Tuesday, May 11, 2010

shindano la ushairi kufanyika jijini dar


Mrisho Mpoto ambaye ni mshindi wa tatu wa mashindano ya Ushairi ya dunia 2009 yaliyofanyika nchini Ufaransa akiimba pamoja na wanakikundi wa Kempu ya Pambazuko Plus iliyoko Mbagala Charambe wakati alipokwenda kuongea nao juu ya kushiriki katika shindano la kuwatafuta wawakilishi wa shindano hilo katika visiwa vya Re-Union na hatimaye nchini Ufarasa yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mrisho amekaribisha vijana mbalimbali wale wanaochipukia katika sanaa ya ushairi na kuwaambia kila kitu kinawezekana ila muhimu ni wao tu kujituma wakati watakapoingia rasmi katika shindano hilo litakalojulikana kama (Dar Poert Slam Competition) linalotarajiwa kufanyika tarehe 29 Mei kabla ya mchujo utakaofanyika tarehe 22 Mei na kuwapata washiriki 20 watakaoingia kwenye fainali.

No comments: