Saturday, June 26, 2010

PICHA ZA MUSIC AWARDS JANA INFO ZINAKUJA SOON


Picha ya walioshinda Tuzo wote

Ali kiba Ndie msanii aliye wapagawisha jana kwenye Tuzo

Dj sum ndie aliekuwa Dj wa show ya jana. Hapa akiwa na Aziza wazir kheri mtangazaji wa Zenjifm

Kushoto ni Rama B ambae alikuwa Mc wa shughuli mimi nikiwa na Aziza Mtangazaji wa Zenjifm na kushoto ni Issa Msabah ambae alikuwa Technician wa Radio kwa ajili ya live

Mb skwash hapa akiwa na Aziza

Juma 20 hapa wakiwa na Dj sum katikati na kushoto ni Rico singo

Juma 20 akiwa na Manager wake Ndugu Seif Mhamed alievalia shirt nyekundu pamoja na Rafiki zake . Juma 20 alinyakuwa tuzo ya Wimbo bora wa kizazi kipya. June jully

Wafanyakazi wa ZMCL mwanzoni hapo ni Dada Winnie alievalia nguo nyekundu akifuatiwa na Ndugu Seif Mhamed.. ambae ndie Manager wa Zenji Entertainment.akifuatiwa na Abdull khafar . wakionekana kwenye pozi pamoja na Ali kiba

Manager wa ZMCL Bw Juda Mapunda hapa akiwa ameshikilia tuzo akiwa kwenye pozi sambabmba na Mh Seif Hatib Wazir anaeshughulikia mambo ya Muungano

Mwanamziki bora wa mwaka Rico singo hapa akiwa kwenye pozi na Msanii bora chipukizi wa mwaka Dida wote hawa wanawakilisha Jupiter Record

Kushoto ni Msanii Metaya akifuatiwa na Dj G au Gulu ramadhani pozi lapamoja na Rico singo pamoja na Producer bora wa mwaka Ndugu Aron name

Hapa ni mimi (Dj side) Nilievalia Suite kama F B I au Agent Jack bowa wa C T U(ndani ya 24)Mbele yangu ni Msnaii Metaya, Producer Aron name na Rico singo

Mtangazaji wa TVZ Has T akiwa kwenye pozi na Baby J,Rico singo, Dida na Metaya

Huyu ndie Bwana Duuu au Mc Duu Mmiliki wa Zanzibar One mordan Taarab hapa akichukuwa Tuzo ya Album bora ya mwaka Iitwayo KAMA NI RAHISI

Berry Black akiwa kwenye pozi na Mtangazaji wa Bomba Fm. Sadiki almaaruf Flash wa pekee. pamoja na Rafiki yao. kwenye pozi la pamoja wakishow love kwenye Tuzo zilizofanyika juzi. Berry Black mwaka huu yeye hakushiriki tuzo hizi

Juma 20 hapa akiongea kilughaa au kimombo baada ya kutangazwa kuwa ameshinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka mziki wa kizazi kipya .. Pia juma 20 alipata nafasi ya kutoa burudani. Jamaa nimemkubali kwenye stage . Alijiandaa vizuri kwani alipanda na Stage show wake wa FACE 2 FACE na kuonesha maajabu . Show ilikuwa mzuka sana


Rico singo akiongea mawili matatu baada ya kushinda Tuzo ya Mwanamziki bora wa mwaka Mziki wa kizazi kipya

Manager wa Zanzibar Petroleum Bw Colin hapa akimkabidhi tuzo Bi Fatma Mbarouk Tuzo ya Msanii bora wa kike wa Taarab asilia


Hawa ndio Dancers wa Face 2 Face wakionesha umahiri wao wa kucheza mbele ya Mgeni rasmin wa siku hii Bi Asha Abdallah Juma Waziri wa kazi maemdeleo ya vijana wanawake na watoto ndani ya ukumbi wa Salama hall Bwawani

Huyu ndie Dida aliechukuwa Tuzo ya Mwanamziki bora chipukizi wa mwaka huu

Hapa Dida akitoa shukrani kwa waandaaji wa Tuzo hizi baada ya kukabidhiwa Tuzo yake ya Msanii bora chipukizi wa mwaka

Dorica hapa akionekana kafurahi sana akipoke Tuzo baada ya kutangazawa kashinda Tuzo ya Msanii bora wa kike Mziki wa kizazi kipyaa.

Huyu ndie Mrembo aliekuwa akipeleka tuzo kwa wahusika anaitwa Sophy.

Mh Seif Hatib ambae ndie mmiliki wa kituo cha Radio ya Zenjifm kilichoandaa Tuzo hizi hapa akitoa nasaha zake kwa wasanii

Mgeni Rasmin wa Tuzo hizi Bi Ashaa Abdallah Juma Waziri wa kazi maemdeleo ya vijana wanawake na watoto. akiwa na Mh Seif Hatib katika maadhimishow ya Utoaji tuzo hizi ndani ya Ukumbi wa salama Hall bwawani

9 comments:

Anonymous said...

ZMA ya mara hii ilikua njema lkn aliyefunika si ali kiba, sijui kwanini akaweka huyu, madansa wake walikua wavivu jukwaani, its like aliwaburura tu hakufanya nao mazoezi

MSEMA UKWELI

Anonymous said...

Tunzo za mara hii zimekwenda suluhu, nimependa, kwanza hata trophy yenyewe haikua rula kama ya mwaka jana, si mchezo, miaka ya mbele tutegemee mabadiliko zaidi...big up zmcl

tasha...au nutasha

Anonymous said...

SIKUPENDA PRESENTATION YA ALI KIBA, MASHABIKI WAKE WALIKUA KAMA HAWAPO SERIOUS...LKN BABY J NA JUMA20 WAMEFUNIKA...NA MADANCA WA FACE TO FACE KIBOKO!

Anonymous said...

Tukio zima lilikua poa lkn sijapenda stage la music awards...lilikua too local, nilitegemea some thing digital lkn instead nimekuta kitu kama stage la harusi, kama mwaka jana, taa zilikua too shiny,,, kwa nini muangaza usiwe mkubwa zaidi pale kwenye stage tu? halafu yale maspika yalikua yanazinnga watu pale juu...hakukuwa na uwezekano wa kuwekwa chini? hayakua hata maspika mazuri kwa kupamba...

Anonymous said...

Yaani nimeona kitu kimenichekesha kweli,kwenye hizo tunzo nyengine it's ok ndo kwanza tunaanza,lakini kwenye tunzo ya albulm bora ya taarab inatia kichefuchefu waungwana.hivi hiyo nyimbo ya kama ni rahisi imetoka mwaka huu?wapi imewahi kutokea katika dunia hii alietoa copyrights akapewa tunzo?si mnaelewa nyimbo hiyo imetungwa na culture musical club?na kama sijakosea imetoka ends of 1980's?kwanini wasipewe wenyewe hiyo tunzo?we are living in 80's au 2010?category inasema nyimbo bora ya mwaka,khaa!jamani huu ni mwaka 1986?au 2010?huku dar hamuoni tunzo zinavyokwenda?hazikuwahi kuimbwa nyimbo za zamani huku?sikatai nyimbo nzuri lakini category inasema wrong na nyimbo yenyewe,si bora mungelieka category ya zilizovuma zamani ndipo hiyo nyimbo ipewe?au ndio kwanza mnaisikia?zanzibar one hawakustahiki kupewa hiyo tunzo na waombeni radhi wenyewe kikundi cha mila na utamaduni au culture.mfano leo mimi nikainunuwe nyimbo ya seif salim inayoitwa nipepee then niirekodi upya tunzo nitunzwe mimi kwa kipi?pesa niliyonunulia?au upigaji niliyoupiga?hamfahamu kwamba kila kitu nimekikuta ready made?inatia kichefuchefu.

Anonymous said...

Tunzo ya albulm bora ya mwaka ina maana albulm ilitotoka mwaka unaozungumzwa,na huu ni mwaka 2010,huko kwetu zanzibar mbona kila kitu kiko kinyume?hao zanzibar one badala ya hiyo nyimbo kama ni rahisi wana nyimbo nyengine?iliyorekodiwa mwaka huu? ipi?hivi waungwana albulm hatujuwi maana yake?ni bora ya hata mungesema singo bora ya mwaka ambayo pia ina makosa,kwa maana hiyo nyimbo haijatoka mwaka huu,tangu 1984,inaonesha wazi kuna mapeano ya tunzo mnavyofikiri nyie,ila mnapotosha umma na mnaurudisha music nyuma,ikiwa mwaka huu mmeipa tunzo nyimbo iliyotoka miaka hiyoo ya nyuma,na mwakani watu wataumiza vichwa kutunga/si watanunua kwa malindi nyimbo nyengine?sasa tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?eti albulm bora ya mwaka??!kichefuchefu khasa?albulm nyimbo moja?tena ilyorekodiwa harusini?

Anonymous said...

Hizo tunzo ki upande wa taarab jaribuni kufikiria upya,nna hakika music wa taarab tumeuanza sisi wazanzibari,kwa ushahidi ya kwamba ipo ocherstra zanzibar imeanza tangu 1905,nayo ni nadii ikhwaan safaa,na zipo nyimbo lukuki zilizovuma miaka ile,kama mnataka kuwaenzi wazee wetu waliotangulia kwanini isiwepo category ya zilizovuma zamani?na tena wapewe walo release mwanzo wimbo husika,eti zanzibar one?situkani la khashaa,lakini ki ukweli khasa mloandaa hizo tunzo mnafaa kushitakiwa ki sheria,kwanini tunzo za hao kina baby j,na aroon name wapewe kulingana na nyimbo walizotoa mwaka huu,halafu taarab iwe kinyume yake?na sisi ndio mabingwa wa taarab duniani?mnakula rushwa ya wazi wazi,au ufahamu wenu ni mdogo kama maisha ya funza.

Anonymous said...

HIVI NIULIZE SUALI?KILA NIKIZIANGALIA HIZI PICHA ZENU ZA HII INAYOITWA ZANZIBAR MEDIA,AMBAYO NDIO WASIMAMIZI WA HIZO TUNZO ZA KUPEANA?!NDIO WAHUSIKA WENYEWE?NATAFUTA WA KUMSHTAKI ALIETOWA TUNZO YA ALBULM BORA YA MWAKA YA TAARAB NIMUULIZE KWA KIGEZO KIPI?AMEWAPA ZANZIBAR ONE?NI MZANZIBAR KHALISI?NISIWE NASEMA HAYA KUMBE MMEAJIRI MFARANSA KUTOA TUNZO,AMBAE KWA HAKIKA HAKUWAHI KUISIKIA HII NYIMBO, (KAMA NI RAHISI,)NA IKIWA NI HIVYO BASI WAUNGWANA HAMNA KOSA,NA SAMAHANINI SANA,LAA KAMA NI WAZANZIBAR NDIO MLOKHUSIKA MNATIA KICHEFUCHEFU KHASA.

Anonymous said...

Naelewa vzr comments lazima ziwekwe hadharani watu wasome,na hii blogger wahusika ni zenj fm 96.8 na dj side,nisipoziona hizi wewe ndo wa kwanza mnaorudisha music wetu nyuma.au hii blogger ifungwe kama ilivyofungwa ze utamu,maana itapotosha watu wengi,wengi hatukuwepo wala kusikia habari za music awards za zanzibar lakini kupitia hii blogger imetufungua macho kuona uozo uliotendeka huko kwetu visiwani,na nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuitangaza hii blogger asaa kheir mtapata mawazo mengi sana kupitia hapa.