Tuesday, May 18, 2010
CHID BENZ MIKONONI MWA POLISI LEO
Msanii bora wa hip hop wa tuzo za Kili Music Awards 2010,Chid Benz mapema leo mchana emetiwa mIkononi na polisi maeneo ya Kilwa Road mara baada ya kudaiwa kuingilia msafara wa kiongozi mmoja aliyekuwa akipita eneo hilo, Polisi wa usalama barabarani wakamtia Chid Benz mokononi huku wakimhoji ni kwa nini ameingilia msafara, Kwa mujibu wa shuhuda Chid Benz amedai kutukanwa tusi zito na mmoja wa polisi wa usalama barabarani ndio kukaibuka patashika hilo ,kufuatia vute nikuvute hiyo Chid Benz akaamua kwenda kutoa taarifa ya kutukanwa kwenye kituo cha Kilwa road. Haya wadau. Kazi hiyo. Maana polisi anasema chid kaingillia msafara wa mkubwa wa nchi. Na Chid nae anasema katukanwa tusi kubwaa.. Mambo yatakuwaje hapa...? Sisi letu jicho tu tusubiri sheria ichukue mkono wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment