Thursday, January 7, 2010

HATIMAEE BIFUU LA AKHENATO NA JUMA 20 LAFIKIA PABAYA


Mkali wa june july Juma20 amesema kwamba ni ngumu kwake kuuelewesha umma kinachoendelea kati yake na crue ya Akhenaton kwa vile chanzo cha kutokuelewana kwao hata yeye hakifahamu vizuri.

Msanii huyo ambae kwa kiasi kikubwa amechangia kuaznishwa kwa familia hiyo ambayo baadae ilikuja kupata mafanikio ya kumiliki studio
Amesema kua anachokumbuka yeye ni kudai haki yake kwa mapromota wa redio Fulani ambao walimtangazia kwamba atakuwepo ktk show Fulani bila ya kukubaliana nae, nay eye kulifikisha suala hilo kwa uongozi wa Akhenaton ambao badala ya kumsaidia kimaamuzi walimchukulia kwamba yeye anahusika kwa namna Fulani kuandaa show hiyo na kituo hicho cha redio.

“nilijaribu kuwaeleza viongozi wa kundi kuhusu jambo hili lakini huenda walinielewa vibaya ama kulikua na namna ambayo mimi sio rahisi kuifahamu”
Msanii juma20 amesema kua kuna kasoro nyingi katika crue ya Akhenaton na hakukua na utaratibu wa kukaa chini na kuzisolve kwa pamoja, na ameeleza kwamba hiyo nayo ni sababu moja wapo iliyokua ikimvunja moyo wa kuendelea nayo.

“nilikua nampigia simu sana lillghetto kumfahamisha kinachoendelea, lakini alikua hapokei na wala hajibu msg zangu, siokuona sababu ya kumsumbua kwa vile nilihisi kwamba labda ule ndio mwisho wangu kuhitajika katika crue yetu au yao”

KWA BAHATI NZURI TULICHONGA NA JUMA KWENYE INTERVIEW YA KUUWAGA MWAKA NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYAA 2010

INTERVIEW ILIKUWA KAMA HIVI

Dj SIDE: Juma ?nini chanzo cha ugomvi?

JUMA20: Nasikia mtangazaji wa redio Fulani ndie alitetuchonganisha
Siwezi kumtaja kwa faida yake nay a wengine…

JUMA20: kusema la ukweli sioni kama nina taarifa yeyote kutoka ktk uongozi ndio maana nimeamua kufanya pirika zangu za muziki mwenyewe mwenyewe..

DJ SAM: umewahi kufukuzwa au kupewa barua yeyote?

JUMA20: anaekufukuza hakwambii toka, nilikua nampigia simu lill ghetto na akawa hapokei, mimi si mtoto mdogo kujua kwamba hana haja na mawasiliano na mimi

Dj SIDE: tunasikia una meneja mpya?

JUMA20: ndio, anaitwa seif mohd seif khatib na nashukuru ananisaidia sana ktk masuala ya kimuziki

Dj SAM: una mpango wa kurudi Akhenaton

JUMA20: hapana sifikirii kwa sabau tayari yenyewe haina mpango na mimi

Hayaa wadau .Zengweee jipyaaa limeanza mwaka mpyaaa Jana nilipokea simu ya Muda criss anataka kufanya kipindi na mimi ili nae aelezee chanzo cha ugomvi huo. Nimemwambia Nitampatia kipindi . So wadau endeleeni kuganda na Zenjfm sooon mtamsikia Muda nae akinguruma kwenye show live.

No comments: