Wednesday, January 27, 2010
LILIAN AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA FACE OF AFRICA
Hatimaye Tanzania ilipata mwakilishi wake katika fainali za mashindano ya Kisura wa Afrika yanayotarajiwa kufanyika February 6 mwaka huu.
Meneja wa uhusiano wa Multichoice Furaha Samalu alisema kwamba Lilian amefanikiwa kupita hatua ya kumi (10) bora baada ya kupita mchujo wa washiriki wengine 24 kutoka nchi mbali mbali.
Kabla ya kupatikana kwa washiriki kumi warembo hao walikuwa kambini nchini Kenya katika mji wa Mombasa katika kambi maalumu.
Lilian anatarajiwa kuondoka tarehe 26 kuelekea Afrika Kusini tayari kwa fainali hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Nigeria katika mji wa Lagos.
Zaidi ya hayo mbunifu wa kitanzania anayeishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini Anisa Mpungwe amepata nafasi ya kuwaandalia mavazi baadhi ya washiriki watakaoshiriki kwenye fainali hizo.
Lilian ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es salaam amewaahidi watanzania kufanya makubwa na kufwata nyao za dada yake Miriam Odemba kama ilivyokuwa mwaka 1999.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment