Friday, January 8, 2010

UMEME ZANZIBAR HADI FEBRUARY 20


Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja inatarajiwa kurejea tena baada ya siku 43 kuanzia leo kutokana na kuhitaji matengenezo yenye utaalamu wa hali ya juu.

Waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema matayarisho ya matengenezo hayo yameshakamilika na kinachosubiriwa ni vifaa vya kuchongesha kutoka Sweedena na Afrika ya Kusini vinavyotarajiwa kuwasili tarehe 20 mwezi huu.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema matengenezo hayo yatafanyika katika vituo vya kuchukulia na kupokelea umeme vya rasi Kiromoni Tanzania bara na Fumba kwa Unguja.
Waziri Mansour amesema umeme huo utaanza kuwashwa tarehe 20 mwezi ujao na majaribio yatafanyika tarehe 18 na 19 Akizungumzia uwezekano wa majenerata ya akiba, waziri Mansour amesema wizara inaendelea kufanya upembezi yakinifu ya ununuzi wa majanareta hayo.
Hata hivyo amesema serikali ya Norway imeonesha nia ya kukubali kugharamia ununuzi wa majenerata hayoHuduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja ilikatika tokea Desemba 10 mwaka jana na kusababisha usumbufu kwa wananchi ikiwemo uhaba wa maji safi na salama. Bonyeza hapa kumsikia waziri akizungumza na waandish wa habari (Waziri)

No comments: