Saturday, June 5, 2010
CHUCHU AFARIKI DUNIA
Mmiliki wa Radio binafsi iliyopo Zanzibar almaaruf CHUCHU FM amefariki dunia leo mjini Nairobi nchini Kenya ambako alikwenda kwa matibabu ya maradhi ambayo kwa mujibu wa madaktari ni kwamba white cells zake zilikuwa ni chache zilishashambuliwa na vijidudu.
Yussuf Aley Chuchu aliwahi kumiliki bendi ya Chuchu Sound iliyokuwa ikitesa vkwa miondoko ya miduara kabla ya kuanzisha Studio ya kurekodia ya Hert beat Record na hivi sasa ameanzisha Radio inayofahamika kama Chuchu Fm.
Chuchu pia kabla ya kufariki kwake alikuwa pia ni mjumbe wa Busara Promotion na pia alikuwa ndie aliyekuwa dhamana ya ukumbi wa Ngome Kongwe.
Yussuf Chuchu anakisiwa kuwa alikuwa na umri wa miaka 51 lakini kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mke wake yupo nchini Marekani lakini hajabahatika kupata mtoto yoyote yule hadi anafariki dunia.
Uongozi wa Flava DJs na Zenji Fm Radio unatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu.
Mungu amlaze mahali pema peponi AAMIN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment