Friday, May 28, 2010
MOVIE YA THING FALL APART ITAMTOA ROHO 50 CENT
Daa jamaa huwenda akatoka roho .Unajua jama anasema alikuwa na mchizi wake alikuwa anaumwa na cancer ndio jamaa akampa mzuka na kuandika script ya movie iitwayo Things fall apart . Sasa hapa 50 emefanya diet ya nguvu ili akonde awe kama ana cancer ili akichukuwa shoot ya movie yake bc iwe ya ukweli.... Daa? hivi wewe unaweza kweli hali hii?
halafu jamaa si kama maskini bc tu.. hmm kaz kweli kweli . Gonga hapa usome mpagngo mzima.
AY ATINGA KWNYE MUSEKE AWARDS
Chaguo la Teenz na Kili Awards tumekamata n' I believe niko na support kubwa nyuma yangu that's y tunashinda. Now ni tym ya Museke Awards. u can vote kwenye website yao for free na mara nyingi utavyoweza ili AY ashinde.
Niko kwa 5 Categories:
Artist of the year / Best Male / Best Collaboration (feat. Avril n' Wahu) / East African Song (Leo; original version) / Hip Hop Song (Leo:Original version).
ingia www.awards.museke.com kisha vote kwa AY.. Awards zitafanyika tarehe 1 June
ONE!
Thursday, May 27, 2010
A BOYS NEW VIDEO - USIBADILIKE FT CHEGE
Hawa ni vijana kutoka Zanzibar wanaitwa A boys . A boys ni kundi linaloundwa na watu wa wili Jackob B na Bad sky.. kikiwa na maskani yake mtaa wa kibweni zanzibar ... Sasa wametoa vide ya ngoma yao mpyaa iitwayo Usibadilike ft chege.
FULL MOON PARTY ONCE AGAIN
FULL MOON PARTY EVER!! THE SPEAKER WIL BE SMOKING. STARTING AT 2pm...DJ SIDE FROM ZENJIFM WIL BE ENTERTAINING U AT THE DECK. LADYS AND GENT' ARE U READY FOR ACROBAT SHOW AND FIRE EATER? SPACIAL BUFFE BEACH EDGE..DRINKS AND ICE CREAM WIL BE AVAILABLE. GET READY FOR FULL MOON PARTY EVER!! MEET US AT KENDWA ROCK THIS SATURDAY FLAVA DJS INA HOUSE!
Sunday, May 23, 2010
JUNE JULY VIDEO JUMA 20 NEW VIDEO
Juma 20 hatimae ameachia video ya ngoma yake iitwayo June July ..Video hii imetengenezwa pale Jupiter Record .Amstrong Dad ndie alie itengeneza ... Nilikuwa naongea na Juma wakati ananipa habari juu ya hii video yake mpyaa . alinitumia sms na tukawa tunachart Juma 20 alianza kwa kunitumia sms isemayo
Juma 20 ... Najua Dj side hautonijibu but angalia video yangu ya JUNE JULLY katika Wall ya facebook yangu, comment then nambie lini niilete uirushe kwenye blog?
Mimi nilimjibu ok bt nilimuuliza whats yr target ya kutoa video ya june jully nw?
Juma 20 alijibu kwa kusema
Target yangu ni kuzidi kujitambuslisha katika anga za kimataifa ,kupata show ,pia kujinadi katika tuzo za ZANZIBAR MUSIC AWARDS .. Wimbo wangu mpya unaitwa KIBAJAJI utafuata.
Niliendelea kumuuliza masuali juma 20 suala lilifuata lilikuwa kama ifuatavyo-
2009 mwezi wa june umeachia wimbo wa june jully ..Mwaka 2010 karibu na june jully umeachia video yake Jee? 2011 mashabiki wako watarajie movie ya june yully au sires?
Juma alijibu kwa kusema -
Hii inaoneha jinsi gani nisivyo na papara na kazi zangu zinaenda na wakati nimefunga ukurasa wa june jully nadhan hakuna wimbo kama huu duniani.
Mimi nikamwambia sijaridhika na jibu jeee? mwakani kuna movie ya june jully?
Juma alinijibu kwa kusema
Mbona nilishakupa jibu kwamba kama ni kitabu basi chapter ya june july imeipita labda November December tena but sitaongelea au kuigiza tena kuhusu tittle hiyo
Nilienedlea kumuuliza Juma 20 na suala lililofuta ninikuwa kama ifuatavyo
Sauti yako imetumika sana katika wimbo wa umoja wa zaznibar ..Hivi una mpango wowote wa kutumia picha yako katika kampeni ya chama tawala cha ccm katika kampeni ya uchaguzi Ili kuhamasisha chama tawala kiendelee kukaa tena madarakani ?
Juma alijibu kwa kusema
Actual mimi si mwana siasa , ni mwanamuziki, na mfano wa kuigwa kimavazi, mitindo ya ndevu na style za nywele , nina nafasi kubwa ya kutambulika kimwili(personalty) kuliko mtu ambae inatakiwa kusikika sauti yake tu pasipokua na haja kuonekana sana
Suala la mwisho kumuuliza Juma 20 ilikuwa gumu sana kwake kwani alichukuwa takriban dakika 5 hadi kinijibu. suala lilikuwa kama ifutavyo
Ricky martin hatimae juzi juzi amekiri kama yeye ni Homosexual baada ya kuficha kwa mda mrefu. Unalizungumzia vipi suala hili kiupande wako ili kuwatoa hofu mashabiki wako kwani kumekuwa na uvumi mkubwa kutoka kwa mapaparazzi kuwa unapenda kujichanganya na watu wa aina hiyo??
Baada ya nukta kazaa za ukimyaan Juma alijibu kwa kusema
Mimi ni rais katika dunia yangu ya mziki Gender si suala ninaloliangalia sana linapokuja suala la marafiki, viongozi , mashoga, mapaparazi, watanagazaji mashoga. Nitajuaje nani yumo nimtenge nani hayumo awe rafiki yangu its ridiculous
Sikuridhika na jibu lake lakini any way nitaendelea kumdig mpaka anianikie aweke mambo hadharani. Kwani hapo juu ameonekana kujitetea kimtindo but hakujibu suali sauli langu.
Ni hayo tu
Angalia video sasa . comments muhim
Friday, May 21, 2010
HATIMAE WASHIRKI WA ZANZIBAR MUSIC AWARDS WATANGAZAWA
HAWA NDIO WASHIRIKI WALIOFANIKIWA KUINGIA KWENYE TUZO ZA ZANZIBAR MUSIC AWARDS 2010.
ILI KUMPIGIA HURA MSHIRIKI TUMA NAMBA YA MSHIRIKII KWENDA KWENYE NAMBA 0655 968 968
5TH ZANZIBAR MUSIC AWARDS 2010
I MUIMBAJI BORA WA MWAKA
01 : BABY J – NITEMBEE MBELE
02 : MTUMWA MBAROUK – UNANITAFUTA UNDANI
03 : RICO SINGLE – WACHA WAONGEE
04 : MAKAME FAKI – VYA KALE NI DHAHABU
II MUIMBAJI BORA WA MWAKA WA KIUME MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
05 : MANYOTA – UNANITESA
06 : BERRY WHITE – MAMBO VIPI
07 : T GUWAY – MAUMIVU YA PENZI
08 : JUMA 20 – JUNE JULY
09 : RICO SINGLE – WACHA WAONGEE
III WIMBO BORA WA MWAKA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
10 : MAMBO VIPI – BERRY WHITE
11 : JUNE JULY – JUMA 20
12 : TAMBUA – I T
13 : WACHA WAONGEE – RICO SINGLE
14 : CHAGUO LANGU – DORICA
IV WIMBO BORA WA MASHIRIKIANO MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
15 : NITEMBEE MBELE – BABY J
16 : HAWANA NENO – DIDA
17 : JUNE JULY – JUMA 20
18 : COLLABO – SHORTGUN
V WIMBO BORA WA MWAKA TAARAB YA KISASA
19 : HATUPUMUI - FATMA HASSAN ( SPICE MODERN )
20 : ONCE MORE – ZUHURA SHAABANI (ZANZIBAR ONE)
21 : TUNAPENDANA KWA SANA – TAHIR KHAMIS ( SAFINA MODERN)
22 : NIDHIBITI - SAADA NA SSOR ( ZANZIBAR ONE)
VI MTUNZI BORA WA MWAKA
23 : MOHAMMED S. NASSOR – HATUPUMUI
24 : SAID BAKAR – WEMA WANGU MTIHANI
25 : MANYOTA – UNANITESA
26 : ALHAJI GOYA – MWANAJESHI HALISI
VII MTAARISHAJI BORA MUZIKI WA MWAKA
27 : AYOUB BEBE – MAUMIVU YA PENZI
28 : AROON NAME – WACHA WAONGEE
VIII MWANAMUZIKI BORA WA MWAKA
29 : NASSOR AMOUR
30 : I T
31` : POZI ADIMU
IX MUIMBAJI BORA CHIPUKIZI
32 : DIDA – ACHANA NAO
33 : DOGO FANI – KISA CHA MAMA
34 : SULTAN BAKAR – SARAFINA
X ALBUM BORA YA MWAKA
35 : HATUPUMUI – SPICE MODERN
36 : KAMA NI RAHISI – ZANZIBAR ONE
37 : TUNAPENDANA KWA RAHA ZETU - SAFINA MODERN
XI MUIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB ASILIA
38 : IDDI SUWEID – NINAE
39 : MOHAMMED ILYAS - NIMESAFI MOYO
40 : MAKAME FAKI – VYA KALE DHAHABU
XII MUIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB ASILIA
41 : FAUZIA ABDALLA – LISHALO
42 : MTUMWA MBAROUK – WANITAFUTA UNDANI
43 : FATMA ISSA – HAYA MAUMBILE YANGU
XIII MUIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB YA KISASA
44 : ZUHURA SHAABAN – ONCE MORE
45 : FATMA HASSAN – HATUPUMUI
46 : SAADA NASSOR - NIDHIBITI
47 : RUKIA RAMADHAN – DAM DAM
XIV MUIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB YA KISASA
48 : HAFIDH ABDUL SALAAM
49 : IBRAHIM KHAMIS – ONE CHANCE
50 : TAHIR KHAMIS – TUNAPENDANA KWA RAHA ZETU
`XV : MUIMBAJI BORA WA KIKE MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
51 : BABY J – NITEMBEE MBELE
52 : DORIKA – HAWANA NENO
53 : DIDA - ACHANA NAO
XVI : KIKUNDI BORA CHA MWAKA NGOMA ASILIA
54 : CHEKA NAO – JANG`OMBE
55 : IMANI NGOMA – KARIAKOO
56 : SANAA – KARIAKOO
57 : SHIRIKISHI – MAGOMENI
NAMBARI ITAKAYO TUMIKA KWA AJILI YA KUPIGA KURA KWA WASHIRIKI NI 0655 968 968 NA MWISHO WA KURA NI 23/06/2010
ZANZIBAR MUSIC AWARDS 2010 IMEWADIA
Manager wa Zenji Entertainment Ndugu Seif Mhmed Seif akizungumza na waandishi wa habari .Katik ukumbi wa habari maelezo. Hapa ilikuwa anataja majina ya washiriki walifanikiwa kuingia kwenye kinyanganyiro cha Tuzo .
HABARI KWA WAANDISHI WA HABARI
Asalamu alleykum ndugu zangu waandishi wa habari
Awali ya yote kwanza na mshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uhai na uzima kwa kukutana leo hapa, pili nikushukuruni nyinyi wandishi wa habari kwa kuacha majukumu yenu mengine kwa kuitika wito wetu huu na kuwa nasi katika mkutano wetu huu.
Pia napenda kuwashukuru wenyeji wetu wa mkutano huu idara ya habari maelezo Zanziar kwa kutupatia sehemu hii ya kufanyia mkutano wetu huu.
Ndugu zangu waandishi wa habari Lengo la kukutana kwetu ni kuelezea matayarisho ya tamasha la tano linalofanyika kila mwaka Zanzibar la utowaji wa tunzo za wasanii bora wa mwaka Zanzibar kwa mwaka 2010 ili nanyi taarifa hizi muzifikishe kwa wananchi kupitia vyombo vyenu tofauti.
Ndugu zangu wandishi wa habari tamasha la utowaji wa tunzo ya mwanamuziki bora Zanzibar zinatarajiwa kutolewa tarehe 26 June mwaka huu katika ukumbi wa Salama Hall wa hoteli ya Bwawani ambapo tamasha hili linatarajiwa kuwa la aina yake ikilinganishwa na matamasha mengine manne tulioandaa miaka iliyopita.
Tamasha hili linaandaliwa na kampuni ya habari Zanzibar Zanzibar Media Coperation kupitia kitengo chake cha Zanzibar Entertainment kwa lengo la kuinua vipaji vya wasaanii wetu wa Zanzibar na kuvienzi kwa kazi kubwa wanazozifanya ili waweze kuleta ushindani katika soko la kazi zao za sanaa na hatimae kufaidika kimapato na kazi zao hizo.Pia ni chachu ya kuwainua wasanii wetu
Ndugu zangu waandishi wa habari tuelewe kwamba Zanzibar imo katika mipango ya kuingia katika soko la pamoja la nchi wanachama wa Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki hivyo fani ya sanaa inaweza kuwa sekta muhimu kwa nchi wanancha kama ni sehemu kubwa ya ajira kwa raia wa nchi hizo. Hivyo kuwepo na matamasha kama haya kutawasaidia wasanii wa Zanzibar kukuza na kuibua vipaji vyao ili waweze kuleta ushindani katika soko hilo na masoko mengine ya kimataifa na pia kuitangaza Zanzibar katika medali za sanaa na ubunifu.
Ndugu zangu waandishi wa habari pia tamasha letu la utowaji wa Tuzo za wanamuziki bora wa Zanzibar linaweza kuisaidia nchi yetu kuitangaza sekta ya utalii Zanzibar na hatimae kuingiza watalii wengi ambao wanasaidia kukuza pato la taifa. Hili linawezekana kwani vyombo vyenu na vyombo vingine vya kimataifa hurusha hewani matangazo ya tamasha letu katika nchi nyingi duniani ambayo yataonyesha mitindo ya wanamuziki wetu.
Ndugu zangu wandishi wa habari tamasha la utowaji wa tunzo mwaka huu litahusisha utowaji wa tunzo katika sanaa zaidi ya kumi na sita hii ikiwa pungufu kidogo ukilinganisha nay a mwaka jana lengo ni kuboresha tamasha hili pekee ndani ya visiwa vya Zanzibar . Tunzo zitakazogombania ni kutoka fani taarab ya kisasa,taarab asilia,muziki wa kizazi kipya,ngoma asilia pia album bora.
Washiriki wa tunzo hizo wataanza kupigiwa kura kuanzia kesho tarehe 22 hadi tarehe 23 mwezi ujao mwaka huu ikiwa ni matokeo ya mchujo wa awali uliofanya na magwiji wa fani za muziki . Jinsi ya kuyapigia kura majina ya washiriki na kazi zitakazopigiwa kura ni kila mshiriki amepewa no maalum kwa ajili ya kupigiwa kura kwa kila kipengele hivyo unachotakiwa kwa mwananchi kuandikia nambari alionayo msanii kisha kutuma kwenda 0655 968 968 .
Matangazo na jinsi ya kupiga kura utasikia kupitia redio mbali mbali na pia utaweza kupiga kura kupitia kuponi ndani ya gazeti la kila wiki la nipe habari.
Ndugu zangu waandishi wa habari tamasha hilo pamoja na utowaji wa tunzo linatarajiwa kugharimu zaidi shilingi milioni 24 za Kitanzania fedha ambazo zinatokana na michango ya wafadhili wetu wa ndani.Hata hivyo milango la wafadhili bado iko wazi tunawakaribisha .
Kabla ya kumaliza hutuba yangu naomba niwashukuru tena ndugu zangu waandishi wa habari kwa kunisikiliza kwa makini na naomba kutoa fursa ya kuuliza masuala pale panapohitajika ufufanuzi zaidi
Baada ya maelezo haya nitaruhusu zitolewe nakala za mchako wa wasanii walipita katika kila kipengele .
Ahsanteni kwa kunisikiliza .
SEIF MOHAMMED SEIF
MENEJA
ZENJI INTERTAINMENT
zenjientertainment@yahoo.com
Thursday, May 20, 2010
COSOZA YAFANYA OPERESHENI KALI KATIKA MADUKA YA CASET ZNZ
Afisi ya haki miliki leo imefanya uperesheni maalum katika maduka yanayokodisha na kuuza Keseti ambayo hayajafanyiwa malipo kwa ajili ya kuendesha biashara ya sanaa katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Zanzibar.
Akizungumza katika Oparesheni hiyo msimamizi na mtendaji mkuu wa afisi hiyo Mtumwa Khatib Khamis amesema lengo la Oparesheni hiyo ni ni kuhakikisha haki za wasanii na wabunifu zinapatikana na kuwashajihisha wafanya bishara kuzitumia kazi za sanaa kihalali.
Amesema biashara ya sanaa imekuwa ikiwanufaisha wafanyabiashara pekee lakini wabunifu asili hawafaidiki vyema na kazi zao.
Msimamizi huyo amesema afisi yake imetoa elimu kwa wananchi na wafanya biashara wa kazi za sanaa kwa muda wa miaka mitatu sasa ili kujisajili na kufanya malipo lakini baadhi ya wafanyabishara hao wameonekana kudharau juu ya hatua hiyo…
Oparesheni hiyo imefanyika katika maeneo ya Amani,Mpendae,Amani Fresh,Melinne ,meli tano ,kwa alinatuu na mali zilizokamatwa zinatarajiwa kuaangamizwa na afisi hiyo.
Jumla ya wafanyabiashara wa madula ya keseti 65 wamejisajili katika afisi hiyo kati ya hao wafanyabishara watano tuu ndio waliolipa kazi za sana hiyo.Opereresheni hiyo itakuwa endelevu ilikuhakikishwa wasanii wananufaika na akazi zao. Maduka kazaa yamekamatwaa ....
Tuesday, May 18, 2010
CHID BENZ MIKONONI MWA POLISI LEO
Msanii bora wa hip hop wa tuzo za Kili Music Awards 2010,Chid Benz mapema leo mchana emetiwa mIkononi na polisi maeneo ya Kilwa Road mara baada ya kudaiwa kuingilia msafara wa kiongozi mmoja aliyekuwa akipita eneo hilo, Polisi wa usalama barabarani wakamtia Chid Benz mokononi huku wakimhoji ni kwa nini ameingilia msafara, Kwa mujibu wa shuhuda Chid Benz amedai kutukanwa tusi zito na mmoja wa polisi wa usalama barabarani ndio kukaibuka patashika hilo ,kufuatia vute nikuvute hiyo Chid Benz akaamua kwenda kutoa taarifa ya kutukanwa kwenye kituo cha Kilwa road. Haya wadau. Kazi hiyo. Maana polisi anasema chid kaingillia msafara wa mkubwa wa nchi. Na Chid nae anasema katukanwa tusi kubwaa.. Mambo yatakuwaje hapa...? Sisi letu jicho tu tusubiri sheria ichukue mkono wake.
Sunday, May 16, 2010
DAIMOND AFUNIKA TUZO ZA KILI 2010
Daimond mwaka huu amchukuwa tuzo 3 kwa Mpigo. Tuzo ya Wimbo bora wa R&B na Msanii Bora chipukizi wa mwakaa. na Wimbo Bora wa Mwaka. (Kamwambie)
The Kilimanjaro Music Awards” pamoja na “Malaria No More” mwaka huu, watampeleka Senegal Msanii chipukizi Diamond kwenda kujionea na kujifunza shughuli azifanyazo mwanamuziki maarufu Youssou N’dou nchini humo katika kupambana na malaria,na namna gani wanatakiwa kujikinga na malaria na pia kwa namna gani wanaweza kupata matibabu pindi wanapokuwa wamepatwa na malaria
Daimond ambaye ndiye Msanii chipukizi atapata nafasi ya kuungana pamoja na Mabalozi wa Malaria No More Lady JD, Marlaw, Mwasiti, Bi Kidude, Banana na Prof Jay wakiwa kama mabalozi kuweza kusambaza ujumbe kwa jamii kwa nini jamii inatakiwa kujikinga dhidi ya malaria,
TUZO ZILIKUWA KAMA HIVI
Mwimbaji bora wa kike
Lady Jaydee
Mwimbani bora wa kiume
Banana Zoro
Albamu bora ya taarab
Daktari wa Mapenzi -Jahazi Mordern taarab
Wimbo Bora wa Taarab
Daktari wa Mapenzi – Jahazi Morden taarab
Wimbo bora wa Kiswahili
Mwana Dar es Salaam – African Stars Band
Albam bora ya Bendi
Mwana Dar es Salaam - African Stars Band
Wimbo bora wa R&B
Kamwambie -Diamond
Wimbo bora asili ya kitanzania
Nikipata nauli - Mrisho Mpoto
Wimbo bora wa Hip Hop
Stimu zimelipiwa - Joh Makini
Wimbo bora wa Reggae
Leo (Reggae remix) -AY
Wimbo bora wa Raga
Bwana misosi - Mungu yuko Bize
Rappa bora aw mwaka (Bendi)
Chokoraa
Msanii bora wa Hip-Hop
Chid Benzi
Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Haturudi nyumba - Kidumu FT. Juliana
Mtunzi bora wa nyimbo
Mzee Yusuf
Mtayarishaji bora wa nyimbo
Lamar
Video bora ya muziki ya mwaka
C Pwaa – Problem
Wimbo bora wa Afro Pop
Pii pii (Missing my baby)
Msanii bora anayechipukia
Diamond
Wimbo bora wa kushirikiana
Nipigie -AT-Stara Thomas
Wimbo bora wa Mwaka
Kamwambie -Diamond
WALK OF FAME
1. ZAHIR ZORRO
2. CLOUDS FM
A T ACHUKUWA TUZO KWENYE KILI AWARDS
Kijana kutoka Zanzibar A T . hapa akikabidhiwa tuzo na Mwanamuziki mkongwe wa Reggae Ras Inno Nganyagwa . Tuzo hii ilikuwa ya Wimbo bora wa kushirikiana . AT ameshirikiana vizuri sana na Mwana dada Stara Thomas katika wimbo wa Nipigie... A T ni msanii kutoka zanzibar katika katagori hii alikuwa akishindana na Mangwea na Fid Q (CNN),
Barnaba na Pipi (Njia Panda),
Mwana FA na Profesa Jay na Sugu (Nazeeka Sasa),
Hussein Machozi na Joh Makini (Utaipenda).
LAMAR NDIE PRODUCER BORA WA MWAKA
MR MISOSI HUU NI MWAKA WAKE
Mr misosi hii itakuwa ni mara ya kwanza kushiriki kwenye tuzo hizi na hatiame amefanikiwa kuchukuwa Tuzo ya Wimbo bora wa Ragga . Hapa Mr misosi akikabidhiwa na Sean kingston Tuzo ya wimbo bora wa Ragga. Mr misosi alikuwa akichuana vikali na
Dully Sykes (Shikide),
Bwana Misosi (Mungu yupo bize),
Drezzy Chief (Wasanii),
Benjamin wa mambo jambo (Fly).
HATIMAE CHID BENZ AUVAA UFALME WA HIPHOP TZ
OFSIDE TRICK WAKIWAKILISHA KWENYE TUZO
Thursday, May 13, 2010
CLUB BILICANAS YANUSURIKA KUUNGUA USIKU YA JANA
Club maarufu na yakimataifa hapa nchini,Club Bilicanas imenusurika kuungua moto usiku huu mara baada ya moja ya TV zilizowekwa ndani ya clab hiyo kuleta shoti na mpaka kulipuka kabisa,kitu ambacho kilimpelekea kila mmoja aliekuwepo ndani humo kudhania ni bomu na kuanza kukimbia kutoka nje na kwa kuulinda uhai wake.lakini kwa bahati nziri wafanyakazi wa jengo hilo walifanikiwa kuwahi kuudhibiti moto huo.Bendi ya Twanga Pepeta ndio iliyokuwa ikitumuiza hapa siku ya leo katika ambapo kila siku za jumatano bendi hiyo hupiga katika kiota hicho.
Gari la faya likiwa limesimama nje ya jengo la club bilicanas kuangalia kama kuna lolote ili kazi yake ianze mara moja.lakini kwa bahati nzuri moto huo uliweza kudhibitiwa na wafanyakazi wa club hiyo. Picha na habari ni kwa mujibu wa http://issamichuzi.blogspot.com/
SEAN KINGSTON AWASILI DAR
Sean Kingston tayari amewasili jijini Dar usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Nyerere International airport kwa ajili ya tuzo za kilimanjaro zinazotarajiwa kufanyika Kesho ijumaa … Sean Kingstone…. Atapewa nafasi ya kutumbuiza pia kutoa tuzo ya Wimbo bora wa RAGGA . baadhi ya wasanii watakao toa burudani kesho ni
AY. . Fid Q. . Joh Makini. . Marlow. . African Stars – Twanga Pepeta.
. Mwansiti. . Lady Jaydee. , Mzee Yusuph na Vijana kutoka ZANZIBAR wanaotesa na wimbo wao wa Bata na Ahmada Offside Trick Pia watakuwepo . Wahapahapa pamoja na Ali Kiba
MSHINDI WA KILIMANJARO MUSIC AWARDS KUPELEKWA SENEGAL NA MALARIA NO MORE
“ZINDUKA Malaria Haikubaliki” ni sehemu ya kampeni ya kitaifa iliyoanzishwa na Wizara ya Afya katika kupambana na malaria nchini. “The Kilimanjaro Music Awards” pamoja na “Malaria No More” mwaka huu, watampeleka nchini Senegal Msanii chipukizi atakaeshinda kinyang’anyiro cha kuwa “Msanii Bora Anaeyechipukia” kwenda kujionea na kujifunza shughuli azifanyazo mwanamuziki maarufu Youssou N’dou nchini humo katika kupambana na malaria.
Miaka 2 iliyopita, “Malaria No More” (Malaria Basi) iliungana na Taasisi ya mwanamuziki Youssour N’dou nchini Senegal katika kupambana na Malaria; na baadae mwaka jana waliungana na Mabalozi wa kupambana na malaria hapa nchini Tanzania katika kufikisha ujumbe kwa jamii usemao; “Malaria Haikubaliki na Tushirikiane Kuitokomeza”.
Msanii chipukizi atapata nafasi ya kuungana pamoja na Mabalozi wa Malaria No More Lady JD, Marlaw, Mwasiti, Bi Kidude, Banana na Prof Jay wakiwa kama mabalozi kuweza kusambaza ujumbe kwa jamii kwa nini jamii inatakiwa kujikinga dhidi ya malaria, kwa namna gani wantakiwa kujikinga na malaria na pia kwa namna gani wanaweza kupata matibabu pindi wanapokuwa wamepatwa na malaria.
Youssou N’dou ni moja kati ya wanamuziki wenye umaarufu mkubwa katika bara la Afrika, na hivi karibuni aliweza kufyatua wimbo maalumu juu ya malaria katika kuhamasisha uelewa juu ya malaria kwa jamii.
Youssou N’dou anaendesha shindano la kutafuta nyimbo bora ya Malaria amabyo fainali itakuwa ni tarehe 9 mwezi wa sita; ambapo mshindi wa kinyang’anyiro “Msanii Bora Anaeyechipukia” katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards ataenda kushiriki fainali hizo. Msanii pia atapata fursa ya kuweza kuona shughuli mbalimbali azifanyazo Youssou N’dou kupitia muziki wake na shughuli zote zifanyikazo Senegal katika kupambana na Malaria kwa ujumla.
Mshindi atarejea na kuungana na mabalozi wenginge nchini, kwa pamoja wataweza kushiriki katika kampeni za ZINDUKA Malaria Haikubaliki kwa mwaka unaofuata.
Wasanii hawa ndo wameteuliwa na Kilimanjaro Tanzania Music Awards katika kinyang’anyiro “Msanii Bora Aneyechipukia”; Quick Racka, Diamond, Belle 9, Barnaba na Amini.
ONA VIDEO MPYAA YA PUFF DADY NI NOMAAA
Dirty Money – Hello, Good Morning (Remix) (Feat. Rick Ross & Nicki Minaj) HOTT!!
Tuesday, May 11, 2010
TBL YAZIBORESHA ZAIDI TUNZO ZA KILI 2010
Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe, wakionyesha tuzo za kisasa zitakazotolewa na kampuni hiyo kwa wanamuziki bora wa mwaka huu kwenye mkutano uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye ofisi za kampuni hiyo.. Kwa mujibu wa Meneja amesema Tuzo za mara hii zitakuwa zz ubora . Anasema wamejitahidi kuziboresha ili ziwe nzuri na mvuto zaidi. Amesema kulingana na wakati na muda bc nilazima tuzo zenyewe ziwe na kiwango . Tuzo hizi zinatarajiwa kufayika keshokutwa 14.05.2010 Diamond Jubilee Hall
T I D ACHEZEA KICHAPO CLUB
Kwa mujibu wa blog yake ..T i D anasema hivi
Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari...nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI....naona MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.
shindano la ushairi kufanyika jijini dar
Mrisho Mpoto ambaye ni mshindi wa tatu wa mashindano ya Ushairi ya dunia 2009 yaliyofanyika nchini Ufaransa akiimba pamoja na wanakikundi wa Kempu ya Pambazuko Plus iliyoko Mbagala Charambe wakati alipokwenda kuongea nao juu ya kushiriki katika shindano la kuwatafuta wawakilishi wa shindano hilo katika visiwa vya Re-Union na hatimaye nchini Ufarasa yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Mrisho amekaribisha vijana mbalimbali wale wanaochipukia katika sanaa ya ushairi na kuwaambia kila kitu kinawezekana ila muhimu ni wao tu kujituma wakati watakapoingia rasmi katika shindano hilo litakalojulikana kama (Dar Poert Slam Competition) linalotarajiwa kufanyika tarehe 29 Mei kabla ya mchujo utakaofanyika tarehe 22 Mei na kuwapata washiriki 20 watakaoingia kwenye fainali.
Friday, May 7, 2010
DOWNLOAD - RICO SINGO NEW SONG
DOWNLOAD HIRE - SOME BODY REMIX - RICO SINGO
Baada ya kuachia some body oring sasa ni remix.. Ngoma hii itakuwa kwenye Album ya rico ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa 7. album tayari imekwisha kamilika ina ngoma kama 18. Mpaka sasa Album bado haijapewa jina,Pia Rico anatafuta wadhamini ambao wako tayari kufanya nao kazi katika uzinduzi wa album yake. Pamoja na kuingia sokoni. Kama wewe upo tayari kusimamia au kutoa msaada wa uzinduzi wa album au kuingia sokoni kwa album basi wasilina nae kwa Email ric_ko_2@hotmail.com Jamaa kwa sasa Yuko poa Yupo kikazi zaid... Haya wadau . Kijana huyo Tumpe support basi. Rico singo aka Rico love!!
Thursday, May 6, 2010
KUNA TAARIFA ZA UMEME KUTOKA TANGA KWENDA PEMBA HUENDA UKAFANYIWA MAJARIBIO HAPO KESHO.
Kuna taarifa za umeme kutoka Tanga kwenda Pemba huenda ukafanyiwa majaribio hapo kesho.
Kwa Mujibu wa taarifa zilizopatikana Kisiwani Pemba, zinadai kuwa Umeme wa kutokaTanga utafanyiwa majaribio hapo kesho, baada ya kuwepo kwa ahadi ya umeme huo kuwa tayari mwishoni mwa mwezi April.
Baada ya kupata taarifa hizo za awali ,ZENJIFM RADIO kama kawaida ulimtafuta Meneja wa Shirika la Umeme Pemba Salum Masoud ili kupata taarifa za uhakika juu ya majaribio hayo.Bonyeza HAPA kumsikia Meneja wa Shirika la Umeme Pemba.....Salum Masoud
TEMBELEA BLOG YA ZENJFM KUPATA HARARI ZA KILA SIKU 96.8 ZENJFM
http://www.zenjfm.blogspot.com/
HUYU NDIE BWAN CHUCHU, HUKU NDIKO ALIKOTOKEA SHOW KILA WIKI HADI KAMILIKI RADIO
Bwan chuchu. Ni mmoja kati ya wadau waburudani wasiosahaulika znz.. Jamaa alianza mbali sana. alikua akichakarika kutafuta hela. Show ilikuwa kila wiki znz. au hakuna show kama hakuna mkono wake chuchu. Ikafika hadi kumiliki bendi ya Chuchu sound. hakuridhika hadi kumiliki studio ya kwake Heart beat record. Mara tukasikia gazeti Ngoma moto. kwa sasa anakituo cha Radio Chuchu FM... bt umeona hiyo picha ? huko ndiko aliko toka jamaa
ONA HII PICHA HAWA NI 2 BERRY KABLA YA KUGOMBANA
ZANZIBAR LEO BONGE LA MVUA
Tokea kumekucha leo Zanzibar nzima hakutokeki. Mvua ni kubwa sana. Hapa ni maeneo ya kwa mchina . Mombasa.. Pia nimepata habari kuwa maeneo ya shamba ndio mvua kubwa sna . Haabari kamili utazipata kwenye blog yetu ya Radio . www.zenjifm.blogspot.com
KISA CHA MPEMBA COMEDY !!
……bruuum bruum bruuuum….
…taxi ya Kengeja inakuja….
…mbele kuna polisi wa trafiki….
……mara polisi akaisimamisha gari…..
Polisi: “assalaam alaykum nzee”
Dereva: “wa alayku nsalaamu”
Polisi: “nakushtaki……kushajua kosalo?”
Dereva: “abaa hadi sasa sijajua…..na kwanjionavyo leo sinakosa”
Polisi: “unzidisha abiria abaa…wakubaliana namie?”
Dereva: “yakhe mie sijazidisha….nionyeshe huyo ntu aliezidi humu”
Polisi: “gariyo inruhusiwa kuchukua watu wanne….hebu esabu watuwo n’wangapi?”
Dereva: “n’wanane”
Polisi: “kutokana hesabuyo huoni kama watu wanne wanzidi hapo?”
Dereva: “nasema tena abaa sijazidisha…ila weye wajua kusoma?….subiri ntoke huko nje”
….dereva akatoka nje ya gari….
Dereva: “soma hapa nlangoni panaandikwaje?”
Polisi: “licensed to carry four passengers”
Dereva: “ha unjua maanaye?”
Polisi: “ehee…..inruhusiwa kuchukua abiria wane….ndio nkakwambia unzidisha abaa”
Dereve: “zunguka na nlango wa huku…uje usome…”
……dereva na polisi wakazunguka mlango wa mbele wa pili wa gari…”
Dereva: “haya soma hapa”
Polisi: “licensed to carry four passengers”
Dereva: “haya abaa nne na nne n’ngapi?”
Polisi: “n’nane
Tuesday, May 4, 2010
DOWNLOAD BAD SKY NEW SONG
DOWNLOAD BAD SKY NEW SONG - LIFE YA KITAAA - BAD SKY
Mchizi anawakilisha kundi la A boys - kwa sasa wapo wawili Bad sky na Jackob B. Mwanzoni walikuwa watatu kabla ya J I kutimliwa kwenye kundi hilo. kwasasa A boys kila moja ana ngoma kali moja, Juzi nilikutanma nao wameniambia kwa sasa wanatarajia kuachia video yao Ijuliknayo kwa Usibadilike waliofanya na Chege. .Pia tayrai wamesharickodi ngoma ya Kundi inayitwa Nipe Chorus kupitia studio za Jupiter record. Ngoma hiyo itaachiwa mwezi wa saba .Msimu wa High season .
Monday, May 3, 2010
DOWNLOAD DORICA NEW SONG
DOWNLOAD HIRE - DORICA - CHAGUO LA MOYO WANGU
Mwana dada Dorika ameachia ngoma mpyaa inayoitwa Chaguo la moyo wangu, Ngoma hii imetengenezwa Akhenato Studio chini ya Producer Lil Getto. Wimbo huu upo katika style ya Zouk . Huu ni wimbo wa pili kuachia. Wimbo wa kwanza ulikuwa unaitwa Siwezi ambayo pia wimbo huo umerikodiwa kwenye studio hiyo hiyo ya Akhenato . Wimbo wa Siwezi ndio wimbo uliompatia tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike chipukizi 2009.... Sasa dorika yupo chini ya Akhenato Record. haya wadau kitu kipyaaa chengine cha Dorica kipo hewani ndo hichoo kipo bombaaaaa.. Anahitaji Promo ya Radio
DOWNLOAD METAYA NEW SONG
DOWNLOAD HIRE (Halla - Metaya ft Aron name_ RADIO PROMO
Metaya kwa sasa ana lebo pale jupiter record.. Ngoma imetengenezawa na Aron name ambae kwa sasa ndie Producer wa pale Jupiter...Album ya mchizi inatarijiwa kutoka ndani ya mwaka huu.Album inaitwa (Dunia stand) Ambayo ina ngoma kama 18. Wiki ijayo Metaya anatarajia kufanya Video ya ngoma hii Hallla .. Video atafanya chini ya Amstorng Dady pale pale Jupiter Record. Pia ameniambia tayari ameshaanza maandalizi ya kutaka kurokodi alburm ya Pili ..
NIMEPATA MZIGO MPYAA WA NGOMA KALI
Habari yako unaetembelea Blog hii. Karibu sana kwenye blog yangu . Nitakuwa naweka ngoma mpyaa za kibongo na zenji flava na zitakuwa zinapatikana kwa kudownload na hii ni kwa ajili ya Radio Promo tu. Zitakuwa kwenye quality nzuri sana. Leo nimeta Mpya kutoka kwa METAYA AKA SHOT GUN , MWANA DADA DORICA, BABY J ft Banana zoro. Kali sana zote. Nilikuwa niziweke zote bt Net Leo Ipo slow sana. Bt soon tu Nitaweka mzigo kwa ajli yenu.
Jambo la pili. Mimi ni Djs na nafatilia sana ngoma za Club vp wadau mnataka ngoma za mbele kaliiiii nikisema kali ni kaliii kwa ajili ya club au show za radio zinazokimpiza vijana vipi mnataka nazo niweke au bongo tu?
Tuwasiliane bc... djside_dj@yahoo.com. Ukiiipata kwenye blog hii tafadhali mwammbie na mwenzio nae aijue . Asante sana.
Sunday, May 2, 2010
FULL MOON PARTY KENDWA ROCK ILIKUWA NOMAA!!
Full moon party hii ilikuwa noma. Mambo yalikuwa hivi ..mpango mzima kwenye mashine nilikuwa mimi (Dj side) na Dj Dully kutoka pale pale kendwa rock. Bt mdna mwingi sana nilikuwa mimi kwenye mashine nikiwapa watu ladha . Muda wa kupumzika kidogo na kuenda chooni au kupata kinywaji ndio niikuwa nikimpa Dj Dully anishikie Kwani mimi hasa ndie Niliekuwa Dj hasaa wa usiku huu wa Full moon party .Watu walienjoy sana tena sana. Ngoma zote all around the world zilisikika . Nilihakikisha watu wote wanapata ladha .Kitu kizuri .tupo kwenye low season bt watu walikuwa wengi sana ..Wageni wa kila aina walikuwepo. kutoka DAR washkaji kibao walitia maguu. wazungu ndo usisemeee ndio kwao hasaa.
Kiufupi party ilikuwa mzuka sana.
Hawa jamaa ni Ma Djs kutoka U,K wakati nakamua hafla wakatokea kwenye sehem niliyokuwa nimetengewa kwa ajili ya Djs kutupa mawe. Nikawafungulia kijilango tukaanza kupiga story. Walijitambulisha Mmoja anaitwa Dj Ruuth. na Moja anitwa Dj Ellow. Walikuja wakawa na wao wamepandwa na mzuka na wao wanataka kukamua. bt wao watumie I phone yao. Niliiangalia Iphone yao nikawsetia Ili nione watafaya nini. Hapa walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya kuanza.
Hapa nilikuwa nampa Maelezo huyu Djs Ruuth kutoka U,k ambae midadi ilimpanda akataka kuja kukamua but kwa kutumia Iphone yake mwenyewe!
Hapa Nilikuwa nawasetia ili waweze kutumia I phone yao waweze kukamua. Walikuwaa wanataka Kupiga ngoma kwa kutumia Iphone yao Ambayo ilikuywa imejaa ngoma za Mbelee. Hawa jaamaa walinishanagza sanaaaa. Maana walipiga tungi mpaka basi .Pombe kwenda mbele . Walikuwa Djs wawili wote wanatoka Uk ..Kitu kilichonishangaza ni Kwamba Bada ya pirikapirika Iphone ya imerambwaa. Hata sijui imeibiwa vipi. Naona wanakuja kwa Djs akili imewaruka Pombe teleee kichwani anasikitika Iphone hawaioni wanasema imeibiwa na alie iiba hawamjui. Alichanganyikiwa kwa kweli Duu. Nikasema Tz bwana hm Noma . Jamaa hata hajui saa ngapi watu wameilamba Iphone aliyokuwa akitilia Unore.
Dance hall bwana nmaaa!!! we acha tu. Huyu jamaa alikua anajinyonga kama nyoka .Maana daaa kaz kwel kwel Hapa akicheza dance hall nilizokua nikizidondosha . Muda huu kila mtu alikuwa bizee kimpango wakee kimyaaaa watu wanakula copo. Ni ma pini kwenda mbele..Mwanzo mwisho!!
Hii ndo campany niliotoka nayo town kwenda Kendwa. huyu ni Mtangazaji mwenzangu Emy C hapa akionekana Bizeee akizirudi. step kwa step.. Unajua ilikuwaje hapa? Hm hapa alikuwa akicheza wimbo wa kiarabu Golo Golo ya Miami. Nilikuwa kwenye michine bt nilipenda style na jinsi alivyokuwa akicheza .Nilikuwa sijamuona bt nilisikia kwa mbali Dj sideee woooowww!!! Nilidhani amepanda shetani Kumbe ni midadi tu. Nikawa namuangalia anachezaje..!!! I say? Sijui kama hana makole ya kimanga kama mimi.
Kwanja limekolea Kila mtu yupo bize na kuzirudi .Watu walikuwa hawajitambui hapa Ulikuwa ni mda wa Techno na House... Ukiona hiyo Picha inakwambia hasaa watu wapo bize kuzirudi . Halafu raha ya party hii ilikuwa na mchanganyiko wa watu tofauti. Wazungu , waarabu. wahindi. wachina. na African ndo usiseme . watu walikuwa nyomi sana
Hawa ni jamaa wa sarakasi wakifanya maajabu yao. Jamaa wanaitwa Jambo Brother wanapatikana hapa hapa znz .Ni waruzi sana na wana mvuto hasa. Kiufupi jamaa kwenye sarakasi wanaweza . Walifanya mambo mengi sana lakin kali zaid ilikuwa Kula moto. Duu Hii ilikuwa nomaa. Pamoja na mtu moja kuwabeba watu sita kwa wakati mojaa. Huwez kuamini bt ni kweli na ni Mambo ya sarakasi .
Pichani Hapa naoneka nikiwa Bizee naset mapini..Kiufupi party jana ilikuwa mzuka sana.Watu waliruka kwanja wasizozitarajia.. Nilicheza ngoma all around the world ... Kila aliefika pale alipata ladha. Ma mix kama kawa! hakuna kutoka nje ya biti wala kupopoa maembee. Raha mwanzo mwisho ladha zote..Nilihakikisha hatoki mtu kwenye Dance floor ila kwa kupata kinywaji au kupumzika. Show ilianza Saa 2 hadi saa 4 tuka break kidogo kwa kuangalia Sarakasi kutoka kwa Kikundi cha Jambo Brother Acrobat show. Ambao na wao walifanya vizuri sana. Kama saa 5 na 30 nikaanza Kushusha mizinga . Jiwe juu jiwe hadi kumi na moja asubuhi. kweupeee bado watu wanaruka kwanjaa..
Shukran zangu za dhati kwa wale wote waliofika kwenye paty. Kulikuwa na jamaa kibao kutoka Dar Nimegundua kweli watu wanapenda burudani .Wazungu ndo usiseme ..
Ni hayo tu .
Subscribe to:
Posts (Atom)