Sunday, May 16, 2010

DAIMOND AFUNIKA TUZO ZA KILI 2010


Daimond mwaka huu amchukuwa tuzo 3 kwa Mpigo. Tuzo ya Wimbo bora wa R&B na Msanii Bora chipukizi wa mwakaa. na Wimbo Bora wa Mwaka. (Kamwambie)
The Kilimanjaro Music Awards” pamoja na “Malaria No More” mwaka huu, watampeleka Senegal Msanii chipukizi Diamond kwenda kujionea na kujifunza shughuli azifanyazo mwanamuziki maarufu Youssou N’dou nchini humo katika kupambana na malaria,na namna gani wanatakiwa kujikinga na malaria na pia kwa namna gani wanaweza kupata matibabu pindi wanapokuwa wamepatwa na malaria

Daimond ambaye ndiye Msanii chipukizi atapata nafasi ya kuungana pamoja na Mabalozi wa Malaria No More Lady JD, Marlaw, Mwasiti, Bi Kidude, Banana na Prof Jay wakiwa kama mabalozi kuweza kusambaza ujumbe kwa jamii kwa nini jamii inatakiwa kujikinga dhidi ya malaria,

TUZO ZILIKUWA KAMA HIVI

Mwimbaji bora wa kike
Lady Jaydee

Mwimbani bora wa kiume
Banana Zoro

Albamu bora ya taarab
Daktari wa Mapenzi -Jahazi Mordern taarab

Wimbo Bora wa Taarab
Daktari wa Mapenzi – Jahazi Morden taarab

Wimbo bora wa Kiswahili
Mwana Dar es Salaam – African Stars Band

Albam bora ya Bendi
Mwana Dar es Salaam - African Stars Band

Wimbo bora wa R&B
Kamwambie -Diamond

Wimbo bora asili ya kitanzania
Nikipata nauli - Mrisho Mpoto

Wimbo bora wa Hip Hop
Stimu zimelipiwa - Joh Makini

Wimbo bora wa Reggae
Leo (Reggae remix) -AY

Wimbo bora wa Raga
Bwana misosi - Mungu yuko Bize

Rappa bora aw mwaka (Bendi)
Chokoraa

Msanii bora wa Hip-Hop
Chid Benzi

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Haturudi nyumba - Kidumu FT. Juliana

Mtunzi bora wa nyimbo
Mzee Yusuf

Mtayarishaji bora wa nyimbo
Lamar

Video bora ya muziki ya mwaka
C Pwaa – Problem

Wimbo bora wa Afro Pop
Pii pii (Missing my baby)

Msanii bora anayechipukia
Diamond

Wimbo bora wa kushirikiana
Nipigie -AT-Stara Thomas

Wimbo bora wa Mwaka
Kamwambie -Diamond

WALK OF FAME
1. ZAHIR ZORRO
2. CLOUDS FM

No comments: