Saturday, June 5, 2010

HATIMAE CHUCHU AZIKWA LEO


Hali ndivyo ilikuwa kama unavyoona picha hiyo hao ni baadhi ya watu waliojitokeza kuusindikiza mwili wa Marehe Yussuf Alley Almaarufu Bwanchuchu


Mamia ya wananchi na wasanii nchini jioni hii wanahudhuria mazishi ya msanii maarufu wa Zanzibar Yusuf Ahmed Alley maarufu bwan’chuchu katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya magharibi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari Marehemu Chuchu amefariki dunia mjini Nairobi, Kenya alikopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kuugua kiasi ya mwezi mmoja uliopita.

Mwili wa msanii umerejeshwa mjini hapa ambapo taratibu za mazishi zilifanyika katika mtaa wa Kisima Majongoo na maziko yanafanyika jioni hii katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya magharibi.

Marehemu Chuchu atakumbukwa kwa uhodari wake katika muziki hasa alipounda bendi ya Chuchu Sound iliyotamba kwa vibao vyake na chapuo za mazungumzo kati yake na Omari Mkali yaliyokuwa yakihitimishwa na neno la ‘ee! kwaheri’.

Marehemu chuchu pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya tamasha la kila mwaka la Sauti za busara na pia alikuwa anamiliki kituo cha redio cha Chuchu Fm kiliopo mjini hapa na studio ya kurekodia muziki.

Marehemu Chuchu aliefariki akiwa na umri wa miaka 51 ameacha mke mmoja ambae kwa sasa yuko nchini Marekani.

Uongozi wa Flava DJs na Zenji Fm Radio unatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu.

Mungu amlaze mahali pema peponi AAMIN


Miongoni mwa walioguswa na kifo chake waliamua kwenda kuupokea mwili wa marehemu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar.Kama kawaida ya Zanzibar kuna usafiri wa aina nyingi miongoni mwao ni vespa kama tunavyomuona jamaa hapo akiwa kwenye foleni ya kuusubiri mwili wa marehemu




Hatimaye ule wakati ulifika,ndege iliyobeba mwili wa Bwanchuchu ikawasili uwanja wa ndege wa Zanzibar kama tunavyoona hapo taratibu ndege hiyo ikitua.



Vilio na simanzi vilitawala uwanja wa ndege na hasa baada ya kufunguliwa kwa mlango wa ndege hiyo kama tunavyoona pichani baadhi ya ndugu wa marehemu hapo wakibubujikwa na machozi baada ya kipenzi chao kuwasili akiwa katika hali nyengine tofauti na ile tuliyoizowea, hapo ni maiti sasa.



Hawa ni miongoni mwa watu waliobaki nje kabisa wakiusubiri mwili wa marehemu.



Wengi hatukuamini lakini ndio hivyo kazi yake mola haina makosa, lakini mapaparazi kama kawaida yao huwa hawakosekani katika sehemu kama hizi kama unavyomuona jamaa huyo akihangaika na camera yake kuhakikisha kuwa anapata kumbukumbu nzuri ya kifo cha Bwanchuchu.



Safari ya kumpeleka mpendwa wetu ilianza kueleka makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.




Kila mtu alitamani kuligusa jeneza la marehemu wakubwa kwa wadogo agalau kuonesha heshima kwa mwenzetu aliyetangulia mbele ya haki.



Hakika ilikuwa ni huzuni kubwa kwa wadau mbali mbali wa habari na muziki nchini,hapo kwenye picha ni miongoni mwa wadau hao wakitafakari na kutoamini kilichotokea kutokana na ukarimu na ucheshi wa Bwanchuchu kwa kila mtu.

2 comments:

Unknown said...

Inalillah wa ina ilaihi rajiun

juerji said...

most of ur story's u dnt write a date son kama story hii ya chuchu hukuandika tarehe aliyofariki