Tuesday, April 26, 2011

DULLY SYKES....KUISHITAKI KAMPUNI YA SIMU TZ?


Mkali toka pande za Ilala,Dully Sykes amefunguka kuwa huenda akaishitaki kampuni moja ya simu nchini Tanzania kwa kuuchukua wimbo wake mpya unaopata airtime ya kutosha kwa sasa Afrika Mashariki,Bongo Flava na kuutia kwenye caller tunes zao bila ridhaa yake! Dully alifunguka "Nashanga jamaa wa (jina kapuni) wameuchukua wimbo wangu bila ridhaa yangu na kuuweka kwenye caller tunes zao,na wakati wao wataingiza mkwanja mi sipati kitu,na mimi nimejisajili pamoja na track yangu kwa vyombo vinavyohusika kama ni mmiliki halali wa wimbo wa Bongo Flava,na yoyote atakayeutumia bila ridhaa yangu anavunja sheria"

Mwaka jana Atrist toka Kenya,DNA alitishia kuishitaki Benki ya KCB kwa kuchukua wimbo wake wa Banjuka na wao kuutumia kwenye promotion ya account kwenye TV na Radio na kuiita Bankika Tu!

No comments: