Friday, May 21, 2010

ZANZIBAR MUSIC AWARDS 2010 IMEWADIA


Manager wa Zenji Entertainment Ndugu Seif Mhmed Seif akizungumza na waandishi wa habari .Katik ukumbi wa habari maelezo. Hapa ilikuwa anataja majina ya washiriki walifanikiwa kuingia kwenye kinyanganyiro cha Tuzo .


HABARI KWA WAANDISHI WA HABARI


Asalamu alleykum ndugu zangu waandishi wa habari
Awali ya yote kwanza na mshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uhai na uzima kwa kukutana leo hapa, pili nikushukuruni nyinyi wandishi wa habari kwa kuacha majukumu yenu mengine kwa kuitika wito wetu huu na kuwa nasi katika mkutano wetu huu.
Pia napenda kuwashukuru wenyeji wetu wa mkutano huu idara ya habari maelezo Zanziar kwa kutupatia sehemu hii ya kufanyia mkutano wetu huu.
Ndugu zangu waandishi wa habari Lengo la kukutana kwetu ni kuelezea matayarisho ya tamasha la tano linalofanyika kila mwaka Zanzibar la utowaji wa tunzo za wasanii bora wa mwaka Zanzibar kwa mwaka 2010 ili nanyi taarifa hizi muzifikishe kwa wananchi kupitia vyombo vyenu tofauti.

Ndugu zangu wandishi wa habari tamasha la utowaji wa tunzo ya mwanamuziki bora Zanzibar zinatarajiwa kutolewa tarehe 26 June mwaka huu katika ukumbi wa Salama Hall wa hoteli ya Bwawani ambapo tamasha hili linatarajiwa kuwa la aina yake ikilinganishwa na matamasha mengine manne tulioandaa miaka iliyopita.

Tamasha hili linaandaliwa na kampuni ya habari Zanzibar Zanzibar Media Coperation kupitia kitengo chake cha Zanzibar Entertainment kwa lengo la kuinua vipaji vya wasaanii wetu wa Zanzibar na kuvienzi kwa kazi kubwa wanazozifanya ili waweze kuleta ushindani katika soko la kazi zao za sanaa na hatimae kufaidika kimapato na kazi zao hizo.Pia ni chachu ya kuwainua wasanii wetu

Ndugu zangu waandishi wa habari tuelewe kwamba Zanzibar imo katika mipango ya kuingia katika soko la pamoja la nchi wanachama wa Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki hivyo fani ya sanaa inaweza kuwa sekta muhimu kwa nchi wanancha kama ni sehemu kubwa ya ajira kwa raia wa nchi hizo. Hivyo kuwepo na matamasha kama haya kutawasaidia wasanii wa Zanzibar kukuza na kuibua vipaji vyao ili waweze kuleta ushindani katika soko hilo na masoko mengine ya kimataifa na pia kuitangaza Zanzibar katika medali za sanaa na ubunifu.

Ndugu zangu waandishi wa habari pia tamasha letu la utowaji wa Tuzo za wanamuziki bora wa Zanzibar linaweza kuisaidia nchi yetu kuitangaza sekta ya utalii Zanzibar na hatimae kuingiza watalii wengi ambao wanasaidia kukuza pato la taifa. Hili linawezekana kwani vyombo vyenu na vyombo vingine vya kimataifa hurusha hewani matangazo ya tamasha letu katika nchi nyingi duniani ambayo yataonyesha mitindo ya wanamuziki wetu.



Ndugu zangu wandishi wa habari tamasha la utowaji wa tunzo mwaka huu litahusisha utowaji wa tunzo katika sanaa zaidi ya kumi na sita hii ikiwa pungufu kidogo ukilinganisha nay a mwaka jana lengo ni kuboresha tamasha hili pekee ndani ya visiwa vya Zanzibar . Tunzo zitakazogombania ni kutoka fani taarab ya kisasa,taarab asilia,muziki wa kizazi kipya,ngoma asilia pia album bora.
Washiriki wa tunzo hizo wataanza kupigiwa kura kuanzia kesho tarehe 22 hadi tarehe 23 mwezi ujao mwaka huu ikiwa ni matokeo ya mchujo wa awali uliofanya na magwiji wa fani za muziki . Jinsi ya kuyapigia kura majina ya washiriki na kazi zitakazopigiwa kura ni kila mshiriki amepewa no maalum kwa ajili ya kupigiwa kura kwa kila kipengele hivyo unachotakiwa kwa mwananchi kuandikia nambari alionayo msanii kisha kutuma kwenda 0655 968 968 .
Matangazo na jinsi ya kupiga kura utasikia kupitia redio mbali mbali na pia utaweza kupiga kura kupitia kuponi ndani ya gazeti la kila wiki la nipe habari.
Ndugu zangu waandishi wa habari tamasha hilo pamoja na utowaji wa tunzo linatarajiwa kugharimu zaidi shilingi milioni 24 za Kitanzania fedha ambazo zinatokana na michango ya wafadhili wetu wa ndani.Hata hivyo milango la wafadhili bado iko wazi tunawakaribisha .
Kabla ya kumaliza hutuba yangu naomba niwashukuru tena ndugu zangu waandishi wa habari kwa kunisikiliza kwa makini na naomba kutoa fursa ya kuuliza masuala pale panapohitajika ufufanuzi zaidi
Baada ya maelezo haya nitaruhusu zitolewe nakala za mchako wa wasanii walipita katika kila kipengele .
Ahsanteni kwa kunisikiliza .



SEIF MOHAMMED SEIF
MENEJA
ZENJI INTERTAINMENT
zenjientertainment@yahoo.com

No comments: