Sunday, January 31, 2010

BEBE COOL ASHAMBULIWA KWA RISASI


Mwanamuziki mashuhuri wa reggae nchini Ugandan, Bebe Cool a.k.a Moses Sali, akiingizwa katika hospitali ya Nsambya jijini Kampala baada ya kupigwa risasi katika klabu moja jijini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la The Monitor, risasi hizo zimevunja miguu yote miwili, amesema Daktari Mrakibu wa hospitali hiyo, Dk. Martin Nsubuga says.
Habari zinasema risasi zilirindima katika klabu ya Effendys katika maeneo ya Centenary Park, na kwamba kuna utata wa sababu zilizopelekea purukushani hilo. Inasemekana watu wengine watatu ikiwa ni pamoja na mabaunsa wa Bebeb Cool na askari wa kikosi maalum pia walijeruhiwa.

No comments: