Tuesday, April 13, 2010

WITO KWA WASANII WANOATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2011


Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote.

Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 280 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jose Chameleone, Samba Mapangala, Saida Karoli, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate,Banana Zorro & the B Band, Joh Makini, Nako2Nako Soldiers, Nyota Ndogo,Thandiswa, Culture Musical Club na wengineo wengi.

MWISHO wa kupokea maombi
31 July 2010

Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri , malazi,chakula na matumizi madogo madogo.Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri

Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa
Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi kutoka kwako kabla ya MWISHO wa kutuma maombi. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:

* form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
* nakala moja au mbili ya kazi zako (CD au DVD)
* picha moja au mbili( JPG au karatasi)

Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo

Busara Promotions, PO Box 3635, Zanzibar, Tanzania au Email busara@zanlink.com
Tel: +255 24 223 2423 or +255 784 925 499 or +255 773 822 294

(Form inaweza kujazwa kupitia mtandao wa intenate) http://www.busaramusic.org/
au http://www.busaramusic.org/callforartists/2011e.php

No comments: