Wednesday, June 2, 2010
KWELI NYIMBO YA RASTA MAN NILIOTOA ILI NILIZA STUDIO
Leo mchana kwenye kipindi changu cha The crush ilinibidi nimtafute Mb Dog ili tuzungumzie wimbo wake wa Rastaman ... Nilifanikiwa kumkamata kwenye line na mazungumzu yetu hasa yalikuwa kutaka kujua hasaa hisia zake kwenye wimbo huu wa rastaman
Mb dog aliniambia wimbo huu wa Rastaman aliyoyaimba yote ni kutoka moyoni mwake na yana mgusa kabisaaa. kiasi kwamba wakati anaweka voko za nyimbo hii bc alimwaga machozi . Producer aliekuwa anarikodi wimbo huu Man water ilibidi amnyamazishe
Wakati anaimba na hadi kufika hatua ya kulia hakujua kama man water alikuwa anarikodi kile kipande . Baada ya kutoka wimbo ndio anaona ile sehem producer hakuitoa ameweka vile vile
Suala jengine ilikuwa vipi ana mpago wowote kuhusu kurudi kwenye Tip top. Mb dog aliniambia si rahisi kwa sasa . Kwa sasa si rahisi Mpaka jamaa wanilipe Hela zangu . Kwani nimefanya mambo mengi sana na nnawadai hela zangu nyingi. Aliniambia nimefany a kazi kubwaa sana tena sana . Tip top ilikuwa haijulikani sisi pamoja na mimi ndie tulieitangaza Tip top. na kuileta juu. Imekuwa na kujulikana hatiame wanaanza kutuzadharau.
Mb dog aliendelea lusema a tayari kishafatwa eti arudi tena kwenye kundi hilo, Ameambiwa mpaka uogozi pia umebadilika kwa sasa. bt yeye bado kurudi mpaka alipwe cha kwake anacho dai na ahakikishiwe mikataba mipyaa sio arudi kichwa mchugwa tu
Mb dog amesema kwa sasa yupo na jamaa mmoja ambae ndie anampa suport na wanajipanga kwa mikataba endapo mambo yatakuwa mambo bc atamtangaza kama ndie manager wake mpyaa
bt kwa sasa bado.
Mchzi kwa sasa ndio ameachia hii pini ya Rastaman ambayo anaonekana kunungunika sana. Pia ameniambia wapenzi wake wakae mkao wa kula kwani Pini za haja za malove davi zinakuja soon
Ni hayo tu kutoka kwa Mb Dog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment