Tuesday, December 29, 2009

VETO IKO KITAANI MASELAA


Baada ya kuzindua albamu yake ya 10 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam wiki iliyopita, mkongwe Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ tayari ameiingiza sokoni santuri hiyo yenye jina la Veto ambayo ina jumla ya mawe 10 ya adabu.

Mr. II a.k.a Sugu, aliingiza albamu hiyo juzi (Jumamosi) na amesema kwamba kazi hiyo itauzwa kwenye maduka ya wazalendo nchi nzima.

“Mapambano yanaendelea, albamu ipo mtaani sasa,” alisema Sugu, alipoongea na kona hii, wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu.

Albamu hiyo, imetengezwa nchini Marekani chini maprodyuza Puzo na Stigo katika Studio ya S&S iliyopo mjini Brocklyn.

Baadhi ya wasanii walioingiza vocal kwenye kazi hiyo ya Sugu ni Prof. Jay, MwanaFA, Balozi Dolla Soul, Solo Thang na wengineo.

Mbali na hilo, Sugu alisema nasi kwamba video ya Hold On tayari imekwishaanza kuchezwa na vituo vya runinga na kueleza kuwa imegharimu zaidi ya dola za Marekani 8000.

CHEGE ALBUM YA TATU IKO SOKONI


Albam ya tatu ya mtu mzima Chege Chigunda inayokwenda kwa jina la Karibu Kiumeni iko mtaani tayari na mikoani kote, ina ngoma 12 na amewashirikisha wasanii kibao kama Mangwear, Lady Jide, Q. Chilla, Wahuu kutoka Nairobi, Wyre kutoka Nairobi na Pipi.
Anasema album imeshiba ngoma zote kali na anawaomba watu wake wamsikilize alichokisema

Sunday, December 27, 2009

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2010 LAWIVA



Mtanange wa saba wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 11 hadi 16 Februari 2010; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla saa kumi na moja.

Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar

Likionyesha wasanii maarufu na wanaochipukia na waliofanyiwa uteuzi makini zaidi ya 400 (vikundi 40 kwa jumla), Sauti za Busara imeweza kuthibitisha kuwa ni tukio kubwa na bora zaidi la muziki hapa Afrika mashariki, ni tukio linalowaunganisha watu katika mazingira ya kusherehekea.

HAWA NDIO WASANII HADI SASA WATAKAO KAMUA 2010
Thandiswa (South Africa) Malick Pathé Sow (Senegal) Fresh Jumbe & African Express (Tanzania / Japan) Simba & Brown Band (Mozambique) Banana Zorro & the B Band (Tanzania) Nyota Ndogo (Kenya) Jimmy Omonga (DRC / NL) Jhikoman (Tanzania) Mzungu Kichaa (Denmark / Tanzania) Makadem (Kenya) Ikwani Safaa Musical Club ft Tamalyn Dallal (Zanzibar / USA) Del & Diho (Mayotte) Mari Boine (Norway) Dawda Jobarteh (The Gambia) Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden) Xova (UK) Massar Egbari (Egypt) Debo Band (Ethiopia / USA) Bamba Nazar & The Pilgrimage (Suriname / NL) Joel Sebunjo & Sundiata (Uganda) Juliana Kanyomozi (Uganda) Maureen Lupo Lilanda (Zambia) Tausi Women's Taarab (Zanzibar) Mim Suleiman (Zanzibar / UK) Swifatui Abraar Group (Tanzania) DJ Eddy (Zanzibar) DJ Yusuf (UK / Zanzibar) Sowers Group (Tanzania) Best of WaPi (Tanzania) Sosolya Dance Academy (Uganda) Mapacha Africa (Kenya) Sinachuki Kidumbak (Zanzibar) Shirikisho Sanaa (Zanzibar) Tunaweza Band (Tanzania) KVZ Tupendane (Pemba) Keita & Swahili Vibes (Zanzibar) Maia Von Lekow (Kenya) na wengineo.

NANI ATASHINDA MILLION MBILI TASILIM ?


Mshindi wa mpambano wa kumtafuta mfalme wa jukwaa katika tamasha lililopewa jina la ˜Hip Hop Battle King of Stage anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh milioni mbili.

Mchujo wa kuwapata washindi ambao watashindana mwezi machi katika fainali utafanyika siku ya sikukuu ya mwaka mpya Januari mosi kwenye ufukwe wa Coco beach, ambapo kiingilio kitakuwa ni sh 5000.

Akichonga na The Crush kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga Masoud Kallapina amabye ndiye anayeratibu shindano hilo alisema mshindi wa pili atapata fursa ya kurekodi albamu nzima katika studio ya 41 record na watatu atarekodi albamu nzima kwenye studio ya Kikosi record na mshindi wanne na watano watarekodi nyimbo moja moja kila mmoja Kikosi record.

Alisema pia kutakuwa na shindano la Freestyle ambapo watakaoshiriki katika shindano hilo ni Dogo sajo, Niki mbishi, Godzillah, Lufunyo na Rage.

Huu mpambano wa kumaliza ubishi wa nani mkali wa Hip Hop Tanzania

BABA MZAZI WA MSANII ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA


Baba mzazi wa Albert Mangwear leo asubuhi amefariki dunia, baba huyu alikuwa anaishi Morogoro. Mazishi ya baba yake Albert ambaye alikuwa anajulikana kwa jina la KENNETH B. MANGWEHA yatafanyika huko kwake alipokuwa anaishi Morogoro. Mzee wetu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

Saturday, December 26, 2009

Friday, December 25, 2009

MERRY X MASS $ HAPPY NEW YEAR


DJ SIDE First lemmie start by saying thanks to all Zenjfm FANS and The CRUSH listerners for all the support you have given me. Got nothing to give you back but all my love, this is my wish for you:
Peace of mind, Prosperity through the year, Happiness that multiplies, Health for you and yours, Fun around every corner, Energy to chase your dreamz and joy to fill your holidays.
MERRY X MASS AND HAPPY NEW YEAR.

Tuesday, December 22, 2009

TATIZO LA UMEME ZNZ KIZAAA ZAAA WAZIRI ASEMA SI CHINI YA MWEZI MOJA NDIO UPO UWEZEKANO WA KURUDI


Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja itaendelea kukosekana kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kuripuka kwa kifaa kingine cha kugawia umeme katika kituo cha Fumba.
Akizungumza na wandishi wa habari waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema hitilafu hiyo imetokea wakati mafundi walipokuwa wakijaribu kurejesha huduma hiyo iliyokosekana kwa kipindi cha wiki mbili.
Amesema kifaa kilichoharibika cha Spliter hakiko madukani na kinahitaji kutengenezwa, lakini kutokana na wakati huu wa kusherehekea siku kuu ya Krismas na mwaka mpya utengenezaji wa kifaa hicho utachelewa.
Hivyo amesema uwezekano wa kurudi tena huduma ya umeme kwa kipindi cha mwezi mmoja ni mdogo sana Aidha waziri Mansour amewataka wananchi kuendelea kuwa na moyo wa subira huku serikali ikiendelea na juhudi za kurejesha huduma hiyo muhimu
Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja ilikatika Desemba 10 mwaka huu baada ya kuripuka njia ya kupitishia umeme katika kituo cha kupokelea umeme kutoka Tanzania bara cha Fumba
Bonyeza hapa kumsikiaa Waziri akieleza tatizo la umeme (Waziri)

Sunday, December 20, 2009

MANGWEA AACHIA PINI MPYAA KWA AJILI YA X MASS



Nyota wa Hip Hop Albert Mangwea ambaye anatamba sokoni na album yake ya Ng'e, atawapa zawadi ya xsmas mashabiki wake kwa kuachia wimbo mpya uitwao TUKO JUU.
Mangwear amesema wimbo huo amemshirikisha George Kasela 'Squeezer' na Steve E, ikiwa imefanywa katika studio kongwe za Bongo Rec chini ya mtu mzima P. Funk.
Namnukuu "Ni kitu kimetulia mzee kwa kweli, kuelekea katika msimu huu wa sikukuu ya xsmas na mwaka mpya nimeona niwape hii ili waweze kuburudika. Uzuri ni kwamba wakati ninapotoa zawadi hii pia nitatoa na video yake na ya wimbo wangu mwingine wa CNN"
Hii ni album ya pili ya msanii huyu ikiwa sokoni, tokea alipoanza kujishughulisha na shughuli za mziki huu wa kizazi kipya. Ikiwa inasambazwa na FM Wasambazaji.

MZEE ZAHIR ALY ZORO AKAMUA NA VIJANA BONGO FLAVA



Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Zahir Ally Zorro, katika kuonyesha ukomavu ameingia studio na nyota wa bongo fleva nikimaanisha Mr. Blue & Baby Boy na kutengeneza kibao kikali kitakachokuwa kwenye miondoko ya Hip Hop.
Mzee Zorro amefurahi sana kufanya kazi na vijana wake lakini amefurahishwa zaidi na aina ya muziki anaokwenda kucheza. Anapenda hip hop na anaamini ataweka ladha ya aina yake katika nyimbo hiyo alisema.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mkongwe huyo kushirikiana na vijana wa bongo fleva, kwani aliwahi kufanya kazi pamoja na nyota mwingine wa Hip hop Farid Kubanda katika kibao kilichoitwa Ripoti za Mtaani.
Zahir hivi sasa anatamba na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Barua pepe wakati Mr. Blue na Baby Boy nao wanafanya vizuri na nyimbo zao walizotoa hivi karibuni.

Wednesday, December 16, 2009

DOWLOAD PINI MPYAA YA BEEZ NA C PWAAA



Kamatia pini mpyaa ya Beeze na C pwaaa ngoma inaitwaa They Don´t Wanna See. Bonyeza hapa ili uwezee kudownloadd

AY ANAKUJA KUFUNIKA NA PINI LAKE JIPYAA ( KINGS AND QUEEN)



Mambo vipi?
Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa katika video yangu mpya inayoitwa KINGS AND QUEENS niliyomshirikisha JOKATE & AMANI kutoka KENYA.Wimbo umetayarishwa na na Super Producer HERMY B ndani ya Studio ya B.Hitz Music Group na kufanyiwa video na OGOPA DEE JAYS toka Kenya.Video ilifanyika Jijini Nairobi na itaanza kuruka wiki ijayo MTV BASE na vituo vingine ndani ya Afrika Mashariki.
Wimbo huu nimejaribu kufikisha fikra zangu kuwa MWANAMKE WA KIAFRIKA NDIE BORA KABISA NA NAJISIKIA FAHARI SANA KUZALIWA NAO NDANI YA BARA MOJA.
Kama nilivyosema TUNAUFUNGA MWAKA NA KUUFUNGUA NA MZEE WA COMMERCIAL basi subirini mambo makubwa toka kwa MZEE WA COMMERCIAL AMBWENE YESSAYAH MWENYE KIU YA KUWAKILISHA TANZANIA NA AFRIKA YA MASHARIKI KWA UJUMLA KATIKA ANGA ZA MBALI.
Pamoja sana

MWANAMUZIKI WA JAHAZI MORDAN TAARAB ABUKUA DIPLOMA YA UWAANDISHI


Mwimbaji nyota wa kundi la muziki wa Taarab la Jahazi Morden Taarabu, Mwanne Othman (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wenzake mara baada ya kupokea cheti cha uhitimu wa Diploma ya uandishi wa habari katika mahafali ya 15 ya chuo cha uandishi wa habari (DSJ ) yaliyofanyika jijini Dar wikiendi ilopita. kuShoto ni Mwajuma Njama na kulia ni Salama Saleh.
Hii ni changamoto kwa wanadada na kwa wasaniii. sio unakaaa kwenye jukwaaa na Mic tuu... Elimu muhim .., Hongera Dadaaaa.. sasa Tunataka mipasho ya ukweli...

Tuesday, December 15, 2009

NAKAYA NA MRISHO POTO KUWARUSHA KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI MWEZI HUU



Mwana Dada Nakaaya, ambae kwasasa yupo chini ya lebo ya Sony BMG Na Mrisho Mpoto, Maarufu kwa style yake ya Mashairi Wamepata mualoko wa kukamua kwenye Tamasha Asilia la kizimkazi Ndani ya Zanzibar ambalo litakuwa la siku tatu kuanzia 29th to 31st December 2009 Wasanii kazaa wa Asilia kushiriki wakiwemo Bi Kidude, Mama C, Zawose, Msafiri, Borafya and Clockwise.
Kauli mbiu ya Tamasha hili ni “Usafi Kama Kawa” kwa maelezo zaid tembelea www.kizinoor.org

Monday, December 14, 2009




Lile bifu la wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohammed ‘TID’ na mwenzake Shabani Katwila ‘Q-Chiller’ lililoripotiwa hivi karibuni, limechukua sura mpya baada ya soo lao kutinga polisi.

Taarifa zilizotufikia zimedai kuwa, bifu la wawili hao limefika polisi baada ya juzi kati Q-Chiller kuanza kumsaka mwenzake huku akiwa na silaha.

Akilonga na DHW, Meneja wa TID Khamisi Dakota alisema kuwa, Desemba 8 mwaka huu, akiwa maeneo ya Magomeni, Q- Chief alimvamia akiwa na wenzake wanne na kuanza ‘kumjazia inzi’ huku akimuuliza aliko TID.

Hata hivyo, kutokana na mazingira ya kutokuelewana kati ya wawili hao, inadaiwa Q-Chiller alianza kumsemea mbovu Dakota na mwishowe kuchomoa kisu na kutaka kumchoma.

Kufuatia hali hiyo, Dakota alikwenda moja kwa moja kuonana na TID ambapo walishauriana kulifikisha suala hilo polisi ambapo walikwenda kituo cha Magomeni na kufungua jalada la kesi lenye namba Mag/RB/22117/09 kutishia kuua kwa kisu.
Kumbuka kuwa tayari Q chila alishatangaza wazi kwenye kituo kimoja cha Tv hapa nyumbani eti Tid amemrogaa. Amemfanyia mambo ya kiuswahili … lakini chanzo cha haya yote ni mkwanjaaaa.. Q chila alikuwa akishutumu juu ya malipo aliokuwa akipata wakati walipokuwa ndani ya Bend yao Top Band kabla ya kujitoaaa

Sunday, December 13, 2009

TATIZO LA UMEME KIZAA ZAAA



Tatizo la umeme Zanznibar laleta kizaa zaaa jionee mwenyewe watu wakipata taabu juu ya huduma ya maji . Kumekuwa na msongamano mkubwaa kwenye baadh ya mifereji ambayo inatoa maji. . Baadhi ya mitaa Maji ni tatizo suguu. nimepata habari baadhi ya mitaa kama michenzani Dumu la maji sh/ 1000. ukitaka kupandishiwa juuu basi unalipa sh/1500. Mitaa mengine kama Magomeni , Jangombee, Nyarugusu nk. Dumu la maji ni sh 500.

MIKANDAMIZO YA AMANI NDANI YA DOM


Duu? lakini hana mvuto wa miguuu!!!! Ana miguuu ya kiumee!!! au?

Mwana dada Amani kutoka kwa watani wetu Kenyaa akifunika mbaya nyumbani kwewenye tamasha la Str8Muzik Festival;Intercollege Special 2009 ndani ya viunga vya hoteli ya Royal Village mjini Dodoma ,Tamasha hilo huandaliwa na kampuni ya Sigara TCC kupitia chapa yake ya muziki ya Str8Muzik,ambapo mpaka sasa limekwishafanyika mikoa mitatu ikiwemo Dar,Mwanza na Dodoma na sehemu zote hizo tamasha hilo lilipokelewa kwa shangwe.

ZANZIBAR UMEME TOTOROO , GIZAAA HUUHAAA!!!1


Hii ndo hali ya Zanzibar!!!

Tanzania bila Ufisadi tutafika?Je Zanzibar Bila Umeme inawezekana?Kuchaji simu 500,Saluni kichwa 2000,Soda 1000,Juice 500,Barafu 200,Maji ya kawaida hayapatikani,Wanaofaidika sasa ni Wazinifu na wizi,Sasa wewe ulioko nje ukijaribu kupiga simu kwa ndugu zako ZNZ usishtuke zikiwa zimefungwa ufahamu hakuna matatizo ila ni umeme tu.


Waziri wa maji ameshatangaza mapema mwakani (2010) umeme utapatikana,Je tatizo kama hili sasa linataka kupelekwa Pemba?Tayari Mh.Karume ashapokea kila nyenzo za kutandaza umeme kutoka Tanga,lakini Je hafahamu kwanza usipoziba ufa,Utajenga Ukuta?