Sunday, May 23, 2010

JUNE JULY VIDEO JUMA 20 NEW VIDEO



Juma 20 hatimae ameachia video ya ngoma yake iitwayo June July ..Video hii imetengenezwa pale Jupiter Record .Amstrong Dad ndie alie itengeneza ... Nilikuwa naongea na Juma wakati ananipa habari juu ya hii video yake mpyaa . alinitumia sms na tukawa tunachart Juma 20 alianza kwa kunitumia sms isemayo

Juma 20 ... Najua Dj side hautonijibu but angalia video yangu ya JUNE JULLY katika Wall ya facebook yangu, comment then nambie lini niilete uirushe kwenye blog?
Mimi nilimjibu ok bt nilimuuliza whats yr target ya kutoa video ya june jully nw?
Juma 20 alijibu kwa kusema
Target yangu ni kuzidi kujitambuslisha katika anga za kimataifa ,kupata show ,pia kujinadi katika tuzo za ZANZIBAR MUSIC AWARDS .. Wimbo wangu mpya unaitwa KIBAJAJI utafuata.

Niliendelea kumuuliza masuali juma 20 suala lilifuata lilikuwa kama ifuatavyo-

2009 mwezi wa june umeachia wimbo wa june jully ..Mwaka 2010 karibu na june jully umeachia video yake Jee? 2011 mashabiki wako watarajie movie ya june yully au sires?

Juma alijibu kwa kusema -

Hii inaoneha jinsi gani nisivyo na papara na kazi zangu zinaenda na wakati nimefunga ukurasa wa june jully nadhan hakuna wimbo kama huu duniani.

Mimi nikamwambia sijaridhika na jibu jeee? mwakani kuna movie ya june jully?

Juma alinijibu kwa kusema

Mbona nilishakupa jibu kwamba kama ni kitabu basi chapter ya june july imeipita labda November December tena but sitaongelea au kuigiza tena kuhusu tittle hiyo

Nilienedlea kumuuliza Juma 20 na suala lililofuta ninikuwa kama ifuatavyo

Sauti yako imetumika sana katika wimbo wa umoja wa zaznibar ..Hivi una mpango wowote wa kutumia picha yako katika kampeni ya chama tawala cha ccm katika kampeni ya uchaguzi Ili kuhamasisha chama tawala kiendelee kukaa tena madarakani ?

Juma alijibu kwa kusema

Actual mimi si mwana siasa , ni mwanamuziki, na mfano wa kuigwa kimavazi, mitindo ya ndevu na style za nywele , nina nafasi kubwa ya kutambulika kimwili(personalty) kuliko mtu ambae inatakiwa kusikika sauti yake tu pasipokua na haja kuonekana sana

Suala la mwisho kumuuliza Juma 20 ilikuwa gumu sana kwake kwani alichukuwa takriban dakika 5 hadi kinijibu. suala lilikuwa kama ifutavyo

Ricky martin hatimae juzi juzi amekiri kama yeye ni Homosexual baada ya kuficha kwa mda mrefu. Unalizungumzia vipi suala hili kiupande wako ili kuwatoa hofu mashabiki wako kwani kumekuwa na uvumi mkubwa kutoka kwa mapaparazzi kuwa unapenda kujichanganya na watu wa aina hiyo??

Baada ya nukta kazaa za ukimyaan Juma alijibu kwa kusema

Mimi ni rais katika dunia yangu ya mziki Gender si suala ninaloliangalia sana linapokuja suala la marafiki, viongozi , mashoga, mapaparazi, watanagazaji mashoga. Nitajuaje nani yumo nimtenge nani hayumo awe rafiki yangu its ridiculous

Sikuridhika na jibu lake lakini any way nitaendelea kumdig mpaka anianikie aweke mambo hadharani. Kwani hapo juu ameonekana kujitetea kimtindo but hakujibu suali sauli langu.

Ni hayo tu

Angalia video sasa . comments muhim

5 comments:

Anonymous said...

Hongera juma20 kwa video yako ya june july ingawa mimi niliona ktk face book.
na kuhusu mashoga umeongea ukweli, kwa sababu siku hizi watu wana wake zao na stil wana tabia hizo na hawajuulikani, so huna makosa kwa kuwa na urafiki na watu coz hujui nani shoga nani rijali

Anonymous said...

MBONA SIONI VIDEO YA JUNE JULY?

Huyo muandishi hajatulia, sasa utajuaje ktk hao washabiki anaosema wana wasi wasi nani shoga nani si shoga? miongoni mwa wanaosikiliza muziki ni mashoga na wasagaji, na hao hao ndio wanaoipiga kura na kukunua kazi za muziki.

Anonymous said...

video haionyeshi, kulikoni, hahaha sasa naona munamlazimisha star kusema kitu kile mungelipenda musikie? stricly ushoga ni tabia ya mtu, na zamani mashoga walikua wakijipaka poda na wanja na ilikua wanatengwa lkn kweli siku hizi mabosi ndio mashoga, ukiwatenga utakula wapi? mashoga wa siku hizi huwezi kujua maana wana sauti base kama ya ndugu muandishi..

Anonymous said...

CONGRATULATIONS KWA VIDEO YA JUNE JULY UR THE BEST

Anonymous said...

CONGRATULATIONS KWA VIDEO YA JUNE JULY UR THE BEST

LOL..NIMEGUSWA NA HILO SUALI LA RICKY MARTIN, SIJAELEWA MUANDISHI ANATAKA 20 AISHI KAMA RICKY MARTIN AU VIPI?
MAISHA YA LEO KWELI UTAISHI BILA KUONGEA NA HAWA WATU? UKIMSEMA MWENZAKO KWA KITU CHOCHOTE JUA KWENU PIA KIPO AU KILIKUWEPO