Monday, January 4, 2010

MAPACHA WALIO UNGANA WAZALIWA ZANZIBAR




WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA WALIOZALIWA NA FARHAT MAULID KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA HATIMAE WAMEFARIKI DUNIA JANUARI 2, 2010 ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA.
WATOTO HAO AMBAO WAMEISHI KWA SIKU MOJA TANGU KUZALIWA WALIHIFADHIWA KATIKA CHOMBO MAALUM CHA KUSAIDIA JOTO PAMOJA NA KUSAIDIWA KUPUMUA
KWA MUJIBU WA DAKTARI, WATOTO HAO WAMEFARIKI DUNIA SAA 12 ASUBUHI JUZI TAREHE 2 IKIWA NI BAADA YA KUISHI KWA MASAA 11 BAADA YA KUZALIWA KWAO.
MAMA MZAZI WA MAREHEMU HAO FARHAT MAULID (18) MKAAZI WA MWANYANYA WILAYA YA MAGHARIBI KATIKA KISIWA CHA UNGUJA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA.
WATOTO HAO WALIKUWA WAMEUNGANA SEHEMU ZA KIFUA NA TUMBONI WAKIWA NA UZITO WA KARIBU KILO 3, AMBAO WAMEZALIWA SAA 3.30 ZA ASUBUHI YA JUZI MKESHA WA MWAKA MPYA JUZI KWA NJIA YAUPASUAJI LIKIWA NI TUKIO LA KWANZA KUTOKEA KATIKA VISIWA VYA ZANZIBAR.
PAMOJA NA KUUNGANA HUKO KWA PAMOJA WALIKUWA WAKITUMIA KITOVU NA MOYO MMOJA, NA BAADHI YA VIUNGO VYENGINE VILIVYOBAKIA KILA MMOJA ALIKUWA NA VYAKE.
MAMA MZAZI ILIBIDI AJIFUNGUE KWA NJIA YA UPASUAJI KUFUATIA KUFIKISHWA HOSPITALINI HAPO AKIWA ANASUMBULIWA NA UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA ILIYOKUWA TAYARI IMESHATIMIA MIEZI TISA.
HII NI MARA YA KWANZA KATIKA VISIWA VYA ZANZIBAR KUZALIWA MAPACHA WALIOUNGANA

No comments: