Tuesday, December 29, 2009

VETO IKO KITAANI MASELAA


Baada ya kuzindua albamu yake ya 10 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam wiki iliyopita, mkongwe Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ tayari ameiingiza sokoni santuri hiyo yenye jina la Veto ambayo ina jumla ya mawe 10 ya adabu.

Mr. II a.k.a Sugu, aliingiza albamu hiyo juzi (Jumamosi) na amesema kwamba kazi hiyo itauzwa kwenye maduka ya wazalendo nchi nzima.

“Mapambano yanaendelea, albamu ipo mtaani sasa,” alisema Sugu, alipoongea na kona hii, wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu.

Albamu hiyo, imetengezwa nchini Marekani chini maprodyuza Puzo na Stigo katika Studio ya S&S iliyopo mjini Brocklyn.

Baadhi ya wasanii walioingiza vocal kwenye kazi hiyo ya Sugu ni Prof. Jay, MwanaFA, Balozi Dolla Soul, Solo Thang na wengineo.

Mbali na hilo, Sugu alisema nasi kwamba video ya Hold On tayari imekwishaanza kuchezwa na vituo vya runinga na kueleza kuwa imegharimu zaidi ya dola za Marekani 8000.

No comments: