Wednesday, January 27, 2010

AFANDE SELE CHID BENZI NDIE MSANII ALIE JUUU KWA SASA


Selemani Msindi a.k.a Afande Sele toka kundi la Watu Pori pande za Motown au Morogoro ameibuka tena lakini safari hii akiongelea anayeamini kuwa ni mtu pekee kwasasa kumvua taji lake la Mfalme wa Ryhmes.

Akichonganasi Afande amesema ya kuwa anaamini kabisa kama kuna msanii wa Bongo fleva anayeweza kumvua taji lake basi ni Chid Benz toka kundi la LA Familia pande zile za Ilala

“Chid ni mkali wa mashairi, ana ryhmes, pia hata kuliburudisha jukwaa anaweza, mimi kwangu Chid ndio yupo juu kwasasa aisee, naweza kusema ndiye pekee anayeweza kuchukuwa taji la Mfalme wa Rhymes kwasasa.” alisema Afande Sele.

Afande Sele ndiye anayeshikilia taji hilo baada ya kufanyika mara moja tu miaka ya nyuma na kukutwa na misukosuko mingi.

No comments: