Wednesday, May 4, 2011
TMK KUJA NA MOVIE YA PAMOJA
Makundi mawili yaliyohasiana ya miondoko ya kizazi kipya toka pande za Temeke,TMK Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi wanatarajiwa kutoa movie la pamoja
Movie hilo linatarajiwa kuwaunganisha mahasimu hao,ambao awali walikuwa kundi moja na kufanya kazi kadhaa wakiongozwa na Meneja wao Said Fella ambaye kwa sasa anasimamia kundi la TMK Wanaume Family
Kwa sasa Maandalizi ya filamu hiyo yanaendelea ambapo wanakamilisha hatua ya kuandaa mwongozo utakaochukua wiki mbili hadi kukamilika kwake,na lengo la kuandaa filamu hiyo ni kuelezea historia ya wanamuziki wa kundi hilo,toka walikotoka katika safari yao ya muziki hadi walipofikia sasa
Wanamuziki wote wa makundi hayo watashiriki bila kubagua pia shughuli za kuunganisha miziki iliyokwisharekodiwa awali na studio hiyo inatengenezwa kwa ajili ya kuingizwa katika filamu hiyo kama soundtrack
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment