Sunday, December 20, 2009

MANGWEA AACHIA PINI MPYAA KWA AJILI YA X MASS



Nyota wa Hip Hop Albert Mangwea ambaye anatamba sokoni na album yake ya Ng'e, atawapa zawadi ya xsmas mashabiki wake kwa kuachia wimbo mpya uitwao TUKO JUU.
Mangwear amesema wimbo huo amemshirikisha George Kasela 'Squeezer' na Steve E, ikiwa imefanywa katika studio kongwe za Bongo Rec chini ya mtu mzima P. Funk.
Namnukuu "Ni kitu kimetulia mzee kwa kweli, kuelekea katika msimu huu wa sikukuu ya xsmas na mwaka mpya nimeona niwape hii ili waweze kuburudika. Uzuri ni kwamba wakati ninapotoa zawadi hii pia nitatoa na video yake na ya wimbo wangu mwingine wa CNN"
Hii ni album ya pili ya msanii huyu ikiwa sokoni, tokea alipoanza kujishughulisha na shughuli za mziki huu wa kizazi kipya. Ikiwa inasambazwa na FM Wasambazaji.

No comments: