Wednesday, January 27, 2010
UCHAWI NI WAIKUMBA ZENJI FLAVA
Hivi kwa nini mwanadamu hawezi kufanya mambo yake kwa kujiamini hadi atumia vitu vya ajabu na kutoa shutma zisizokuwa na msingi katika maisha yake?Nauliza suali hili kutokana na kile kinachoendelea hivi sasa katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya kwa upande wa Zanzibar almaarufu Zenji flava.
Kipaji ni kipaji tu kama kipo hakiwezi kuondolewa na mwanadamu isipokuwa kwa nguvu za muweza.
Hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya makundi ya muziki wa Zenj flava yakisambaratika na mengine kugombana na kuhasimiana kwa sababu zisizokuwa na msingi.
Miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na kundi la Offside Trick,kundi ambalo ni miongoni mwa makundi na wasanii waliochangia kusimamisha a muziki wa Zabnzibar kwa asilimia kubwa.Tulishuhudia baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo wakigombana na kushutumiana kwa mambo yasiyokuwa na msingi kwani endapo kama wahusika wangeyasulihisha wenyewe yote yasingetokea
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na isiyotegemewa na wengi mmiliki wa studio ya Teddy Records, Ahmed almaarufu Tguay ameibuka na kudai kuwa hana mafahamiano mazuri na Berry Black aka mfalme wa Zanzibar
Bifu la Berry Black na Tguay linaonekana kupamba moto baada ya madai kuwa msanii huyo aliyetamba na vibao vyake vingi vya kimapenzi kuwa amempa udaku producer wa kuaminika na kutegemewa wa Tguay katika studio yake ya Teddy Records mjanja kutoka kule nchini Kenya Shirko.
Habari za kuaminika zinasema kuwa kwa sasa Berry Balck ameshahama katika nyumba aliyokuwa akiishi ambayo ni nyumba ya kina Teddy na kwa sasa anaishi kimpango wake Kwa Upande wa Shirko inadaiwa kuwa yeye na Teddy kwasasa hakuna stori zaidi ya salam.. Na kwa mujibu wa Shirko Anasema yumo mbioni kufungua studio yake hapahapa ZNZ
Jee nani mkweli?? Tutafika wapi endapo watu wanaanza kubweteka kwa kupata mafanikio kidogo tu?? Na ni kwanini wasanii wasiwe kitu kimoja il.i kuliendeleza gurudumu kla muziki huu ambao unaonekana kuwagusa wengi hasa vijana ambao wengi miongoni mwao ndio ajira yao ya kudumu?
Tafakari, tafuta jibu na toa maoni yako juu ya hili….tchao beibiiiiiiiiiiii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment