORE THAN DJS

Muda cris akiitendea haki mic wakati wakikamua wimbo wa bata ndani ya hotel ya Kendwa rock juzi . Show hii iliandaliwa na kikosi cha maangamizi Flava Djs .Katika show hii kulikuwa na wasani kama 9 hivi. alikuwepo Lil Geto. Rico singo, Dorica, Lil zinyo, Bad sky. Jackob B,Tani B na kadamila . Mc wa show hii alikuwa Mb squash.. aka The matrixx . Kwa upande wa 1 na 2 nilikuwa mimi (Dj side)
Show ilikuwa mzuka sana. Kulikuwa na watu kibao.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa wakina dada wakibanjuka baada ya kumaliza show, Unaemuona hapo kulia yako ni mwana dada Dorica akiwa na shoga yake wakiruka kwanja. Hii ilikuwa baada ya kumaliza show ya uzinduzi , Kulikuwa na Disco la nguvu. Si unajua mtu mzima nipo kwenye mashine? Usipime!!!
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mb Bobby!!! Yeye ndie aliekuwa Mc wa shughuli nzima. Alinifurahisha sana kwani jamaa kwenye mic ni noma. Alikuwa anongea lugha 3. Kiswahili, English, na Kitaliano. Jamaa aliimudu hasa Mic. kwani kila aliefika pale kendwa kwenye show alijiskia burudani. Unajua kwa nini? Yap coz Mc wenyewe ni burudani raha raha tu .
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mwana dada Emy C wa Zenjifm hapa akiwa kwenye pozi ya ukweli na star wa miondoko ya Hip hop Rico singo. Hapa ilikuwa baada ya Mtu mzima Rico kumaliza tu kukamua . Kushuka tu chini wakaanza Kukamua Mapicha wow!!! Hapa nimependa style.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Mtu Mzima Shot Gun aka metaya aka Dege la jeshi akiwa kwenye Pozi na mwana dada wa Zenjifm Aziza wariz Baada tu ya kumaliza show ya kula bata. Hapa walikuwa wanajipongeza.Hii ni ndani ya Kendwa rock . Kulikuwa na mastar kibao ambao walikuja kuwapa wazzeee wa albaataa
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa ni mastar watupu . Mkali rico singo kushoto . katikati ni Mtangazaji wa Zenjifm Emy C kuliani mwake ni Shot Gun .
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa Emy C akiwapongeza boyz baada ya kushuka kwenye stage .. Jamaa malikamua na Ngoma yao mpyaa ambayo bado haijatoka Inaitwa Nipe CHORUS . Huyu hapa kwenye poz ni Jackob B akiwa na Emy C
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Washakaji wakibanjuka... Albaaata ndio nyimbo iliyowabamba sana siku hiyo. Ama kweliiiii Zanzibar kwa miduara?
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa ni timu nzima ya Jupiter Record. Kulia ni Producer Aron name . akima wa Metaya. katikati ni Aziza wariz na kulia ni Rico singo baada ya kula bata.
FLEVA DJS MORE THAN DJS

Hapa hakija badilika kitu ila hapa katikati ni Emy c . Mtu mzima aron name kulia , metaya, emy c katkati na rico singo . Kiufupi hiii ilikuwa show ya kuenjoy zaid . Baada ya kumaliza wasanii kuparform hapo tena ilikuwa kazi yangu ya kuwarusha. Hapo ni kwanja hadi Kumekucha.
FLEVA DJS MORE THAN DJS
Hii ndio mambo yalivyokuwa ndani ya Hotel ya kendwa rock Juzi Ijuma mosi . kwenye uzinduzi wa Album ya Ofside Trick . Ambapo tulianza Ijumaa ndani ya Kiwengwa Obama Pub. na siku ya pili tukahitimsiha Ndani ya Hotel ya Kendwa rock
Nawashukuru wote waliohudhuria. Pia nawashukuru wote walisababisha kufanikisha show zote mbii. One love
FLEVA DJS MORE THAN DJS

No comments: