Sunday, January 31, 2010
BEBE COOL ASHAMBULIWA KWA RISASI
Mwanamuziki mashuhuri wa reggae nchini Ugandan, Bebe Cool a.k.a Moses Sali, akiingizwa katika hospitali ya Nsambya jijini Kampala baada ya kupigwa risasi katika klabu moja jijini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la The Monitor, risasi hizo zimevunja miguu yote miwili, amesema Daktari Mrakibu wa hospitali hiyo, Dk. Martin Nsubuga says.
Habari zinasema risasi zilirindima katika klabu ya Effendys katika maeneo ya Centenary Park, na kwamba kuna utata wa sababu zilizopelekea purukushani hilo. Inasemekana watu wengine watatu ikiwa ni pamoja na mabaunsa wa Bebeb Cool na askari wa kikosi maalum pia walijeruhiwa.
Thursday, January 28, 2010
AY NEW VIDEO CHECK IT OUT!
AY ameachia video yake mpyaa inayoitwa "Kings & Queens akimshirikisha Jokate Mwegelo na Mwanadada Amani..Mwanamitindo wa Zanzibar Farouk Abdallah ndie aliebeba dhamana ya kuwapangia mavazi na style nzima ya video hiyo.
Wednesday, January 27, 2010
UCHAWI NI WAIKUMBA ZENJI FLAVA
Hivi kwa nini mwanadamu hawezi kufanya mambo yake kwa kujiamini hadi atumia vitu vya ajabu na kutoa shutma zisizokuwa na msingi katika maisha yake?Nauliza suali hili kutokana na kile kinachoendelea hivi sasa katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya kwa upande wa Zanzibar almaarufu Zenji flava.
Kipaji ni kipaji tu kama kipo hakiwezi kuondolewa na mwanadamu isipokuwa kwa nguvu za muweza.
Hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya makundi ya muziki wa Zenj flava yakisambaratika na mengine kugombana na kuhasimiana kwa sababu zisizokuwa na msingi.
Miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na kundi la Offside Trick,kundi ambalo ni miongoni mwa makundi na wasanii waliochangia kusimamisha a muziki wa Zabnzibar kwa asilimia kubwa.Tulishuhudia baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo wakigombana na kushutumiana kwa mambo yasiyokuwa na msingi kwani endapo kama wahusika wangeyasulihisha wenyewe yote yasingetokea
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotegemewa na wengi mmiliki wa studio ya Teddy Records, Ahmed almaarufu Tguay ameibuka na kudai kuwa hana mafahamiano mazuri na Berry Black aka mfalme wa Zanzibar
Bifu la Berry Black na Tguay linaonekana kupamba moto baada ya madai kuwa msanii huyo aliyetamba na vibao vyake vingi vya kimapenzi kuwa amempa udaku producer wa kuaminika na kutegemewa wa Tguay katika studio yake ya Teddy Records mjanja kutoka kule nchini Kenya Shirko.
Habari za kuaminika zinasema kuwa kwa sasa Berry Balck ameshahama katika nyumba aliyokuwa akiishi ambayo ni nyumba ya kina Teddy na kwa sasa anaishi kimpango wake Kwa Upande wa Shirko inadaiwa kuwa yeye na Teddy kwasasa hakuna stori zaidi ya salam.. Na kwa mujibu wa Shirko Anasema yumo mbioni kufungua studio yake hapahapa ZNZ
Jee nani mkweli?? Tutafika wapi endapo watu wanaanza kubweteka kwa kupata mafanikio kidogo tu?? Na ni kwanini wasanii wasiwe kitu kimoja il.i kuliendeleza gurudumu kla muziki huu ambao unaonekana kuwagusa wengi hasa vijana ambao wengi miongoni mwao ndio ajira yao ya kudumu?
Tafakari, tafuta jibu na toa maoni yako juu ya hili….tchao beibiiiiiiiiiiii
AFANDE SELE CHID BENZI NDIE MSANII ALIE JUUU KWA SASA
Selemani Msindi a.k.a Afande Sele toka kundi la Watu Pori pande za Motown au Morogoro ameibuka tena lakini safari hii akiongelea anayeamini kuwa ni mtu pekee kwasasa kumvua taji lake la Mfalme wa Ryhmes.
Akichonganasi Afande amesema ya kuwa anaamini kabisa kama kuna msanii wa Bongo fleva anayeweza kumvua taji lake basi ni Chid Benz toka kundi la LA Familia pande zile za Ilala
“Chid ni mkali wa mashairi, ana ryhmes, pia hata kuliburudisha jukwaa anaweza, mimi kwangu Chid ndio yupo juu kwasasa aisee, naweza kusema ndiye pekee anayeweza kuchukuwa taji la Mfalme wa Rhymes kwasasa.” alisema Afande Sele.
Afande Sele ndiye anayeshikilia taji hilo baada ya kufanyika mara moja tu miaka ya nyuma na kukutwa na misukosuko mingi.
lIONEL RICHIE ATIA MAGUU UGANDAA
Hayaa jamani... Juzi tuu Mtu mzima R kelly alitia maguu Uganda nakupiga show ya maana. Ambapo ujio wa R kelly ulidhaminiwa na Zain mtandao wa sim za mkononi .. Wiki haijafika MTN washatangaza kuleta Lionel Richie ndani ya Uganda . Tujiulizee hivi ni lini ZANZIBAR atakuja Msanii mkubwa kuja Kupiga show?
HIVI SANAA BILA YA UCHAWI HAYENDI? H BABA ADAI KAROGWAA
Mmoja wa wanamuziki wanaofanya mtindo wa TAKEU style Hamis Ramadhan “H Baba” ameibuka na kuzusha madai ambayo ni ya kushangaza.
Akiongea na Dar411 H Baba alisema kuwa alitupiwa uchawi na mmoja wa wasanii wenzake ndio maana mambo yake mengi yalikwenda kombo siku za karibuni.
“Unajuwa mtu ataniona mimi kama naongopa lakini ukweli ni kuwa nilichezewa ila nilikuwa sijui nimekuja kungundua baada ya kupita pita kwenye tiba, nilianza kujihisi hivyo mara baada ya kugombana na watu wengi sana nikiwa sijielewi” alisema H Baba
H Baba kwasasa anakiri kupona matatizo hayo mara baada ya kupata tiba toka kwa wataalamu wa miti shamba.
Alizidi kusema “ Unajuwa ni ukweli kabisa waswahili hawakukosea walivyosema kikulacho kinguoni mwako, kwani yote hayo yalikuwa yakifanywa na mtu wa karibu kabisa tena rafiki yangu mkubwa” alisema H Baba kwa uchungu.
Alimaliza kwa kusema “Matatizo mengi yalitokana na Irene, unajua watu wengi hawakupenda niwe na Irene, kwahiyo ili kunikomoa ikabidi waniroge, mimi na Irene tukawa hatuelewani, tunagombana mpaka tukaachana,” alisema H.
Hata hivyo H Baba alikataa kumuweka wazi mchawi wake huyo.
LILIAN AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA FACE OF AFRICA
Hatimaye Tanzania ilipata mwakilishi wake katika fainali za mashindano ya Kisura wa Afrika yanayotarajiwa kufanyika February 6 mwaka huu.
Meneja wa uhusiano wa Multichoice Furaha Samalu alisema kwamba Lilian amefanikiwa kupita hatua ya kumi (10) bora baada ya kupita mchujo wa washiriki wengine 24 kutoka nchi mbali mbali.
Kabla ya kupatikana kwa washiriki kumi warembo hao walikuwa kambini nchini Kenya katika mji wa Mombasa katika kambi maalumu.
Lilian anatarajiwa kuondoka tarehe 26 kuelekea Afrika Kusini tayari kwa fainali hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Nigeria katika mji wa Lagos.
Zaidi ya hayo mbunifu wa kitanzania anayeishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini Anisa Mpungwe amepata nafasi ya kuwaandalia mavazi baadhi ya washiriki watakaoshiriki kwenye fainali hizo.
Lilian ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es salaam amewaahidi watanzania kufanya makubwa na kufwata nyao za dada yake Miriam Odemba kama ilivyokuwa mwaka 1999.
SAUTI ZA BUSARA ZAWIVA ZANZIBAR
Mwanamuziki mkongwe mwenye makazi yake ya kimuziki nchini Japan Fresh Jumbe akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi kuhusu ushiriki wake pamoja na bendi yake nzima katika tamasha la sauti za busara
Hatimaye,kuna habari njema kutoka Zanzibari… Ukiachana na hali mbaya ya kiuchumi ya Dunia iliyoathiri bodi ya Utalii, na ukosefu wa umeme wa muda mrefu, tangu kati kati ya Disemba, hatimaye kuna mtazamo chanya juu ya Tamasha la saba la muziki la Sauti za Busara linalotazamiwa kung’arisha Zanzibar!
“Ni wakati mgumu sana tunajua, lakini juu ya sababu zote! lengo letu ni kusonga mbele, pamoja na Sauti za Busara”, Yussuf Mahmoud anasema, Mkurugenzi wa Busara Promotions. “Tamasha hili ambalo kauli mbiu yake mwaka huu ni MOTO ZAIDI litaleta watu pamoja katika kusherehekea, kuwasaidia vijana wenye uwezo wa kiutamaduni, kuwapa bahati ya kukutana na wasanii wakubwa katika jukwaa moja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine. Lakini si hivyo tu, Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia Tamasha la Sauti za Busara linatuwezesha kuboresha utalii mpya wa kiutamaduni nchini Tanzania.”
“Ni kweli”, tumedhamiria kuendelea, “kukosekana kwa umeme kisiwani imetuletea sote wakati mgumu, lakini tumejipanga na majenereta ya kutosha ili kuhakikisha mambo yote yanaendelea kama yalivyopangwa, usalama umeboreshwa na mpangilio mzuri kwa watazamaji. Ukiwepo umeme au ukikosekana, Sauti za Busara iko TAYARI!”
Labda tuwapashe tu kidogo kuwa; Toleo la saba la sauti za busara linaelekea kuleta “habari nzuri” kwa ajili ya Afrika, wasanii kutoka kona mbalimbali za Afrika wanajongea visiwani tayari kwa burudani. Hivi Mahoteli ndani ya mji mkongwe yamekwisha furika, wawezeshaji wa muziki duniani, wanautamaduni pamoja na waandishi wa habari kutoka pande mbali mbali za dunia wako tayari kuja pamoja kushuhudia nini kinaendelea katika mandhari nzuri ya muziki wa Afrika Mashariki.
Tofauti na miaka iliyopita, Sauti za Busara 2010 linakuja na vionjo adhimu, zaidi ya wanamuziki 400 watapanda jukwaa moja. Mbali na vikundi kumi na mbili kutoka Zanzibar na nane kutoka Tanzania Bara, Tamasha hili pia limeshirikisha makundi ishirini kutoka nje ya Nchi kama vile Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Mozambique, Mayotte, Egypt, Guinea, Senegal, Gambia na Zambia.
Kama kawaida, tamasha hili hutokea kipindi cha sikukuu ya wapendanao hivyo kuongeza ladha zaidi. Kutoka viwanja vya watoto Kariakoo saa kumi kamili za jioni siku ya alhamisi tarehe kumi na moja februari kutakuwepo na maandamano makubwa na ya kipekee yatakayo ashiria ufunguzi rasmi wa tamasha hili la aina yake, wakiwemo wana sarakasi, mdundiko, ngoma na bendi, wote wakielekea Ngome Kongwe hadi itakapofika mida ya saa kumi na moja jioni. Kutoka hapo na kuendelea, kutakuwa na shoo za muziki kwa siku nne , pamoja na vikundi 40 (wanamuziki 400) akiwemo Thandiswa(Afrika Kusini), Nyota ndogo na Makadem (Kenya), Ba Cissoko (Guinea), Malick Pathe Sow (Senegal), Massar Egbari (Egypt), Banana Zorro, Fresh Jumbe, Chidi Benz (Tanzania) na wengi wengineo.
Kama kawaida, Tamasha huandaa mikutano na watu wajuzi mbali mbali na wasanii kwa mafunzo ya kiufundi kwa lengo la kuwawezesha watu kupata ujuzi kwa wapenzi wote wa muziki. Februari 16, kutakuwa na sherehe ya kumaliza tamasha zitakazofanyika Jambiani, muziki utakuwepo pamoja na ma DJ wa kimataifa kutumbuiza mpaka asubuhi.
Thursday, January 21, 2010
Wednesday, January 20, 2010
SALON YA MASTAA ZANZIBAR
Kwa wale watanashati wanaweza kwenda katika salon ya LAAZIZI HAIR CUTTING SALON iliyopo mitaa ya kwa mchina mwanzo hapa hapa kutoka visiwa vyetu vya marashi ya karafuu.
Usijiulize masuali mengi sana mtu mzima hiyo ni salon inayokwenda na wakati kutokana na huduma zake nzuri na mukidee.
Ukiingia tu unajihisi kama uko Mbele kwa mbele vile, kumbe ni hapa hapa Unguja baba ake mimi mwenyewe nilioshuhudia kwa macho yuangu wakubwa wa nchi na heshima zao wakipata huduma pale, watangazaji wa radio stations tofauti, watoto wa vigogo na hata akina sisi pia tunakaribishwa kwa sababu bei zao ni nafuu.
Kama huamini angalia picha hizo ambazo zinakuonesha jinsi wakubwa walivyobobea katika kazi yao na walivyomakini katika kuuendeleza usemi uleeeee wa mteja ni mfalme.
Wanaotoa Huduma ni Mkali Ayub , Mkali Stopaaa. Mkali Rama.. Uspiiiiiiiiiimee!! Oi
Saturday, January 16, 2010
ASHURA JUMA MAULID
Hellow Tz niajeeeeeeeeeeeeeee?!?!?!?!!!!????
Ashura bint wa Maulid hapaaa bt jus call me Csta Shouu coz I realy feel dis name.
Ni student wa ukwe-e from collage ya wajanja{DSJ}, nikiwa nakamilisha masomo ya Diploma.
Nafurahi kinyama kuwa miongoni mwa wanafunz wa dat collage coz I’hv got 2knw manythngs n manyp’po dat I ddn knw them b4.
Mzuka zaid ninapopata chance ya kuvsit sehem tofaut tofaut kwa ziara ya masomo na kukutana na wa2 muhim sana wa fani yangu.
Hebu icheki hii hapaaaaaaaaaaa
Ni ndani ya ZNZ ktk ki2o bora kabsa kinachorusha matangazo ya ukwe-e kijulikanacho as Saut ya pwani 96.8 Zenj Fm Radio.
Hapo chachaaa, dahh!!!! Ucpyme mkubwa ni ushirkiano wa kutosha toka kwa Tallented host wa dat Fm Radio.
Kuptia dis station nimepata kujuana as well as kuwaona host wakali from ZNZ island.
Mara ya kwanza naanza field ckufikiria kuwa itawadia tym ya machungu pndi nitakaposignout na kujawa na cmanz bt ‘n’way 2ko pa1 coz ni family ryt now.
Ni hayo 2 kwa sasa, mengi zaid endelea kuifungulia macho blog ya mkali wa The CRUSH Dj Siiiiiiideeeeeee.
My short message 2u
Live’s not always easy bt never gve up ur courage.
Often there’ll come a new began which’ll give u luck
I wish u all a gud tym in pc n luv , which’ll delight everyone.
Thanxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MREMBO HUYOO KWENYE POZI NA MTU MZIMA
Bi FATMA ISSA
MSANII WA TAARAB ASILIA MAKAME FAKI AKIWA TAABAN KWENYE BOTI YEYE NA KIKUNDI CHAKEE
KWA KERI PEMBA
Hapa tulikuwa kwenye Boti Kwa bahati nzuri tumekutana na Ustadh Rashid Ambae huwa anafanya vipindi vya dini Zenjifm. hapo akiwa siti moja na Aziza . Picha ya kati ni Meneger wa Zenjifm Hafidh kasim akiwa na Program Meneger wa Histfm Juma Ayub . Picha ya Juuu ni mimi mtu Mzima-- {Dj side} Pamoja na Juma Ayb aka P lava.
MPIGA DEBE MAARUFU BANDARINI PEMBA
Huyu ndie Bin Daud... Mpiga Debe maarufu Bandarini Pemba .. Hapa alikuwa ananiba kisomo Hajui kama kakutana na Mwalim wakee.. Kumwambia kama Mimi ni Dj sidee. daaaaa? kashangaa akaanza kunivangatiaaa. kelele mtindo mzimaaa. Dj sideeee Dj sideeeee eeeehhh. akachukua mzigo wangu wa Bov ya Microphone anataka nimtoeee... Daaa? Jamaa kaichaaa sanaa . Jamaa ni Noma. Wakati napiga nae stoty akaniambia yeye ni Mzanzibari Mzaliwa wa Chaani ... Huyu ndie Bin Daud
SOKO LA MKOANI PEMBA
Hapa tulikuwa sokoni Mkoani hii ilikuwa siku ya Pili baada ya kumaliza sherehe za mapinduzi ..Mkoani palifurika Wajeda.. au majeshi au ma mweraa... Kila mtu alikuwa bizeee kutafuta zawadi za kuwaletea ndugu zao Unguja....Sisi tulikuwa hapa kwa ajili ya kuchukua boti kurudi znz... Crew ya Zenjifm Ilikuwa hapo kwa ajili ya kununu halua na Tosi.. Kama Mnavomuona Mrembo hapo picha ya kati Mtangazaji wa Zenjifm Bi Aziza Wazir kheri akinunua Halua ya Pemba .
DUU? GARI LA FIRE LARUDISHWA ZNZ?
SAFARI YA KURUDI ZANZIBAR IMEWADIA
ASIKMWAMBIE MTU HALUA YA PEMBA TAMU
STUDIO YA ZENJIFM PEMBAA
Haya wadau wa blog hii.. Nilipata nafasi pia ya kutembelea sehem ambayo Zenjifm Inarusha matangazo yake huko Pemba. Hapa ni chake chake Gombani ambapo hata TVZ ilipo studio yao na sehem wanayorusha matangazo.. Huo ndio mnara ambao tumefunga antena zetu za kusukuma mawimbi ya sauti, Na hicho kijumba hapo ndimo mlimo mitambo ya Zenjifm .Kwa kweli Pemba Nzima Zenjifm inasikika vizuri sana
KIKUNDI CHA TAIFA CULTURE KIKITOA BURUDANI KATIKA UKUMBI WA GOMBANI USIKU WA SHEREHE ZA MAPINDUZI
HILI NDILO KABURI LA MAREHEM DR OMAR
Nilipata nafasi ya kutembele Jimbo la Wawi Pemba lengo hasa la kwenda Wawi ilikuwa Pia kudhuru Kaburi la Marehm Dr Omar Ally Juma ... Aliekuwa Makam wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania... Hili ndio kaburi lake. Kulikuwa na Tetesi Eti lilikuwa limedharauliwa eti lina msitu mkubwaaa hali ambayo nsio ya kweli. Mimi Binafsi nimefika na nimejionea Mwenyewe . Hiyo hapo juu ni picha likiwa linaonekana safi halina msitu .
SHEREHE ZA MAPINDUZI ZAPATA DOSARI
HAPA MHESHIMIWA RAIS AKIKAGUA GWARIDE KATIKA SHEREHE ZA MAPINDUZI HATA HIVYO KATIKA HALI ISYOKUWA YA KAWAIDA MTU MOJA AMEFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA KUTOKANA NA MSONGAMANO MKUBWA ULIOJITOKEZA MAPEMA ASUBUHI KATIKA UWANJA WA WAGOMBANI ALIYEFARIKI NI HUMUDI KATIBU MWENEZI WA KATA YA KIGAMBONI JIJINI DAR ES SAALAM ALIAALIKWA NA WAKAZI WA JIMBO LA MUYUNI KATIKA SHEREHE HIZO
SIKU YA MAPINDUZI ILIKUWA KA,MA HIVI HII NI SEHEM YA MAFUNDI
Wadau hapa ni uwanja wa Gombani Pembaaa, Na hapa ndipo sehem pa utangazaji na Ufundi. Mimi nikiwa kama Fundi Mkuu wa Zenjifm nilikuwa Gombani kwa ajili ya Kurusha Live Hapa ndio sehem tulipokuwa na mafundi . Kutoka STZ sauti ya Tanzania Zanzibar na Mafundi wa TTCL Kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawiaaa
HII NDO CHAI NILIOKUWA NIKINYWAA KILA SIKU WAKATI NILOPOKUA PEMBA
Friday, January 15, 2010
WATANGAZAJI WA ZENJIFM
Wadau hapa Tulikuwa tumekaribishwa Pemba mitaa ya Machomanee nyumbani kwa Mmoja wa wafanyakazi wetu wa Tawi la Pemba . Nyumbani kwa Bi Hadija .. Tulikaribishwa kwa kupikiwa Maembe mabivu Madodo ya nazi . chakula cha kipembaa .. Kulia ni Hafidh kasim meneger wa Zenjifm , Akifuatiwa na Aziza Wazi Kheri Msaidizi Program Meneger .Mimi nikiwa katikati (Dj sideeeeeeeee)..... Kushoto yangu ni Muandishi wa Hits Fm Bi Ajuzaa
Tuesday, January 12, 2010
HAWA NI WADAU WANGU WA PEMBAA
Wadau mambo vipi? Nilikuwa kimyaa kidodgo,Bado nipo Pemba kwenye sherehe za mapinduzi nilikuwa nimebanwaa sana kupita maaelezo ..Leo ndio tumemaliza mpango mzimaaa raha rahaa tuuu.. Hao hap juuu ni wadau wa kipindi cha The crush Pembaaa Maskani yao inaitwaa Wonderfull beber shop salon pande za macho manee . Tukiwa kwenye pozi la ukweli .Mimi nikiwa kati na Mchizi moja anaitwa Othman kondo, Dogo hamndu Dogo chande, Salum Henry..
Big up sana wadau wa Pemba pamoja sana
Friday, January 8, 2010
UMEME ZANZIBAR HADI FEBRUARY 20
Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja inatarajiwa kurejea tena baada ya siku 43 kuanzia leo kutokana na kuhitaji matengenezo yenye utaalamu wa hali ya juu.
Waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema matayarisho ya matengenezo hayo yameshakamilika na kinachosubiriwa ni vifaa vya kuchongesha kutoka Sweedena na Afrika ya Kusini vinavyotarajiwa kuwasili tarehe 20 mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema matengenezo hayo yatafanyika katika vituo vya kuchukulia na kupokelea umeme vya rasi Kiromoni Tanzania bara na Fumba kwa Unguja.
Waziri Mansour amesema umeme huo utaanza kuwashwa tarehe 20 mwezi ujao na majaribio yatafanyika tarehe 18 na 19 Akizungumzia uwezekano wa majenerata ya akiba, waziri Mansour amesema wizara inaendelea kufanya upembezi yakinifu ya ununuzi wa majanareta hayo.
Hata hivyo amesema serikali ya Norway imeonesha nia ya kukubali kugharamia ununuzi wa majenerata hayoHuduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja ilikatika tokea Desemba 10 mwaka jana na kusababisha usumbufu kwa wananchi ikiwemo uhaba wa maji safi na salama. Bonyeza hapa kumsikia waziri akizungumza na waandish wa habari (Waziri)
Thursday, January 7, 2010
HATIMAEE BIFUU LA AKHENATO NA JUMA 20 LAFIKIA PABAYA
Mkali wa june july Juma20 amesema kwamba ni ngumu kwake kuuelewesha umma kinachoendelea kati yake na crue ya Akhenaton kwa vile chanzo cha kutokuelewana kwao hata yeye hakifahamu vizuri.
Msanii huyo ambae kwa kiasi kikubwa amechangia kuaznishwa kwa familia hiyo ambayo baadae ilikuja kupata mafanikio ya kumiliki studio
Amesema kua anachokumbuka yeye ni kudai haki yake kwa mapromota wa redio Fulani ambao walimtangazia kwamba atakuwepo ktk show Fulani bila ya kukubaliana nae, nay eye kulifikisha suala hilo kwa uongozi wa Akhenaton ambao badala ya kumsaidia kimaamuzi walimchukulia kwamba yeye anahusika kwa namna Fulani kuandaa show hiyo na kituo hicho cha redio.
“nilijaribu kuwaeleza viongozi wa kundi kuhusu jambo hili lakini huenda walinielewa vibaya ama kulikua na namna ambayo mimi sio rahisi kuifahamu”
Msanii juma20 amesema kua kuna kasoro nyingi katika crue ya Akhenaton na hakukua na utaratibu wa kukaa chini na kuzisolve kwa pamoja, na ameeleza kwamba hiyo nayo ni sababu moja wapo iliyokua ikimvunja moyo wa kuendelea nayo.
“nilikua nampigia simu sana lillghetto kumfahamisha kinachoendelea, lakini alikua hapokei na wala hajibu msg zangu, siokuona sababu ya kumsumbua kwa vile nilihisi kwamba labda ule ndio mwisho wangu kuhitajika katika crue yetu au yao”
KWA BAHATI NZURI TULICHONGA NA JUMA KWENYE INTERVIEW YA KUUWAGA MWAKA NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYAA 2010
INTERVIEW ILIKUWA KAMA HIVI
Dj SIDE: Juma ?nini chanzo cha ugomvi?
JUMA20: Nasikia mtangazaji wa redio Fulani ndie alitetuchonganisha
Siwezi kumtaja kwa faida yake nay a wengine…
JUMA20: kusema la ukweli sioni kama nina taarifa yeyote kutoka ktk uongozi ndio maana nimeamua kufanya pirika zangu za muziki mwenyewe mwenyewe..
DJ SAM: umewahi kufukuzwa au kupewa barua yeyote?
JUMA20: anaekufukuza hakwambii toka, nilikua nampigia simu lill ghetto na akawa hapokei, mimi si mtoto mdogo kujua kwamba hana haja na mawasiliano na mimi
Dj SIDE: tunasikia una meneja mpya?
JUMA20: ndio, anaitwa seif mohd seif khatib na nashukuru ananisaidia sana ktk masuala ya kimuziki
Dj SAM: una mpango wa kurudi Akhenaton
JUMA20: hapana sifikirii kwa sabau tayari yenyewe haina mpango na mimi
Hayaa wadau .Zengweee jipyaaa limeanza mwaka mpyaaa Jana nilipokea simu ya Muda criss anataka kufanya kipindi na mimi ili nae aelezee chanzo cha ugomvi huo. Nimemwambia Nitampatia kipindi . So wadau endeleeni kuganda na Zenjfm sooon mtamsikia Muda nae akinguruma kwenye show live.
BINAADAM ANALIWA KAMA MBUZI?
Kwakweli hata lakuandika sijui.. Maana haya ninayo yaona hapa sijapata kuyaona tokea nazalia . Naona ni maajabu tu... Yaani binaadam analiwa kama mnyama? Nimesika wachina wanakula Nyokaaa, Mbwaaa, vyuraaaa majongooo. konokono lakini hii kali. Huyu ni babu alie kimbia njaa africa akenda kwenye kisiwa kimoja huko china . Hatimae haya ndio yaliomkutaaa. Amechinjwaaa kama kuku watu wakagawana nyamaa. Ilikuwa ni mwituni baadae wakapika ubwabwaa wakalaa.
Lakini jamanii huu si unyanyasaji? Inafaaa kuungana kupiga vita unyanyasaji na vitendo vya kinyama kama hivi. Hawa watu ni waaajabu kweli .
Subscribe to:
Posts (Atom)