Thursday, May 20, 2010

COSOZA YAFANYA OPERESHENI KALI KATIKA MADUKA YA CASET ZNZ


Afisi ya haki miliki leo imefanya uperesheni maalum katika maduka yanayokodisha na kuuza Keseti ambayo hayajafanyiwa malipo kwa ajili ya kuendesha biashara ya sanaa katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Zanzibar.
Akizungumza katika Oparesheni hiyo msimamizi na mtendaji mkuu wa afisi hiyo Mtumwa Khatib Khamis amesema lengo la Oparesheni hiyo ni ni kuhakikisha haki za wasanii na wabunifu zinapatikana na kuwashajihisha wafanya bishara kuzitumia kazi za sanaa kihalali.
Amesema biashara ya sanaa imekuwa ikiwanufaisha wafanyabiashara pekee lakini wabunifu asili hawafaidiki vyema na kazi zao.
Msimamizi huyo amesema afisi yake imetoa elimu kwa wananchi na wafanya biashara wa kazi za sanaa kwa muda wa miaka mitatu sasa ili kujisajili na kufanya malipo lakini baadhi ya wafanyabishara hao wameonekana kudharau juu ya hatua hiyo…
Oparesheni hiyo imefanyika katika maeneo ya Amani,Mpendae,Amani Fresh,Melinne ,meli tano ,kwa alinatuu na mali zilizokamatwa zinatarajiwa kuaangamizwa na afisi hiyo.
Jumla ya wafanyabiashara wa madula ya keseti 65 wamejisajili katika afisi hiyo kati ya hao wafanyabishara watano tuu ndio waliolipa kazi za sana hiyo.Opereresheni hiyo itakuwa endelevu ilikuhakikishwa wasanii wananufaika na akazi zao. Maduka kazaa yamekamatwaa ....

No comments: