Wednesday, May 4, 2011

YAJUE MAMBO 10 YA OSAM A BIN LADEN




1- Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden aka Osama bin Laden alizaliwa tarehe 10 March,1957 Riyadh-Saudi Arabia,akiwa ni mtoto wa 17 kati watoto 57 kuzaliwa toka kwa baba yake Mohammad bin Laden,tajiri-bilionea na mama yake Hamida Al-Attas anayetokea Syria alikua ni mke wa 10 kwa baba yake!

2 - Baba yake Mohammed bin Laden alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1967,baada ya pilot wa kimarekani kufanya makosa wakati wa kutua na kumuachia Osama Bin Laden urithi wa dola milioni 80 akiwa tu na miaka 11

3 - Osama Bin Laden alikua ni muanzilishi na kiongozi wa kundi la Al-Qaeda mwezi August 1988 - 1989na alisomea Economics na business Administration kwenye Chuo cha King Abdulaziz na inasemekana kuwa alipata degree ya Civil Engineering in 1979,au degree ya Public Administration mwaka 1981!

4 - Kuanzia mwaka 2002 Osama bin Laden alioa wake 4 na anakadiriwa kuwa na watoto 25 mpaka 26!

5 - Jeshi la Marekani lilimtafuta osama Bin Laden kwa miaka 10,lakini kikosi cha watu 20–25 toka US Navy Seals aka Seal Team Six lililoitwa 'Geromino' liliwachukua dakika 40 tu kabla ya kumuua kwa kumpiga risasi kichwani na kifuani!

6 - Wakati wanajeshi wa Marekani wanavamia nyumbani kwa Osama,Rais Barack Obama alikua anaangalia live kupitia real time video,mishe mishe zote za kuuwawa kwake!

7- Nyumba aliyokua anakaa pande za Abbottabad ilikua ina thamani ya dola milioni 1 za kimarekani,lakini eneo lililokuepo ilikua ni nyumba mbaya kati ya 40 zilizokuepo pande hizo,usioitegemea kama inaweza ikawa makazi ya mtu,isiyokua na mawasiliano ya simu wala internet!

8 - Majirani zake pande za Abbottabadd walikua hawajui kuwa Osama alikua anaishi eneo hilo coz nyumbani kwake kulikua kumetulia sana,na baada ya kuona kuwa kusikia milio ya risasi,waliamua kuwasha TV na kushangaa kuona Rais Obama akitangaza kuwa Osama ameuliwa eneo lao wanaloishi!

9 - Baada ya kutangazwa kuwa ameuwawa,mtandao wa twetter uliweka historia,Jumapili ya tarehe 01 May,2011 kwa kupata tweeter sms 3,440 kwa sekunde!

10 - Baada ya kutangaza kuwa ameuwawa Rais Obama aliandaa dinner na alipewa 'standing ovation' (wakati anaingia watu walikua wameshakaa na wakasimama na kumshangilia kwa kumpigia makofi) kwenye ikulu ya White House na kuwapongeza mashujaa waliomuua Osama Bin Laden!

No comments: