Thursday, May 13, 2010
MSHINDI WA KILIMANJARO MUSIC AWARDS KUPELEKWA SENEGAL NA MALARIA NO MORE
“ZINDUKA Malaria Haikubaliki” ni sehemu ya kampeni ya kitaifa iliyoanzishwa na Wizara ya Afya katika kupambana na malaria nchini. “The Kilimanjaro Music Awards” pamoja na “Malaria No More” mwaka huu, watampeleka nchini Senegal Msanii chipukizi atakaeshinda kinyang’anyiro cha kuwa “Msanii Bora Anaeyechipukia” kwenda kujionea na kujifunza shughuli azifanyazo mwanamuziki maarufu Youssou N’dou nchini humo katika kupambana na malaria.
Miaka 2 iliyopita, “Malaria No More” (Malaria Basi) iliungana na Taasisi ya mwanamuziki Youssour N’dou nchini Senegal katika kupambana na Malaria; na baadae mwaka jana waliungana na Mabalozi wa kupambana na malaria hapa nchini Tanzania katika kufikisha ujumbe kwa jamii usemao; “Malaria Haikubaliki na Tushirikiane Kuitokomeza”.
Msanii chipukizi atapata nafasi ya kuungana pamoja na Mabalozi wa Malaria No More Lady JD, Marlaw, Mwasiti, Bi Kidude, Banana na Prof Jay wakiwa kama mabalozi kuweza kusambaza ujumbe kwa jamii kwa nini jamii inatakiwa kujikinga dhidi ya malaria, kwa namna gani wantakiwa kujikinga na malaria na pia kwa namna gani wanaweza kupata matibabu pindi wanapokuwa wamepatwa na malaria.
Youssou N’dou ni moja kati ya wanamuziki wenye umaarufu mkubwa katika bara la Afrika, na hivi karibuni aliweza kufyatua wimbo maalumu juu ya malaria katika kuhamasisha uelewa juu ya malaria kwa jamii.
Youssou N’dou anaendesha shindano la kutafuta nyimbo bora ya Malaria amabyo fainali itakuwa ni tarehe 9 mwezi wa sita; ambapo mshindi wa kinyang’anyiro “Msanii Bora Anaeyechipukia” katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards ataenda kushiriki fainali hizo. Msanii pia atapata fursa ya kuweza kuona shughuli mbalimbali azifanyazo Youssou N’dou kupitia muziki wake na shughuli zote zifanyikazo Senegal katika kupambana na Malaria kwa ujumla.
Mshindi atarejea na kuungana na mabalozi wenginge nchini, kwa pamoja wataweza kushiriki katika kampeni za ZINDUKA Malaria Haikubaliki kwa mwaka unaofuata.
Wasanii hawa ndo wameteuliwa na Kilimanjaro Tanzania Music Awards katika kinyang’anyiro “Msanii Bora Aneyechipukia”; Quick Racka, Diamond, Belle 9, Barnaba na Amini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment